OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 52,035
- 114,457
Kama tunavyofahamu Guru wa Sheria na aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Katiba Mpya Prof.Kabudi Palamagamba ameteuliwa kama mbunge wa viti maalumu.
Uteuzi huu ni mwendelezo wa kuteuliwa kwa waliokuwa wajumbe wa tume ya katiba,awali akiteuliwa Bwn.Polepole na kufuatiwa Mwenyekiti Warioba kuwa mwenyekiti wa moja ya bodies
Kutokana kumbukumbu zilizopo kwa wateuliwa wa rais huweka kando misimamo na weledi wao na kuwa kitu kimoja na mteuaji!Ajabu hii hufanyika pia hata kwa wanasheria wasomi. Tumeshuhudia Dr.Mwakyembe akinukuu katiba na sheria kinyumenyume. Sote tulisikia akisema katazo la mikutano ya kisiasa na maandamano ni kwa mujibu wa katiba lakini mpasa sasa hajawahi kunukuu kifungu cha katiba wala sheria......list ni ndefu
Ni kwa nini tusiamini kuwa Prof.Kabudi hatakuwa anaongea wakati wa kula?! Kama yamewezekana kwa Dr.Ayubu Rioba,H.Polepole kwa nini isiwe kwa Prof.Kabudi?Tutegemee toka kwa muumini wa katiba Prof.Kabudi kwamba katiba sio kipaumbele tuache rais anyooshe nchi kwanza? Serikali tatu je?
Maono yangu yanaonyesha Prof.Kabudi anaenda kuteuliwa kuwa waziri wa sheria na katiba baada ya Dr.Mwakyembe kutokuonyesha dira yeyote! Je waziri mtarajiwa huyu atawezaje kufunguka na matonge mdomoni?
Wadau mnifikishie