Uchambuzi Wa Kitabu 21; Rent To Own (Kununua Nyumba Kwa Kupanga Na Robert Irwin Cha Mwaka 2007)

Aliko Musa

Senior Member
Aug 25, 2018
156
240
Kuhusu Mwandishi; Robert Irwin

Robert Irwin ni mwekezaji kwenye viwanja na nyumba. Irwin ni mbobezi, kocha, na mwandishi maarufu sana katika nchi ya Marekani.

Irwin ametajwa kama mtaalamu namba moja na vyanzo mbalimbali vya taarifa. Irwin ameandika zaidi ya vitabu arobaini (40) vinavyohusu uwekezaji kwenye viwanja na nyumba.

Irwin amekuwa dalali wa viwanja na nyumba, mwenye nyumba (landlord) na mshauri wa watoa mikopo, madalali na wawekezaji kwenye viwanja na nyumba.

Irwin amekuwa na uzoefu wa ubobezi kwenye viwanja na nyumba kwa zaidi ya miaka thelathini (30).

Irwin anaishi kijiji cha Westlake huko Marekani, mji wa California. Irwin amekuwa mwelimishaji kupitia redio na Televisheni mbalimbali kuhusu uwekezaji katika viwanja na nyumba.

Baadhi ya vitabu alivyoandika Robert Irwin ni kama ifuatavyo;-

(a) How to get started in real estate investing (Jinsi ya kuanza kuwekeza kwenye ardhi na majengo).

(b) Tips and traps when negotiating real estate (Vidokezo na mitego wakati wa kunegoshieti majengo).

(c) How to find hidden real estate bargains (Jinsi ya kufikia maafikiano mazuri kwenye majengo).

(d) Home buyer's checklist (mwongozo wa mnunuzi wa nyumba).

(e) Tips and traps when buying a home (Vidokezo na mitego wakati wa kununua nyumba).

(f) Home renovation checklist (Mwongozo wa kukarabati nyumba).

(g) Buy, Rent And Sell (Nunua, Pangisha Na Uza Nyumba).

(h) Tips and traps for getting started as real estate agent (Vidokezo na mitego kwa dalali wa ardhi na nyumba).

(i) The home inspection troubleshooter (mtatuzi wa ukaguzi wa nyumba).

(j) How to invest in real estate with little or no money down (Jinsi ya kuwekeza kwenye majengo kwa kutumia mtaji fedha kidogo).

Huu ni uchambuzi wa kitabu cha Robert Irwin kiitwacho Rent To Own (kununua nyumba kwa kupanga cha mwaka 2007).

Utangulizi.

Kununua kwa kupanga nyumba ni njia ya kununua nyumba ambapo mpangaji hulipia nyumba kidogo kidogo kwa kutumia malipo ya kodi yake ya kila mwezi.

Kwa njia hii ya uwekezaji, mpangaji huitwa mpangaji mnunuzi na mwenye nyumba huitwa muuzaji mpangishaji. Robert Irwin anatushirikisha jinsi ya kununua nyumba kwa kupanga nyumba husika.

Manunuzi haya huambatana na makubaliano maalumu kati ya mwenye nyumba na mpangaji.

Ni vyema makubaliano yafanyike kwa njia ya maandishi mbele ya wakili ambaye ataanda au atahakikisha mkataba kati yako na mwenye nyumba.

SURA YA 01; Kwanini Unatakiwa Kumiliki Nyumba Yako.

Asilimia 99 ya wapangaji hutamani kutengeneza fedha kupitia nyumba za kupangisha. Wapangaji hawawezi kutengeneza fedha kwa kupanga nyumba.

Njia pekee ya kuanza kutengeneza kipato endelevu kupitia nyumba za kupangisha ni kumiliki nyumba hizo na sio kupanga.

Kumiliki nyumba ndipo ambapo faida hupatikana na sio kupanga nyumba. Unahitaji kumiliki nyumba za kupangisha ili uanze kutengeneza kipato endelevu na kipato chanya kila mwezi.

Muda ukiwa mzuri, nyumba za kupangisha huongezeka thamani ndani ya miaka michache tu. Hivyo wenye nyumba hunufaika kwa kupandisha kiasi cha kodi ya kila mwezi.

Muda ukiwa mzuri sana, nyumba za kupangisha huongezeka thamani mara mbili ya thamani ya mwanzo ndani ya mwaka mmoja tu.

Kati ya miaka 2000 hadi 2006, nyumba nyingi za mji wa kalifonia ziliongezeka thamani mara mbili ya thamani zao za mwanzo.

Faida Inapatikana Hapa Kwenye Ardhi Na Majengo.

Moja.

Mtaji fedha kwa njia ya mkopo wa majengo (leverage).

Mwanamahesabu wa kigiriki aitwaye Archimedes aliwahi kunukuliwa akisema "Give me a lever long enough and a fulcrum on which to place it and I will move the world".

Archimedes alikuwa anamaanisha kuwa ukiwa na nyenzo ndefu vya kutosha na mahali pa kusimama unaweza kuihamisha dunia.

Mikopo ya majengo ni nyenzo ambayo ukiitumia vizuri inaweza kufanya maajabu kwenye safari yako ya kujenga utajiri kupitia uwekezaji kwenye ardhi na majengo.

Robert anaendelea kutushirikisha kuwa kwenye ardhi na majengo, mikopo ya majengo ni nguvu anayoweza kuitumia mnunuzi wa majengo husika.

Mfano; unaweza kuchukua mkopo wa kununulia nyumba inayouzwa milioni kumi (10,000,000). Ili uweze kupata mkopo wa kununulia nyumba hii, utatakiwa kuwa na kiasi fulani cha fedha kulingana na benki husika.

Kwa kawaida utatakiwa kuwa na 10% ya bei nyumba unayotaka kununua. Hivyo unatakiwa kuwa na milioni moja ili upewe mkopo wa kununulia nyumba ya milioni kumi.

Kwenye maeneo ambayo majengo hupanda thamani kwa 10% kila mwaka. Nyumba unayonunua kwa milioni kumi mwisho wa mwaka itakuwa na thamani ya milioni kumi na moja.

Hivyo utakuwa umetengeneza kipato cha 100% ya milioni moja uliyowekeza kwenye nyumba ya bei ya milioni kumi. Kwa benki zinazotoa mikopo ya majengo ya zaidi ya 90% ya bei ya nyumba, utakuwa umetengeneza faida za zaidi ya 100% ifikapo mwisho wa mwaka.

Mbili.

Mfumuko wa bei (price infalation).

Mfumuko wa bei unaweza kuwa mbaya au mzuri kufuatana na mtu mwenyewe. Kama unamiliki nyumba na ardhi mfumuko wa bei unakunufaisha.

Kama umetunza fedha kwenye benki, mfumuko wa bei unakula utajiri wako. Ndani ya miaka kadhaa utajiri wako utakuwa umepungua sana.

Mfano; gari linalouzwa milioni kumi (10), mfumuko wa bei ukiwa ni 4% utatakiwa kununua gari hilo kwa milioni 10.4. Hii ni kwa sababu milioni kumi imeliwa na mfumuko wa bei.

Kwa lugha nyingine, milioni kumi imepungua nguvu ya kununulia gari la thamani ya milioni kumi. Kupungua kwa nguvu ya shilingi ya kununua bidhaa na huduma kwa kila mwaka ndiyo huitwa MFUMUKO WA BEI.

Mfumuko mkubwa wa bei huchochea kuongezeka kwa thamani ya nyumba ndani ya muda mfupi. Faida kubwa itaonekana endapo utaunganisha nguvu ya mikopo ya majengo (leverage) na matokeo ya mfumuko mkubwa wa bei.

Tatu.

Kukusanya mtaji (Equity return).

Hapa ni mahali pa tatu ambapo faida kwenye uwekezaji wa nyumba hupatikana. Mtaji hukusanywa kila mwezi kwa kulipia mkopo wa majengo kila mwezi.

Mtaji unaongezeka kila mwezi kwa kulipa marejesho ya mkopo wa majengo. Hii inakuwa kweli endapo mnunuzi ameomba mkopo wa majengo ambao marejesho ya kila mwezi hujumuisha mkopo na tiba (amortized loans).

Haiwezekani kukusanya mtaji fedha endapo umepewa mkopo wenye marejesho ya mwezi ya riba tu (interest-only mortgages).

Hii ni sababu mojawapo ya kuepuka mikopo ya majengo ya marejesho ya mwezi ya riba tu bila kujumuisha mkopo (principal).

Kwa sababu hiyo hiyo, unatakiwa kuweka shabaha kwenye kupata mikopo ya majengo ambayo marejesho yake ya kila mwezi hujumuisha mkopo (principal) na riba.

Kukusanya mtaji fedha ni njia ya nguvu kabisa ya kutengeneza fedha kwa miaka mingi. Kila unapofanya marejesho ya kila mwezi unakuwa unakusanya mtaji fedha.

Baada ya mwaka wa mwisho wa marejesho kukamilisha marejesho utakuwa hudaiwi chochote na hivyo nyumba yako itakuwa mtaji fedha kwa kiasi ulichonunua jumlisha thamani iliyopanda kwa miaka husika.

Mikopo ya majengo ambayo riba yake hubadilika (adujstable-rate loan), kukusanya mtaji huathiriwa na mabadiliko ya riba ukilinganisha na riba ya mwanzo.

Faida Za Kuwa Mwenye Nyumba Dhidi Ya Kuwa Mpangaji.

Moja.

Mwenye nyumba anaweza kutumia nyumba yake kupata dhamana ya mkopo wa majengo kwa ajili ya kukuza uwekezaji wake.

Mbili.

Mwenye nyumba anaweza kupata punguzo la kodi kutoka kwenye riba ya mkopo wa majengo. Mpangaji hawezi kupata punguzo la kodi serikalini kutokana na riba ya mkopo kwenye nyumba anayoishi.

Tatu.

Mwenye nyumba hunufaika na mfumuko wa bei (price inflation) wakati wapangaji hawawezi hawawezi kunufaika na mfumuko wa bei. Mfumuko wa bei huwafilisi zaidi na zaidi wapangaji kwa kuendelea kuwa wapangaji.

Nne.

Usalama mdogo kwenye nyumba za kupanga.

Mwenye nyumba anakuwa salama zaidi kwa kuishi kwenye nyumba yake ukilinganisha na wapangaji.

Matukio ya kiuhalifu yameonyesha kuwa mengi zaidi kwenye nyumba za kupangisha ukilinganisha na nyumba ambazo zinakaliwa na wenye nyumba wenyewe.

Kwa kawaida, wenye nyumba hushirikiana kulinda nyumba zao na mali zao kwenye nyumba zao na nyumba za majirani zao.

Wapangaji hufikiria kuwa ni wapitaji tu. Huwa hawajali kuhusu mali na nyumba ambazo wamepanga.

Tano.

Wenye nyumba huishi kwenye mitaa ya utulivu.

Wakati huohuo wapangaji huendelea kuishi mazingira ya idadi kubwa ya watu. Wapangaji huvumilia maeneo yenye kelele kwa sababu hawana namna ya kufanya.

Wenye nyumba huchagua mitaa yenye utulivu na idadi ndogo ya watu. Wenye nyumba wanaweza kujitengenezea sheria ndogo kwa ajili ya kuulinda utulivu wa mtaa wao.

Wapangaji kwenye apatimenti huishi mazingira yenye kelele na mazingira ya idadi kubwa ya watu. Huku wenye nyumba huishi kwenye nyumba zao za vyumba vichache vya kulala bila kelele na kuzungukwa na watu wengi.

Nani ambaye hapendi hali ya hewa ya utulivu na isiyo na kelele za ajabu ajabu?. Nani anayependa kuishi nyumba za nyumba vingi vya kulala kama hosteli za wanafunzi?.

Sita.

Mwenye nyumba anaweza kutumia nyumba yake kukusanya mtaji zaidi na zaidi (Equity return).

Wapangaji hawawezi kukusanya mitaji fedha kwa kutumia mikopo ya majengo kwa kurejesha mkopo kila mwezi.

Saba.

Ni mali ya kustaafu kwa wenye nyumba.

Mwenye nyumba anaweza kuitumia nyumba yake kama mali kwa ajili ya kuitumia akiwa mzee. Hapa mwenye nyumba anauza nyumba yake baada ya kuishi miaka mingi kwenye nyumba hiyo kwa bei kubwa.

Kisha hununua nyumba ya gharama nafuu, fedha zinazobaki hutumiwa kwa ajili ya mahitaji yao ya kila siku. Wengi watashindwa kabisa kuwa na fedha za kutumia uzeeni kwa kuhifadhi benki na njia nyingine.

Hii ni kwa sababu inahitaji nidhamu ya miaka mingi na kutunza kiasi kikubwa cha fedha kwenye benki na kampuni za uwekezaji ukilinganisha na kumiliki nyumba.

Hivyo, bila kumiliki nyumba mamilioni ya watu watakuwa tegemezi sana kwenye kipindi ambacho hawana kazi za kufanya kwa sababu ya umri wao mkubwa.

Chanagamoto Za Kumiliki Nyumba.

Moja; ukarabati wa majengo.

Mbili; maboresho ya nyumba.

Chanagamoto hizi mbili ndivyo humchosha zaidi mmiliki wa nyumba. Hivyo utahitaji kujiandaa vyema ili uweze kuendelea kumiliki nyumba hiyo kwa ubora mzuri kwa miaka mingi.

Kwa Sababu Hizi Ni Bora Kupanga Kuliko Kumiliki Nyumba.

Moja.

Kuishi kwenye eneo kwa muda mfupi.

Sababu za kuishi kwa muda mfupi kwenye eneo husika zinaweza kuwa ni ajira za muda mfupi, utafiti wa muda mfupi, uwekezaji wa muda mfupi, biashara za muda mfupi, masomo/elimu, matibabu, majanga ya asili na kadhalika.

Pia, kutatua migogoro ya ardhi au nyumba unazomiliki na changamoto zingine za kisheria.

Miezi sita hadi mwaka mmoja ni kipindi kifupi cha kukufanya umiliki nyumba. Lakini kwenye hali nzuri sana ya masoko ya ardhi na nyumba, unaweza kumiliki nyumba kwa ajili ya kuuza ndani ya muda mfupi.

Mbili.

Tofauti kubwa kati ya gharama za kupanga na gharama za umiliki wa nyumba.

Uwepo wa tofauti kubwa kati ya gharama za upangaji na gharama za umiliki wa nyumba ni sababu nyingine ya kushawishi uwe mpangaji wa nyumba badala ya kuwa mmiliki.

Kukaribiana kwa gharama za upangaji na gharama za umiliki wa nyumba humaanisha, umiliki wa nyumba unalipa zaidi kuliko upangaji wa nyumba.

Dhana/mawazo (assumptions) unayotakiwa kufahamu wakati wa ukadiriaji wa gharama za upangaji wa nyumba ni kama ifuatavyo;-

✓ Muda wa umiliki; kwa wastani watu humiliki nyumba kwa miaka 7 hadi 9.

✓ Ongezeko la kodi; je ni kiasi gani kodi inaongezeka kila mwaka?.

✓ Riba ya mkopo wa majengo; ni kiasi gani cha riba hutolewa kila mwaka kwenye mkopo uliopata?.

✓ Kodi ya ardhi na jengo; mara nyingi huongezeka kwa kiasi kidogo kila mwaka.

✓ Gharama za mauzo; kwa kawaida kila mauzo au manunuzi hugharimu 7% hadi 10% ya bei ya kuuzia nyumba.

✓ Gharama za ukarabati za mwaka; unatakiwa ufahamu jumla ya gharama za ukarabati na maboresho ya nyumba ya kila mwaka.

✓ Ongezeko la thamani; kwa miaka hamsini (50) iliyopita, nyumba zimeongezeka thamani kila mwaka kwa 5%.

✓ Kukusanya mtaji (equity return); mtaji huu hupatikana kwenye mikopo ya majengo ya marejesho yanayojumuisha riba na mkopo (principal).

Baada ya kufahamu dhana hizi, utatakiwa kutumia kanuni maalumu ambayo Robert ametushirikisha kwenye kitabu hiki.

Tatu.

Kushuka kwa soko la nyumba za kupangisha.

Kodi za nyumba zinapokuwa chini sana kuliko gharama za ujenzi wa nyumba ni bora kupanga kuliko kumiliki nyumba. Hii inatokea kwenye hali mbaya ya masoko ya upangishaji wa nyumba.

Tangu kutokea kwa anguko la uchumi wa kidunia miaka ya 1930, mzunguko wa ardhi na majengo umekuwa ni jumla ya miaka 14 tu.

Miaka saba (7) mzunguko unakuwa kwenye ukuaji na miaka saba (7) inayofuata mzunguko unakuwa kwenye hali mbaya.

Hii ni sehemu ya uchambuzi wa kitabu kiitwacho Rent To Own by Robert Irwin (Nunua Nyumba Kwa Kupanga).

Muhimu; Ada ya kuwa mwanachama wa kundi la uchambuzi wa vitabu ni shilingi elfu tano (Tshs.5,000/=) kwa kila mwezi. Lipia leo kujiunga na kundi hili liitwalo REAL ESTATE BEGINNERS.

Rafiki yako,

Aliko Musa.

WhatsApp; +255 752 413 711
 
mkuu naomba hiki kitabu
 
Back
Top Bottom