Uchambuzi wa Soka: Nani bora zaidi kati ya Mwalimu Kashasha na Dr. Leakey?

Mel. Kashasha changa nyingi, Dr. Leaky mfungaji mahiri.
Kila mtu ana ladha yake.
Kashasha anachambua kama mwalimu wa wachezaji, Dr anachambua kama Rais wa timu.
Kumbuka rais wa timu ndio mwenye maono (vision) ya timu, mwalimu ni mtimiza maono
Big NO
 
Wewe utakuwa dr leakey mwenyewe...unataka kiki ila kiukweli yule mzee kashasha wewe humuwezi kabisa kwani yule ni mchambuzi wa kiufundi ila ww una story nyingi sijui kazaliwa wapi kakulia wap anapenda kula nn.....baada ya kuchambua ya dk 90 ww unaleta story za miaka 20 iliyopita
Wewe pimbi humjui Dr Leakey Abdullah, kwa taarifa yako Dr anamiliki kampuni ya uwindaji na ana pesa ya kufa mtu, huo muda wa kupiga porojo na majobless autowe wapi?
 
Nilichogundua humu wengi wamemjua Dr. Lekey Juzi juzi hapa, wala hawana ufahamu juu yake toka DTV na chambuzi zake ambaye ame inspire au ndio pioner wa segment ya uchambuzi wa mpira katika Tv!

Wanaomuna Mwalimu wangu wa Darasani Kashasha ni mzuri kwa sababu wanamjua kupitia ligi za ndani ya nchi na majuzi juzi kwenye TBC!

Hawa ni watu wawili tofauti. Dr. Lekey anajua si tu historia za timu, mchezaji mmoja mmoja na kuuishi mpira wa miguu kwa kutembelea maeneo na viwanja vingi vya mpira bali pia anakumbukumbu za matukio mengi ya mpira hasa kwa timu za nje ya nchi. Kifupi yeye ni wa KIMATAIFA!

Mwl wangu kabisa Gashasha ni mwalimu wa Physical Education. Anaujua mpira wa vitabuni na ni mbobezi kwa wachezaji na mechi za ndani ya nchi yetu. Kifupi anaujua mpira kwa kusomea na si passion au experiences kama Dr. Lekey!

Ipendeze kusema tu kwamba hawa watu ni hazina ya Taifa katika maswala haya ya ujadilifu wa mechi za mpira wa miguu.
Ss huyo leakey kama anajua sana historia za watu bora aende makumbusho
 
Wewe pimbi humjui Dr Leakey Abdullah, kwa taarifa yako Dr anamiliki kampuni ya uwindaji na ana pesa ya kufa mtu, huo muda wa kupiga porojo na majobless autowe wapi?
Ww tutusa kama ana makampuni ya uwindaji hapo tbc anaenda kufanya nn na porojo zake
 
Wewe pimbi humjui Dr Leakey Abdullah, kwa taarifa yako Dr anamiliki kampuni ya uwindaji na ana pesa ya kufa mtu, huo muda wa kupiga porojo na majobless autowe wapi?
Ww tutusa kama ana makampuni ya uwindaji na hana muda wa kupiga porojo hapo tbc anaenda kufanya nn na porojo zake,funga bakuli lako wewe au ww ni mkewe?
 
sema ukwel huyu mzee anatupaga chai
Mimi huwa nafuatilia uchambuzi vituo vingi vya TV hata nje sijawahi kusikia mchambuz akitumia technical jargons kama za kashasha. Mzee anajichoshwa kumeza yale mamisamiati
 
Kuwalinganisha hawa ni kukosea sana kwani Mwalimu Kashasha ni mwalimu wa soka na Dr Leak ni mchambuzi wa soka sasa usishangae kuona hizo technical terms za Kashasha ukaona anajua sana ni porojo tu kama zingekuwa nzuri zingesaidi team anayoifundisha kufika mbali but Dr Leaky anachambua kuanzua historia ya mchezaji na kwakutumia uwezo na mfumo anaweza kusema team ipi itapata nafasi zaidi ya ushindi kama unabisha ninachokisema waauliza Premier bet watakuambia kazi ya Dr Leak.
 
Wewe unakila bange ya wapi?mwl kashasha anafundisha timu gani?kama humjui mtu sio lazma umuelezee bora ukae kimya huyu ni mwl wa darasani kabisa sio kocha......
Huyo leakey yeye ni kumeza stori na kuzisimulia hana anachokichambua kitaalam
 
Kwanza hongera JF kwa kurudi hewani

Ningependa kujua mtazamo wa watu juu ya wachambuzi hawa wawili wa soka hapa Tanzania.

Mwalimu Kashasha na Dr. Leakey, Wamekuwa wakichambua soka stesheni ya TBC wakati huu wa kombe la dunia. Kwa kweli Mwalimu Kashasha kwa mtazamo wangu kamuacha mbali sana Dr. Leakey. Licha ya Mwalimu Kashasha kuwa na technical jargons za soka ila anajua kuuchambua mpira kiufundi zaidi

Dr. Leakey sioni akichambua mpira upande wa mbinu za mchezo bali yeye ni masimulizi ya kawaida tu kama ya kupiga stori kijiweni kuhusu soka.

Je wewe wadhani nani ni zaidi?[

Mwalimu Kashasha..KWAKO JESSE JOHN!
 
Back
Top Bottom