Stabilaiza
JF-Expert Member
- Jul 11, 2012
- 1,843
- 1,143
Kuna mambo kadhaa ambayo yanaonekana katika hotuba ya rais aliyoitoa UDSM hivi karibuni. Uchambuzi huu unajikita katika kuonyesha picha kubwa kuhusu dhana ya Kilaza. Kwa ufupi dhana hiyo aliyotumia rais inamapungufu mbalimbali ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiusalama, kitabia na uongozi
Mapungufu ya kisiasa ya hotuba ya rais
Kwa kuwaita vilaza wanafunzi wa UDOM waliorudishwa nyumbani ni sawa na kuwatukuna wapiga kura wake waliomwingiza madarakani au wazazi, walezi, familia, ndugu na marafiki wa wanafunzi hao. Hii kisiasa si jambo zuri kumtukuna mpiga kura wako
Mapungufu ya kiuchumi, kijamii na kiusalama ya hotuba ya rais
Rais anaona kuwa Watanzania waliokosa nafasi ya kujiunga vyuo vikuu na wanaofanya kazi katika sekta nje ya vyuo vikuu ni vilazi. Tafsiri yake ni kwamba rais anaona kuwa sekta nyingine si bora na muhimu kama vyuo vikuu. Hii ni kosa kubwa sana kiuchumiu maana vyuo vikuu pekee haviwezi kuendesha uchumi wan chi. Kauli hii ya vilaza waliosoma vyuo vya saizi yao inamaanisha kuwa sekta na taaluma nyingine si muhimu. Madereva, polisi, wanajeshi, manesi, mafundi waliosoma VETA na wanaofanya kazi sehemu nyingine ni vilaza. Kauli hiyo pia inaleta ujumbe wa matabaka katika nchi. Kwamba kuna tabaka muhimu katika nchi na nyingine si muhimu kwa kuwa linavilaza. Kwamba hata walinzi wa viongozi, wanajeshi na polisi wetu nao kwa kuwa walienda vyuo vya saizi yao wanaingia katika kundi la vilaza. Hii ni kauli mbaya kabisa kuwahi kutolewa na rais wa nchi. Pia kusema kuwa aliwafukuza wanafunzi wa St. Joseph kwa kuwa waligoma na kuongeza kuwa kama UDOM wangegoma angewafukuza wote inaonyesha kuwa rais ni wa visasi.
Mapungufu ya uongozi wa hotuba ya rais
Kiongozi yoyote anawajibu wa kuhamasisha watu wake katika kufikia malengo ya taasisi anayoiongoza. Kuwaita wanachi unaowangoza kuwa ni vilaza ni kuwakatisha kabisa tamaa badala ya kuwatia moyo. Ndiyo maana wengine tulisema kabla kuwa rais wetu huyu si kiongozi bali ni mtawala.
Mapungufu ya kitabia ya hotuba ya rais
Kwa kutumia lugha ya kuudhi kuwaita vilaza watu waliofukuzwa badala ya kuwatia moyo inaonyesha kuwa rais hajali kuumiza mtu kwa maneno ya aina hiyo. Katika taaluma ya tiba ya binadama kuna kitu kinaitwa sadism. Hii ni tabia ya kibinadamu kujisikia furaha pale anapoumiza wengine au anapoona binadamu mwenzake anaumia. Ingawa mwenyewe alishajitetea kuwa si mtu katili lakini matendo yake yanamwonyesha kinyume chake.
Hitimisho
Kuna mambo mengi sana yameshajitokeza katika utawala wa awamu ya tano ambayo ni mabaya kabisa ikiwemo staili ya kufukuza wafanyakazi, kuwasumbua wafanyabiashara waliotunza sukari yao katika stoo yeye anasema wameficha, kuvunja nyumba za watu ingawa bila hata huruma na kuzingatia utapeli wa wafanyakazi wa ardhi na sasa anafukuza wanafunzi bila huruma na kuwatukana. Rais wa nchi anatakiwa awe ni kiongozi si mtawala asiyejali maumivu ya wananchi wake.