raiamwematz24
Member
- Dec 6, 2025
- 8
- 20
Demokrasia inahitaji sauti huru na uwajibikaji wa viongozi lakini pale ambapo kundi la vijana linageuka kuwa mashabiki badala ya walinzi, misingi hiyo taifa na misingi imara ya demokrasia huanguka taratibu.
“Viongozi wanajua wakifanya kosa, watatetewa. Wapinzani wakisema ukweli, watashambuliwa. Hiyo si siasa ya demokrasia, ni udikteta wa kimyakimya unaovumiliwa,” alisema mchambuzi wa siasa.
Kwa mtazamo wake, “uchawa” umeua dhana ya uwajibikaji wa kijamii. Vijana badala ya kuhoji bajeti, mikopo au ubadhilifu, sasa wanahoji nani anaongea vibaya kuhusu kiongozi wao.
Baada ya kufanya uchunguzi wangu huru kupitia maandamano yaliyogeuka vurugu yaliyotokea tarehe 29, Oktoba 2025 hapa nchini Tanzania kwa namna moja yalisababisha uharibifu mkubwa wa mali na biashara.
Ni wazi kabisa wapo waliokutwa wakiwa hawana hatia lakini baadhi ya biashara zilizoharibiwa ziliwagusa vijana baadhi waliokuwa machawa wa Wanasiasa.
Duka la simu (Nenga Tronics) la kijana msanii William Nicholaus Lyimo “Billnass” lilivunjwa na kuharibiwa na kusababisha upotevu wa mali zote ndani ya duka hilo.
Upande mwingine pia msanii mwanadada Zena Yusuf Mohammed maarufu kama Shilole alipoteza mgahawa wake unaofahamika kwa jina la Shishi Food baada ya kundi la vijana hao kuchoma moto na kuteketeza kila kitu.
Kwa mtazamo wangu baada ya kufanya uchunguzi nimegundua kuwa waandamanaji hao walionyesha nia ya wazi ya kuwakomesha wale wote wanaojipachika karibu na Wanasiasa na kukiuka haki ya msingi ya kuwa kioo cha jamii kama watu maarufu katika kundi la vijana.
Katika mahojiano ya wazi na kikundi cha madereva wa Bodaboda katika Kata ya Kimara, Kituo cha Kimara Mwisho, vijana hawa walionekana kuchoshwa na mwenendo wa “uchawa” unaoenea miongoni mwa vijana maarufu na wanaofuatiliwa zaidi na jamii na kulalamika kuwa Siasa imekuwa sababu ya kuwagawa wananchi na sio kuleta maendeleo kwao.
“Hawa vijana wanapigana kwa majina ya wanasiasa, lakini wanasiasa hao hata hawajui hali yetu. Kila siku tunawaona tu wanaimba na kujipendekeza mitandaoni kwenye kampeni zao na kula nao sahani ya mema ya nchi na wanasahau hata wao wengine walitoka kwenye umaskini kama wetu yaani kiukweli kabisa tunataka Serikali isimamie haki, lakini si vijana kutumiwa kama vyombo vya kampeni,” anasema Bodaboda mmoja.
Kwa mtazamo wangu hali iliyopo sasa kijana akisema ukweli, anaambiwa ni msaliti lakini akimsifia Mwanasiasa, anapata posho. Hapo ndipo demokrasia inapokufa.
VIJANA WAMEPOTEZEA ZOEZI LA KUPIGA KURA
Ukweli mchungu ni kuwa vijana wengi hawajashiriki kabisa kwenye kutimiza jukumu lao la kidemokrasia la kupiga kura na kushiriki kwenye uchaguzi mkuu na wengi wao walikata tamaa na kuamini sio jukumu lao kufanya hivyo.
Na hali hii imethibitika wazi kupitia mitandao ya kijamii ambapo vijana wengi walishiriki zoezi la maandamano na sio kupiga kura.
Mtaalamu mmoja wa masuala ya utawala bora kutoka Chuo Kikuu fulani, anasema kuwa Uchawa ni sumu ya demokrasia na unavunja misingi ya uwajibikaji kwa sababu viongozi wanajua watalindwa na mashabiki, si kwa utendaji wao, bali kwa maneno.
Vijana wanapaswa kuwa walinzi wa uwazi, si makundi ya kupigia makofi kila kitu kwa maslahi binafsi.
Kwa sasa hali hii ya uchawa imechangia mno kuporomoka kwa imani ya Wananchi kwa Serikali, huku vijana ambao ndiyo nguvu kazi ya taifa wakigeuzwa kuwa watumishi wa maslahi binafsi ya wanasiasa.
Tanzania ina vijana wengi wenye nguvu, maarifa, na ubunifu lakini kama nguvu hizo zitaendelea kutumika kulinda maslahi ya watu wachache kupitia “uchawa,” misingi ya demokrasia na utawala bora itazidi kuyumba.
Ni wakati wa vijana kujitazama upya si kama makundi ya kushangilia, bali kama walinzi wa haki, uwajibikaji, na mustakabali wa taifa letu.
Demokrasia si kupiga kelele, ni kufanya maamuzi yenye uelewa. Tukikosa hilo, tutabaki tukiwasha moto, huku tukiteketeza ndoto zetu wenyewe.