Uchapakazi wa Dkt. Tulia wawakosha wana Mbeya, watoa onyo kali kwa atakayechukua fomu kushindana naye

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,338
9,766
Ndugu zangu Watanzania,

Baada ya jimbo la Mbeya mjini kwa miaka kumi kukosa mwakilishi sahihi Bungeni, kukosa wakulisemea Bungeni, kukosa Mbunge mwenye ushawishi na mwenye kuwaunganisha Wanambeya, sasa jimbo limepata Mbunge wa kweli, mpenda maendeleo, mchapa kazi na kiongozi mwenye maono.

Huyu ni Dr. Tulia Acksoni Mwansasu kipenzi cha wana Mbeya, chaguo la wana Mbeya, dada wa mkoa, sauti ya wana Mbeya, nembo ya wana Mbeya, nguvu ya wana Mbeya, nguzo ya Mbeya na fahari ya wana Mbeya. Huyu ni dada msomi, mbobezi na nguli wa sheria ambaye ni Spika wa Bunge, Mjumbe wa CCM kuanzia ngazi ya Tawi mpaka ngazi ya Kamati Kuu ya CCM Taifa na Rais mtarajiwa wa Umoja wa Mabunge Duniani anayeungwa mkono na Umoja wa Afrika. Aliyekuja kuleta tabasamu katika jiji na Mkoa mzima wa Mbeya na Nyanda za juu Kusini.

Kwa sasa, tangia Vikao vya Bunge vimalizike pale Dodoma alirejea moja kwa moja mkoani Mbeya katika jimbo lake analolipenda na kuwapenda Wanambeya kwa dhati ya moyo wake wote. Ndio maana kwa upendo huo ameonekana muda wote pasipo kupumzika wala kukaa ofisini, ameonekana akipita maeneo mbalimbali kusaidia watu, kueleza mipango ya serikali yao, kueleza miradi ambayo inakwenda kutekelezwa jijini Mbeya.

Ni kila kona unamuona Dr. Tulia akiwa na wananchi wake, muda wote yupo kazini kuwahudumia wananchi, kuwapa majibu, kuwapa, matumaini, kuwapa njia, kuwaondoa hofu. Hachagua wala habagui wakuzungumza naye au kumsaidia shida yake.

Leo hii pamoja na mambo mengine mengi alikuwa kukagua ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kike shule ya Sekondari Samora, hali itakayo chochea kufaulu na kufanya vizuri kimasomo kwa wanafunzi wa kike na kupata muda mzuri wa kujisomea.

Imefika wakati wana Mbeya wanajuta kwanini walipoteza miaka yao kumi kwa mtu ambaye alikuwa hatambui wajibu wake kama kiongozi,wanasema Dr Tulia alikuwa wapi? Kwanini hakuja mapema? Wanasema Mbeya ya Dr. Tulia inapaa na kung'ara kimaendeleo, Mbeya ya Dr. Tulia inaleta matumaini kwa makundi yote na rika zote.

Ndio maana ukienda kwa vijana wa bodaboda au bajaji unaona namnaa ambavyo wanampenda na kumkubali Dr. Tulia kama ilivyo kwa akina mama, wazee, watu wenye ulemavu, yatima, wajane na hata watu wa vipato vya chini, kwa kuwa Dr. Tulia amegusa maisha ya watu wote na makundi yote, hakuna utakako kwenda usikute alama za Dr. Tulia.

Dr. Tulia ni mshindi katika mioyo ya wana Mbeya, amefanikiwa kupandisha bendera ya jina lake katika kilele cha mioyo ya wana Mbeya, amefanikiwa kuiteka mioyo ya wengi na kulituliza jiji la Mbeya, ameliletea sifa na heshima kubwa sana jiji.

Sasa linasikika na kusikilizwa masikioni mwa serikali, sasa lina vuma kwa miradi ya kimaendeleo na kuwa kivutio cha wengi katika utafutaji wa maisha. Ni kazi ya Tulia, ni juhudi zake,ni mikono yake, ni uhodari wake, ni utayari wake kuwasadia na kuwatumikia wana Mbeya, ni moyo wake wa upendo, ni uchapa kazi wake, ni kujitoa na kujitolea kwake ndiko kumelifikisha jiji hapo lilipo kimaendeleo.

Hii ndio sababu ya wana Mbeya kutoa onyo kali kwa yeyote atakaye taka kuchukua Fomu ya Ubunge kushindana na Dr. Tulia, atapata aibu kubwa sana, atagaragazwa na kutupwa kwa aibu kubwa ambayo hataweza kusahau maishani mwake.

Dr. Tulia anafanya kazi kwa ukaribu sana na Mh. Rais na serikali yake, ndio maana amekuwa akisikilizwa katika mahitaji ya wana Mbeya. Ndio maana viongozi wakuu wote kitaifa kwa nyakati tofauti wamelitembelea na wamefika katika jiji la Mbeya.

Sasa Mbeya haipo tayari kupeleka mtu mwingine ambaye ataleta vurugu jijini na kulikwamisha jiji kupiga hatua za kimaendeleo katika utekelezaji wa miradi mbalimbali, ambayo inafanywa kwa sasa ni Dr. Tulia.

Kazi iendelee, Mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Ndugu zangu watanzania,

Baada ya jimbo la Mbeya mjini kwa miaka kumi kukosa mwakilishi sahihi bungeni, kukosa wakulisemea Bungeni,kukosa mbunge mwenye ushawishi na mwenye kuwaunganisha wanambeya .sasa jimbo limepata mbunge wa kweli , mpenda maendeleo,mchapa kazi na kiongozi mwenye maono.

Huyu Ni Dr Tulia Acksoni mwansasu kipenzi cha wana Mbeya,chaguo la wana Mbeya,Dada wa mkoa ,sauti ya wana Mbeya ,Nembo ya wana Mbeya,Nguvu ya wana Mbeya , nguzo ya Mbeya na fahari ya wana mbeya .Huyu Ni dada msomi ,mbobezi na nguli wa sheria ambaye ni spika wa Bunge ,mjumbe wa CCM kuanzia ngazi ya Tawi mpaka ngazi ya kamati kuu ya CCM Taifa na Rais mtarajiwa wa umoja wa mabunge Duniani anayeungwa mkono na Umoja wa Afrika . Aliyekuja kuleta Tabasamu katika jiji na mkoa mzima wa Mbeya na nyanda za juu kusini.

kwa sasa Tangia vikao vya Bunge vimalizike pale Dodoma alirejea moja kwa moja mkoani Mbeya katika jimbo lake analolipenda na kuwapenda wanambeya kwa dhati ya moyo wake wote,ndio maana kwa upendo huo ameonekana muda wote pasipo kupumzika wala kukaa ofisini ,ameonekana akipita maeneo mbalimbali kusaidia watu,kueleza mipango ya serikali yao,kueleza miradi ambayo inakwenda kutekelezwa jijini Mbeya.

Ni kila kona ,kila sehemu ,kila mahali unamuona Dr Tulia akiwa na wananchi wake, muda wote yupo kazini kuwahudumia wananchi,kuwapa majibu,kuwapa, matumaini,kuwapa njia,kuwaondoa hofu.Hachagua wala habagui wakuzungumza naye au kumsaidia shida yake.leo hii pamoja na mambo mengine mengi alikuwa kukagua ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kike shule ya sekondari samora,hali itakayo chochea kufaulu na kufanya vizuri kimasomo kwa wanafunzi wa kike na kupata muda mzuri wa kujisomea.

Imefika wakati wana Mbeya wanajuta kwanini walipoteza miaka yao kumi kwa mtu ambaye alikuwa hatambui wajibu wake kama kiongozi,wanasema Dr Tulia alikuwa wapi? Kwanini hakuja mapema? Wanasema Mbeya ya Dr Tulia inapaa na kung'ara kimaendeleo,Mbeya ya Dr Tulia inaleta matumaini kwa makundi yote na rika zote,ndio maana ukienda kwa vijana wa bodaboda au bajaji unaona namnaa ambavyo wanampenda na kumkubali Dr Tulia kama ilivyo kwa akina mama,wazee,watu wenye ulemavu ,yatima,wajane na hata watu wa vipato vya chini,kwa kuwa Dr Tulia amegusa maisha ya watu wote na makundi yote,hakuna utakako kwenda usikute alama za Dr Tulia.

Dr Tulia ni mshindi katika mioyo ya wana Mbeya, amefanikiwa kupandisha bendera ya jina lake katika kilele cha mioyo ya wana Mbeya ,amefanikiwa kuiteka mioyo ya wengi na kulituliza jiji la Mbeya,ameliletea sifa na heshima kubwa sana jiji,sasa linasikika na kusikilizwa masikioni mwa serikali,sasa lina vuma kwa miradi ya kimaendeleo na kuwa kivutio cha wengi katika utafutaji wa maisha. Ni kazi ya Tulia,ni juhudi zake,ni mikono yake , ni uhodari wake ,ni utayari wake kuwasadia na kuwatumikia wana Mbeya ,ni moyo wake wa upendo,ni uchapa kazi wake ,ni kujitoa na kujitolea kwake ndiko kumelifikisha jiji hapo lilipo kimaendeleo.

Hii ndio sababu ya wana Mbeya kutoa onyo kali kwa yeyote atakaye taka kuchukua Fomu ya ubunge kushindana na Dr Tulia,atapata aibu kubwa sana ,atagaragazwa na kutupwa kwa aibu kubwa ambayo hataweza kusahau maishani mwake.Dr Tulia anafanya kazi kwa ukaribu sana na mh Rais na serikali yake ndio maana amekuwa akisikilizwa katika mahitaji ya wana Mbeya ,ndio maana viongozi wakuu wote kitaifa kwa nyakati Tofauti wamelitembelea na wamefika katika jiji la Mbeya. sasa Mbeya haipo Tayari kupeleka mtu mwingine ambaye ataleta mavurugu jijini na kulikwamisha jiji kupiga hatua za kimaendeleo katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ambayo inafanywa kwa sasa ni Dr Tulia.

Kazi iendelee ,mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa,kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Mwambie atafute kazi ya kufanya mapema.
 
Back
Top Bottom