Kihodombi Kingamba
JF-Expert Member
- Feb 9, 2016
- 243
- 108
JWTZ imekuwa inapeleka askari wetu kwenda kuchangia kwenye ulinzi wa amani katika nchi zenye matatizo kama ambavyo tunapaswa kufanya hivyo kwa mujibu ya matakwa ya Umoja wa Mataifa kwa nchi zote wanachama wa umoja huo. Jeshi letu limekuwa linapeleka askari wetu ktk nchi za DRC, SUDAN(Jimbo la Darfur) na Lebanon. Ninachofahamu Umoja wa mataifa huilipa Serikali husika fedha kwa kila askari anayeshiriki pamoja na vifaa vinavyotumika kuendesha shughuli hizo za ulinzi na usalama. Ninachojiuliza fedha hizi huenda wapi ? Maana sijawahi kusikia hata siku moja kama Wizara ya Ulinzi imeongeza kwenye pato la Taifa kiwango Fulani cha pesa kama zilivyo wizara nyingine kama Wizara ya Mali asili na Utalii, Mambo ya ndani kupitia idara zake za Polisi kitengo cha Traffic, Uhamiaji na mara chache idara ya magereza, Wizara ya Madini, Wizara ya Ardhi n.k. Isije ikawa kunamajipu nako huko yanayohitaji kutumbuliwa. Nchi kama Rwanda moja ya vyanzo vya kuipatia pesa za kigeni ni hili swala la kushiki kwenye maswala ya ulinzi na usalama. Kwa kulijua hilo wamepeleka askari katika nchi za Sudan(battalion 3) South Sudan(battalion moja) CAR na kwingineko. Isije ikawa labda serikali haijui kuhusu swala hili. Najua wapo watakaochangia hoja hii ili nipewe elimu na kujua fedha hizo zinamchango gani kuwahudumia wananchi wanyonge hasa akina mama wanaokosa vitanda kabla na baada ya kujifungua kwenye mahospitali yetu Nchini. Nawasilisha hoja tafadhali.