Uchambuzi wa Soka: Nani bora zaidi kati ya Mwalimu Kashasha na Dr. Leakey?

Kashasha ni muongomuongo, anachambua mpira kama anasolve physics
Hio kitaalam inaitwa LOCOMOTIVE FEINT,, yani Mchambuzi anampiga kamba msikilizaji kwa kutumia kingereza cha ndani yani CORE LINGUISTICS INSTINCT na naimani mpenzi msikilizaji atamwaga makofi bilq kuelewa hata anashabikia nini!
 
Huyo mwl kashasha akielezea goli la kichwa utamsikia "pale ilikua head bending tactically heart controllel kwenye movement in order to score organism
Dakika za nyongeza anakwambia ni injury time
Hahahah aisee leo nimecheka kinoma, nilikuwa namsikia tu huyo mzee nikaamua kumfatilia baada kumuona akichambua body spray ya Fyn by Falsafa.

Kuna clip moja anachambua goli la tiktaka anasema kitaalamu ile ni "Backside bicycle kick" yani mchezaji alipokea mpira uliokuwa umepigwa kuelekea kati kati kisha akafanya kupunguza kasi kama muendesha baskeli anvyorudisha pedal nyuma kwenye mporomoko. Kisha kuachia mkwaju mkali wa tiktak.

Aiseee nimecheka hadi sio vizuri!!! Jamaa ni mchambuzi ila vingine anatupiga kamba za wazi sema ukimuangalia sura yake na anachoongea ni vituko sana.
 
Back
Top Bottom