Nanyaro Ephata
JF-Expert Member
- Jan 22, 2011
- 1,232
- 1,810
Kitabu. My Life
Mwandishi.Bill clinton
Mchambuzi.Nanyaro EJ
Dibaji
Mwandishi anasema kuwa alipokuwa kijana mdogo akiwa na matamanio makubwa ya kimaisha,alisoma kitabu fulani ambacho kimekuwa msaada mkubwa kwenye maisha yake,na ambacho kilimsaidia kuwa alivo leo.Hiki kitabu kinaitwa *How to get control of your time and life by Alain Lakein*
ujumbe mkubwa kwenye kitabu hicho ni kuhusu namna bora ya kuweka mpangilio wa shughuli na malengo katika utaratibu wa muda wa mfupi,muda wa kati,na muda mrefu,kisha malengo haya unayagawa katika umuhimu wake yaani unaweka vipaumbele !
Mwandishi anasema kuwa unaweza kuweka utaratibu wa kundi A kuwa ndio kundi muhimu zaidi,Kundi B kundi linalofuatia kwa umuhimu,kundi c ambalo sio muhimu sana.Bill Clinton anasema miaka 30 baadae bado anakumbuka utaratibu huu ambao pia aliuandika kwenye sehemu ya diary zake hadi leo anayo anakumbuka kwenye malengo yake mahususi alipanga kuwa mtu mwema,awe na ndoa nzuri,na watoto bora,awe na marafiki wazuri,afanikiwe katika maisha ya kisiasa na aje kuwa mwandishi mzuri wa kitabu bora!
Kwamba ni mtu mwema hiyo ni Mungu atahukumu,ingawa anatambua sio mwema sana kama wengi wanavomchukulia! Ila pia sio mtu mbaya kama wakosoaji wake wanavomchukulia na kumsema.Anasema kuhusu ndoa amebarikiwa sana na Hilary na Chelsea.Kama familia nyingi zilivo yake pia haijakamilika lakini ina baraka na mafanikio mengi licha ya kuwepo kwa changamoto kadhaa
Anasema alipata Urais kwa msaada wa marafiki zake wakati huo wakiitwa Friends of Bill (FOBs),anasema alifurahia maisha ya kisiasa,alifurahia kufanya kampeni na kuongoza(uongozi) mara zote alitoa uongozi na kuonyesha njia,na kuhakikisha kila kitu kinaenda katika mwelekeo sahihi!alihakikisha kila mmoja akafikia ndoto zake,aliwatia moyo wenzake,na alihakikisha watu wanakuja pamoja ndio siri ya kufanikiwa kwake
Sehemu ya kwanza
Mwandishi anasema alizaliwa mapema asubuhi ya 19/8/1946 katika hospitali ya Julia Chester iliyopo mjini Jipe,mji huu upo kilomita 60 kusini magharibi mwa Jimbo la Arkansas na maili 30 Mashariki mwa Texas
Mama yake ambaye alikuwa mjane alimwita jina la William Jefferson Blythe III baada ya Baba yake mzazi ambaye alikuwa marehemu wakati na aliitwa William Jefferson Blythe Jr.(Kuna utamaduni wa USA kuita watoto wanaitwa Wiliam Bill na hapo ndio alianza kuitwa Bill hadi leo ila jina halisi ndio hilo Wiliam )Baba yake Alikuwa mmoja wa watoto tisa wa mkulima maskini katika kitongoji cha Sherman huko Texas,Babu yake yaani huyu mkulima Maskini alikufa wakati Baba yake Bill akiwa na miaka kumi na saba,kwa mujibu wa simulizi za Shangazi zake Bill Clinton ni kwamba Baba yake na Bill alikuwa mchapakazi,na mtu mwenye upendo sana kwa ndugu zake na watu wengine.
Bill Clinton alifiwa na baba yake wakati mama akiwa na ujauzito wa miezi saba,hivo Bill hakuwahi kumwona Baba yake,mzazi alilelewa na mama pekee,kwa mujibu wa simulizi za mama alimwelezea kuwa wao Mama na Baba walikutana katika hospitali ya Tri-State Hospital in Shreveport, Louisiana, 1943, wakati Mama akiwa anafanya kozi ya kujifunza kuwa Nesi.Walipoona hapo walisalimiana na baadae baba alituma ua baada ya kuambiwa kuwa hajaolewa,mama alipokea lile ua na ukawa mwanzo mpya wa mahusiano yao.Miezi miwili baadaye walifunga ndoa na baba kuondoka kwenda vitani! Baba alikuwa fundi Makenika hivo vitani alikuwa akirepea gari za jeshi.
Mwandishi anasema baada ya vita alirejea nyumbani kisha wakahamia Jiji la Chicago,baba alipata kazi kampuni ya Manbee Equipment,kazi iliyomfanya waweze kununua nyumba kwenye viunga vya mji,wakati huo Mama yake alikuwa na ujauzito wake Yeye Bill.Mei 17 mwaka 1946 baba alikuwa njiani kumfuata mkewe ili wahame moja kwa moja kwenye nyumba mpya,kwa bahati mbaya akapata ajali mbaya iliyochukua uhai wake.Kwa maelezo ya mashuhuda gari ilipoteza mwelekeo ikaingia kwenye mtaro na dereva ambaye ni Baba yake Bill akatupwa mtaroni(Magari ya zamani hizo hayakuwa na mikanda wala airbag),alikuja kuokotwa masaa matatu baada ya ajali kutokea akiwa ni marehemu,alikutwa kwenye mtaro inaonekana alijaribu kutoka mtaroni ilishindikana,wakati huo Baba alikuwa na umri wa miaka 28 na ndoa ya miaka miwili.
Bill anasema hayo tu ndio anayojua kuhusu baba yake,hili lilimfanya tamani kujua zaidi kuhusu baba,yaani kiu ya kumjua baba yake haikuisha kabisa!kipande cha picha au maelezo kuhusu Baba yake kilikuwa kitu cha dhamani sana kwake
Mwandishi anasema kuwa gazeti maarufu la Washington Post lilifanya uchunguzi mwaka 1993 kuhusu ukweli wa Baba yake,katika uchunguzi huo walikubaliana na maelezo ambayo mama yake alikuwa amempa.Ingawa gazeti liligundua kuwa kabla ya Baba yake kumwoa Mama yake alikuwa ameoa mara mbili na kuachana na pia alikuwa na watoto wawili kwenye hayo mahusiano,mmoja wa kike na mwingine wa kiume,huyu wa kiume aliitwa Leon na baada ya gazeti kufichua alifanya utaratibu akakutana na kaka yake kwa mama mwingine,anasema walifanana sana,ila hakufanikiwa kuonana na dada yake.Bill anasema habari hii ya mwaka 1993 ilikuwa na mshtuko mkubwa kwa mama yake,hata hivo mama alisema kuwa jambo moja la hakika analojua ni kuwa marehemu mume wake alikuwa anampenda sana,hilo linatosha.
Mwandishi anasema wakati wa mwisho wa Urais wake aliamua kuaga watu wa USA kwa kutembelea maeneo muhimu ambayo baba yake aliwahi kuishi,au kufanya kazi,lengo likiwa ni kumuenzi Baba yake,ambaye simulizi zake zilikuwa kichocheo kikubwa katika kufanikiwa kwake,yaani ndio alikuwa Role Model wake! Fikra kuwa anaweza akafa akiwa mdogo kama baba yake ilimfanya atumie kila sekunde ya muda wake kwa ufanisi mkubwa,kwake muda ilikuwa rasimali muhimu ambayo haikupaswa kuchezewa hata sekunde moja.Hii ilimfanya ajisikie fahari kukabiliana na kila changamoto mpya,yaani hakuogopa changamoto.Hata nyakati ambazo hakuwa na uhakika wa mwelekeo lakini bado alikaza buti kusonga mbele!
Sehemu ya Pili
Mwandishi anasema alizaliwa siku ambayo ndio ilikuwa siku ya kuzaliwa ya Marehemu Baba yake!(Yaani siku yao ya kuzaliwa ni moja).Alilelewa na bibi yake mzaa mama kwa miaka mitatu,anasema alipata makuzi mazuri ya upendo wa hali ya juu kutoka kwa bibi yake,alikuwa mjukuu anayependwa zaidi,bibi alinijengea msingi imara wa maisha, na kisha akahamia New Orleans ambako mama yake alikuwa amepata kazi.Anasema New Orleans ni moja ya eneo analopenda sana.
Bibi alimfunza mambo muhimu kuwa ni kula vizuri,kusoma sana na kwa bidii,na kuwa msafi,hivo alikula hasa na wakati wa kula bibi yake angempigia soga na simulizi mbalimbali ikiwemo maswala ya kujua hesabu,na kucheza karata,karata ilikuwa moja ya njia za kujua hesabu/hisabati
Babu yake alikuwa muuza ice cream alikuwa na baiskeli mfano wa hizi za azam ila enzi hizo inatumia barafu kama ambayo tunatumia nyumbani.Huyu babu alikuwa anafanya kazi hii mchana na usiku alikuwa mlinzi kwenye timber moja huko,sasa Bill alikuwa anaenda kulinda na Babu yake kwenye hilo lindo
Mwandishi anasema wakazi wengi kwenye mji wa New Orleans hawakuwa na TV ndani,hadi mwishoni mwa 1950.Familia nyingi zilikuwa ni extended family wakati,huo hivi yeye hapo kwa Babu kulikuwa na wajukuu wengine pamoja na ndugu jamaa! Licha ya hali ya umaskini ambako wengi walikuwa wakulima walilima ili kuishi watu hawakuwa na lawama zozote.Walifurahia maisha na kufanya kazi ili waishi na sio kuishi ili kufanya kazi
Sehemu ya tatu
Mwandishi anasema kuwa baada ya muda Mama yake mzazi alihama kutoka jimbo la New Orleans kurudi mji wa Hope,kwa mujibu wa diary ya Mama yake inayoitwa Leading with my heart(ambayo mwandishi anaamini kama ingekuwa kitabu kingekuwa moja ya vitabu bora kabisa Duniani) mama ali date wanaume kadhaa akiwa New Orleans na alikuwa anaandika kwenye diary hiyo matukio yote muhimu.
Kwenye mji wa Hope mama alikuja kukutana na jamaa mmoja aliyeitwa Roger Clinton,ambaye walifunga ndoa mwaka 1950 wakati huo mama akiwa na miaka 27 tu.Huyu baba wa kambo alikuwa mtu mwema sana akawa anamtunza vizuri kama mwanae,na alikuwa anampenda mama pia,hapo wote yaani mama na mwanae wakadata ndio mwanzo wa jina lake Bill Clinton akaacha yale majina aliyopewa na *****!
Bill anasema walikuwa wanacheza michezo mingi ya utotoni ikiwepo ule wa kurushiana mpira,al maarufu kama ready,pia ule mchezo ambao kunakuwa na watoto wawili ambao wanashika kamba kisha mmoja anakuwa anaruka hiyo kamba,au waweza funga kwenye mti alafu upande mmoja anakuwa mtu mmoja ambaye atakuwa anaizungusha,unaruka bila kuigusa kamba,kamba ukiugusa unakuwa umeshindwa! miongoni mwa majirani aliocheza nao ni watoto wa Mack McLarty ambaye alikuja kuwa miongoni wa wafanyabiashara waliofanikiwa na Katibu mkuu kiongozi wakati Bill alivoukwaa Urais.
Mwandishi anasema licha ya uzuri na upendo wa baba yake wa kambo,bado alikuwa baba mkali sana kwa mama yake,anakumbuka siku moja Mama alitaka kwenda hospitali kumsalimia Babu yake,Baba akagoma,mama alipotaka kulazimisha akaambulia kuchapa cha mbwa koko,yaani Rogers Clinton alikuwa anampiga mkewe pamoja na matusi makubwa.Hii siku sasa yeye Bill aliposikia mama yake akilia akamua kwenda chumbani kwa wazazi wake kujua nini tatizo,alipoingia tu mzee Roger akatoa Bunduki akafyatua risasi ya moto kuelekea alikokuwa Bill na Mama yake mzazi,bahati ile risasi haikupata mtu ikakita ukutani!walifanikiwa kutoroka wakakimbilia kwa jirani,polisi walifika wakaja kumkamata mzee Baba aliyekuwa anafura kwa hasira,alishikiliwa kwa muda wa siku moja kisha kuachiwa na polisi
Sehemu ya nne
Mwandishi anasema baada ya masomo yake ya shule ya upili,wazazi wake walihamia shambani,baba yake alikuwa na shamba zaidi ya ekari 400 nje kidogo ya mji,shamba hili likiwa na mifugo,kama Mbuzi,kondoo na ng'ombe,pia lilikuwa na nyumba lakini nyumba hii ya shambani haikuwa na choo cha ndani bali choo kilikuwa kimejengwa nje mbali kidogo na nyumba,ililazimu kutembea kupita kwenye machaka(vichaka)kufika chooni au bafuni,
Shamba hili lilikuwa na nyoka na wadudu wengine,ni moja ya uzoefu mkubwa kabisa kwenye maisha yake!anasema kuishi shambani lilikuja kumsaidia sana kwenye kampeni zake,hasa pale alipokuwa anahutubia na kutoa ushuhuda wa kuishi shambani........anakumbuka pia siku amepigwa na dume la kondoo akiwa machungani........
Mwandishi anasema kuwa alianza kufanya kazi akiwa na miaka kumi na tatu tu,akitoka shule alikuwa anaenda kwenye kiwanda kidogo cha kutengeneza mayonaise,kazi yake ilikuwa kuweka lebo kwenye dumu,lebo za kampuni(Huko USA Mayonaise inatumika sana,sawa na Karanga huku kwetu) kwa kazi hii alikuwa analipwa ujira wa dola moja kwa saa,pesa ambayo ilikuwa nyingi sana kwake,na alitumia muda mwingi kibaruani na kwenye maktaba,hapo ndio alianza kupenda kusoma!
Sehemu ya Tano
Mwandishi Bill Clinton anasema mwaka 1956 alipata mdogo wake wa kiume kwa mama yake,aliitwa Roger Cassidy Clinton alizaliwa July 25 siku ambayo ndio siku ya kuzaliwa ya baba yake(Bill alizaliwa siku ya kuzaliwa ya baba yake Marehemu,na sasa mdogo wake anazaliwa siku moja na baba yake Bill wa kambo)
Ingawa mbali na huyu mdogo wake wa tumbo moja alikuwa na ndugu zake kwa upande wa baba yake wa kambo!wakati huu baba yake alishakuwa mtu wa tungi sana,aliposikia mkewe kajifungua alienda kumwangalia kidogo akarudi zake klabuni kunywa pombe za kienyeji!
Ni mwaka huu 1956 ambao familia yao walipata uwezo wa kununua TV,yes TV hizi enzi hizo ni mali adimu kabisa!kwa hiyo pamoja na furaha na ya kupata mdogo wake,lakini alikuwa na furaha zaidi ya kuwa na TV mpya nyumbani ili aweze kuangalia vipindi hasa katuni mbalimbali kama,Captain Kangaroo andHowdy Doody , with Buffalo Bob Smith, hizi ni katuni ambazo kama mtoto walikuwa wenzake wanapiga stori shuleni ila sasa kwa mara ya kwanza ana uhakika wa kuziangalia nyumbani!
Alipowasha TV alikutana na mjadala kati ya wagombea wa Democrats na Republican,mijadala ya kisiasa ikaanza kumwingia taratibu akajikuta anavutiwa na
Rais Eisenhower
Mwandishi anasema baba yake alifariki mwaka 1957 akiwa na umri wa miaka 56,katika umri wake baba alikuwa busy na shughuli za uchumi,lakini alipata nafasi pia ya kufurahia kazi ya mikono yake!
Bill anasema mwaka 1958 ilikuwa mara yake ya kwanza kusafiri nje ya mji wao kwenda Jijini kubwa la Dallas(Kama utoke mkoani ufike Dar),alifikia mahali akaamua kwenda sehemu inayoonyesha movie wakati huu alikuwa na miaka 12 alikuwa bado mtoto,muuza tiketi aligoma kabisa kuamini kuwa ni mtoto maana alikuwa na mwili mkubwa,akalazimishwa kulipa tiketi kwa bei ya mtu mzima,ilikuwa mara ya kwanza kwake mtu kukataa kumwamini,ilimuma sana,ila ikawa fundisho kubwa kwenye maisha yake.Hii ilimfanya aamue kuwa huru kufanya jambo hata kama sio kila mmoja anaunga mkono,na ikawa mwanzo wa safari yake ndefu kuelekea Washington......
Sehemu ya Sita
Mwandishi anasema kuwa alishangazwa sana jinsi mama yake mzazi alivokuwa na muda wa kufanya shughuli zote,kuwatunza yeye na mdogo wake Roger,muda wa kwenda kazini,mama yao hakuwahi kukosa tukio lolote la shuleni kwao,kuanzia yeye na mdogo wake,pia aliwatembelea marafiki zao,kwa ufupi Bill anamuelezea mama yake kuwa mama bora kabisa kuwahi kutokea hapa Duniani
Bill anaendelea kuandika kuwa hata kazini Mama alikuwa nesi bora,alitibu wagonjwa wote bila ubaguzi,hata wale maskini kabisa ambao hawakuwa na uwezo wa kulipia huduma,(Wakati huo hakukuwa na Bima,huduma zilitolewa kwa Cash na watu wengi hawapendi huduma za afya)anasema baadhi ya wagonjwa walikuwa wakipewa huduma basi humshukuru mama yake kwa kumpa vitu mbalimbali hasa matunda,ambayo yeye aliyala sana,hivo alipenda watu wasiwe na fedha ili waletewe matunda!(Bill alikuwa mtu anayependa kula sana)
Bill anagusia hapa kuwa kuna kipindi huko nyuma mdogo wake Rogers akiwa na miaka tano,wazazi wao walitalakiana,kutokana ba ulevi na manyanyaso ya kijinsia(unyanyasi majumbani).Baada ya Talaka walienda kuishi na mama yao,yaani mama yao aliondoka na watoto kisha akaomba Talaka.Baada ya muda mama yao aliwaita yeye Bill na Roger jr kuwataka maoni yao kuhusu kurejeana na Baba,yeye Bill aligoma lakini mama alimsisitizia kuwa wanahitaji kuwa na mwanamme ndani(nyumba ni mwanamume),hatimae wakaoana tena! Anasema alikuwa huu ulikuwa ukarimu na uvumilivu mkubwa na alijifunza sana kuhusu swala la msamaha na nguvu yake!
Wakati mdogo wake Rogers Jr anaanza shule ndipo yeye Bill aliamua kuhalalisha kabisa jina Clinton kisheria,alienda mahakama ya mwanzo ambako aliapishwa kuacha kutumia yale majina mengine,anasema alifanya hivi ili mdogo wake Roger asipate wakati mgumu wala kuumia hisia kuwa wana ubini tofauti!haya yalikuwa msingi wa uamuzi wake!
Sehemu ya saba
Katika sehemu hii ya Saba mwandishi anaelezea maisha yake ya shule(High School)anasema akiwa shule anakumbuka kuona tukio la mapinduzi ya Cuba kwenye tv,alimwona Castro akiingia viunga vya Havana kwa ushindi mkubwa,ingawa kama kijana maswala ya siasa hakuyapa uzito wowote.Kila jioni alitazama kipindi kwenye tv kuhusu haki za kiraia,moja ya vipindi alivopenda
Ni kipindi hiki alianza kupenda muziki,alipenda sana mziki wa Jazz band na Nyimbo za Injili.Hii ilipelekea kuwa mpiga Solo maarufu,alishiriki na kushinda tuzo ya mpiga Solo wa mwaka.Na baadae alikuja kuwa kiongozi wa bendi yao ya shuleni
Mbali na muziki alifanya vizuri kwenye masomo mengine hasa sayansi,mwandishi anasema wakati akiwa shule ndio kipindi Urusi ilikuwa imeshinda USA kwenda kwenye space chombo maarufu cha Urusi Spritnik kilikuwa kimefanikiwa kwenda anga za juu,hivo Rais W USA Eisnowhver na baadae JFK walitoa agizo kuwa mkazo shuleni uwekwe kwenye masomo ya sayansi na hesabu,yeye bili alifanya vizuri kwenye baoloji kuliko kemia(kwenye kemia anakumbuka aliambiwa na mwalimu wake kuwa akifika mika 40 apungze kula maana chakula hugeuka kuwa sumu kwa kadri umri unavyoenda,kuna umri ambao digestion haitafanyika kwa ufasaha)hili somo analo hadi leo maana yupo zaidi 40.(tafiti za kisayansi zinaonyesha kuwa watu wazima wanaweza kuongeza maisha kwa kupunguza kiwango cha chakula)
Mwandishi anasema walikuwa na club za mijadala mbalimbali shuleni,pamoja na matukio na hotuba mbalimbali.Hotuba hizi zilifanya mtu ajulikane mrengo wake kutokana na mtazamo wake,sasa yeye alijikuta akivutiwa na Rais JFK,na hii club yao walipata mwaliko wa kwenda Ikulu,alikuwa mmoja wa waalikwa kutoka shuleni kwao,alijiapiza kuwa lazima apambane kufa kupona ashikane mkono na Rais Kennedy,na alimwomba mpiga picha kuwa akipata hiyo nafasi basi mpiga picha ahakikishe anampiga picha!bahati nzuri alifanikiwa kushikana mkono na Rais Kennedy na tukio hilo likapigwa picha ambayo alikuja kuitumia baadae wakati anagombea Urais miaka ya tisini!
Anasema hakumbuki kuni hasa alipenda kuwa mwanasiasa,anachokumbuka ni kuwa alitamani sana kuhudumia watu,kuna kipindi alitamani kuwa mwanamuziki mkubwa,baadae akatamani kuwa Daktari mkubwa,ila watu wengi walimwambia anafaa kuwa Mwanasiasa pengine kupenda kwake mambo ya haki za kiraia,na kuleta mabadiliko makubwa ya kisera kulifanya awe mwanasiasa
tutaendelea...........
nanyaro EJ