Emc2
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 16,808
- 16,966
Bado kuna sehemu uchaguzi haujamalizika, lakini haituzuii kufanya uchambuzi mpaka sasa kwa kuwa mpaka sasa sehemu kubwa uchaguzi umefanyika.
Kusema kweli vyama vya upinzani vimejitahidi. Tunasema hii ndio demokrasia. Lakini nina chelea kusema kwamba jitihada ya vyama vya upinzani haikutakiwa iwe hivi. Vilitakiwa kuwa zaidi ya hapo.
Mimi nimeshangaa imekuwaje ngome kuu ya upinzani Jijini arusha kwamba ccm imepata viti vingi. Hii ni ishara gani kwa vyama vya upinzani hususani CHADEMA.
Vilevile kwa upande wa mikoa ya mtwara na lindi nilitegemea CUF wangepata viti vingi lakini hapakuwa hivyo.
Sasa basi kwa upande wa upinzani wameshindwa kuutumia mwanya wa SCROW kujipatia ushindi mnono. Hii ni hali mbaya sana kwa vyama vya upinzani.
Nieshangaa pia kwanini wilaya ya hai ambayo ametokea mwenyekiti wa CHADEMA, CCM imejinyakulia viti vingi.
Kwa mantiki ya maelezo yangu vyama vya upinzani bado havijawa na nguvu na vinahitaji mda. Pia wanatakiwa wabadili namna ya uendeshaji wa siasa. Waache siasa za vurugu.
Kwa upande mwingine CCM wanatakiwa kuamka kutoka usingizini. Huu uchaguzi wa uwe chachu ya kujipanga ki mkakati. Na sio kubweteka tu.
Nawaomba tuchambue kwa hoja sio matusi na vioja. Hii ni nchi yetu sote.