Uchambuzi wa magazeti Clouds TV hauvutii

Hawana chambuzi wa habari hata mmoja,imebidi waombe msaada kwa Nick wa 2
 
Sivutiwi kabisa na clouds TV kiasi kwamba kila nikijaribu kujilazimisha kuiangali ndio nazidi kuchefuka.

Hawa jamaa wasoma magazeti asubuhi utadhani wako katika kijiwe cha kahawa, maneno yao hovyoo! duh.

ila i hope katika hizi lawama zako dada yetu baby kabaye hujamuhusisha kwani sidhani kama anafanana nao kuanzia kifikra na kimtazamo wa kujenga hoja pia.
 
Nilidhani ni mimi mwenyewe siku nilipoangalia hicho kipindi hao vijana niliona wanaongea kama watu wanaopiga story kijiweni! Siwezi kurudia tena kuwasikiliza..
 
wanaitaji viongoz thabiti

kama kazi zenyewe zinapatikana kwa ushikaji, kujuana na hata rushwa zetu hizi wewe unategemea nini hapo mkuu? japo tuna chuki na tbc lakini ukweli utabaki kuwa pale pale kuwa ndiyo media pekee hapa nchini tanzania inayofuata maadili kamili ya kiuandishi wa habari na hawaajili watu wa certificate au diploma bali hapo mwendo ni degree na masters tu. mapungufu ya waandishi na watangazi wa tbc ni kwamba wanafanya tu kazi kwa matakwa ya serikali ila kwa qualifications za masuala ya habari na utangazaji wapo vizuri. mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
 
Nilidhani ni mimi mwenyewe siku nilipoangalia hicho kipindi hao vijana niliona wanaongea kama watu wanaopiga story kijiweni! Siwezi kurudia tena kuwasikiliza..

boss wao ruge nadhani yupo chimbo akiandaa matamasha yajayo ya fiesta. na nimepata nyepesi nyepesi kuwa huyo kamoga kapata shavu hapo baada tu ya kuwa rafiki na ruge kupitia shughuli zake za mc na unaambiwa anakubalika na boss ruge kushinda hata wafanyakazi wote wengine hapo clouds. labda wanaojua zaidi watatuweka wazi. ila ukweli na kwamba sam sasali mwanzoni alianza vizuri sana ila na yeye akaingia katika mtego wa kamoga wa yeye kuingizwa katika uswahili na upuuzi na sasa umemkolea na amekuwa mswahili ile mbaya. sam sasali namjua ni kijana mwenye upeo na uwezo mkubwa na mzuri wa kufikiri na ni mjenga hoja makini ila sasa maarifa yake yamefichwa na utoto na upuuzi wa hudson.
 
We kweli kichaa.... Cloud hata hapo Pwani, Kibaha haishiki.... Radio one ndio inaongoza

siku nyingine jaribu kuficha ujinga na upumbavu wako. siasa hizi za maji taka zinakuharibu. najua umejibu kihasira ukijua kwamba clouds fm na tv ni pro ccm na umeisifia hapo radio one kwakuwa umeshajua kuwa ni pro chadema ambako wewe uko. kwa kukusaidia tu ingia ktk website ya tcra kisha angalia coverage ya clouds fm na tv kwa hapa nchini tanzania kisha nakushauri urudi tena humu uje kufuta kauli yako uliyomtolea member huyo. jamani hivi hizi electronic gadgets tulizonazo tunazitumiaje? kuangalia tu picha za utupu na upuuzi upuuzi mwingine usio hata na tija? na huyu nae eti ni mpiga kura wa tanzania anayetegemea kupiga kura yake ndani ya siku 10 zijazo! acheni tu wakenya, waganda na wanyarwanda watucheke kwa kuwa na upeo wa kimo cha nyoka.
 
We kweli kichaa.... Cloud hata hapo Pwani, Kibaha haishiki.... Radio one ndio inaongoza

Wewe Wasema,kama Huku Iringa Inasikika Vizuri Tu Sembuse Hapo Pwani Na Kibaha?
Redio One Kipind Cha Habari Tu Ndo Inasikilizwa Tofauti Na Hapo Haisikilizwi Sana...
Halafu Tujaribu Kuwa Tofauti Cloudstv Ni Tv Ya Vijana Hawawezi Wakawa Wote Sawa Kama Tv Nyingine...Lazima Kila Tv Iwe Na Something Unique From Others
 
Wanasoma sana gazet la uhuru ad hudson kamwaga kajshtukia kasema wik ijayo baadh ya mgagazet yanayoegeme upand 1 hawatayasoma.
 
Back
Top Bottom