Uchambuzi kuhusu Tottenham Hotspur

Dec 28, 2016
50
52
Habari za asubuhi wakuu

Nimekaa chini kwa mda mrefu na kuamua kuichambua Tottenham ya Mauricio Potchetino kwa ufupi tu

Tangu Mauricio Potchetino ameichukua hii team kumekuwa na uimara mkubwa sana, team inacheza mpira mzuri na wa kueleweka, team ina spirit nzuri sana ndani ya uwanja, kwa kifupi imekuwa sio team ya kubeza kwa miaka ya hivi karibuni....lakini team hii ni kama imeganda palepale ilipo na miaka yote ya Potchetino,ndio imekuwa bora lakini kama ubora huu umekuwa fixed, hauongezeki wala haupungui

JE WANAKWAMA WAPI??

1. LIMITED TRANSFER BUDGET?? MAYBE

Tottenham chini ya Daniel Levy kutoka miaka ya 2001 kama sijakosea imekuwa team ya kupanda na kushuka ,imekuwa team ambayo ni nzuri ya kawaida ,imekuwa team ya kupambana na wakubwa ndani ya uwanja, ndani ya mda wote huo haijawa team kubwa, haijawa team ya kupambania makombe makubwa

Misingi ya team huu imekuwa kujenga team ya ushindani kwa kuchukua vijana wadogo ambao wana potential ya kuwa wachezaji wazuri, falsafa hii ilifanikiwa sana siku za nyuma, team kama Arsenal,Manchester United zilinufaika sana na mfumo huu, wakati Mauricio Potchetino anaipokea team ilikuwa na young players wengi, na yeye aliongeza vijana wengi na kuwakuza baadhi yao kutokea team ya watoto..muunganiko wa watoto hao ndio Tottenham ya sasa ambayo tunaiona...matumizi makubwa ya watoto yametokana na ufinyu wa hela, Tottenham haina budget ya kwenda sokoni kuchukua wachezaji wakubwa wa kuboresha kikosi chao na kukifanya kuwa hatari,angalia mfano Liverpool ilivyobadilishwa na individual qualities za Allison, VVD, Mane, Salah, Fabinho, Tottenham wanakosa fungu la kuongeza individual particulars kwenye kikosi chao, hivyo wanalazimika kuwatumia watoto hata kama hawana uwezo wa ku offer world class moments mara kwa mara hasa wakati team imeelemewa

Imeishia kusajili wachezaji kama Wanyama

Msimu uliopita wameweka rekodi ya kuwa team ambayo haijafanya usajili wowote kwenye ligi ya Uingereza

2. AVERAGE PLAYERS WENGI WENYE MORALI

Tottenham inacheza mpira mzuri ambao unafanya mashabiki tuone kama ni team ambayo imekamilika, hata upinzani wanaounyesha vs big team unatupumbaza na kuona hii team imetimia, jambo ambalo si kweli,team hii ina watu wengi sana ambao performance zao ni nzuri kutokana na mfumo wa team, team work na jitihada zao zinafanya waonekane bora ila wengi wana uwezo wa kawaida sana

Starting from Danny Rose,Trippier, Wanyama, Dier, Dele Alli, Winks, Moura..hawa wote ni first eleven players,wanacheza with nothing special to offer ,wanacheza vizuri lakini wana individual mistakes ambazo zinaigharimu team,kama Tottenham wanataka kuwa team kubwa wanahitaji kutafuta wachezaji bora zaidi ya hao..wakubali kuwekeza sokoni na kuchukua wachezaji ambao wapo gifted tactically

3. FEELINGS OF BEING A SMALL TEAM

Team ambayo ilikuwa ndogo inapata wakati mgumu sana kufikia hatua ya kujiona yenyewe ni team kubwa, team kubwa, zina kawaida ya kupata matokea at any cost, team kubwa zinapambana msimu mzima, team kubwa zina react positively baada ya matokeo mabaya, team kubwa zinapambania makombe in and out, team kubwa ikipoteana msimu huu au misimu kadhaa, ikirejea inaendelea na spirit ile ile ya ukubwa wako

Tottenham wamekikosa hiki, hata namna wanavyocheza uwanjani wanaonekana bado ni team ndogo, team kubwa zinaingia kwa mentality ya kupata matokeo katika kila mechi

4. SQUAD

Pamoja na kwamba wana watu wengi wa kawaida, bado muunganiko wao ni mzuri,changamoto inakuja anapoumia mchezaji mkubwa mmoja, msimu huu majeraha ya Harry Kane yaliwapunguzia kasi hawa jamaa hasa kwenye mechi za ligi

5. MAURICIO POTCHETINO???

Baada ya mechi ya fainali ya klabu bingwa alisema project ya miaka 5 imeisha,kama Tottenham Hotspur wanataka kumbakisha inabidi waanzishe project mpya ambayo itampa uhuru wa kuchukua wachezaji wazuri na kuimarisha kikosi ili kuifanya team kuwa ya ushindani zaidi

Binafsi nimemtizama Potchetino kwa mda mrefu sana na kuhisi mbinu zake zipo limited...kwa kubaki Tottenham Hotspur sitarajii muujiza kutoka kwake, nafikiri angeenda team kama Juventus ingemsaidia kuimarisha uwezo wake kama kocha, aende kwenye winning team ili apate makombe, then inaweza kumfanya awe manager mzuri

ARSENAL MANCHESTER UNITED, CHELSEA...safari ya maisha yetu itakuwa ngumu sana msimu ujao kama wachezaji tunaosajili ndio hao, kwa sasa Tottenham ni team bora kuliko sisi ila sio kubwa kuliko sisi

SWALI LA NYONGEZA- TOTTENHAM WATAFANYA MAKUBWA MSIMU UJAO UCL KAMA WALIVYOFANYA MSIMU HUU??

#STEPH.P.M
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom