UCHAMBUZI: Kauli ya kocha Gamond kuwa Yanga haina kikosi kipana imebeba ujumbe uliotumwa nje na ndani ya klabu ya Yanga

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
3,647
9,228
Kwa tunaopenda kusoma between the line, Gamond amenukuliwa akisema Yanga haina kikosi kipana, kwani amewahi kujaribu kufanya rotation na akaambulia kupoteza dhidi ya ihefu, alipojaribu kwenda na kikosi cha kwanza kwa kila mechi akaanza kupokea lawama, ameyasema hayo ni baada ya kumalizika kwa mchezo wa yanga na KVZ ulioisha kwa sare ya bila bila.

Huu ni ujumbe kwa wachezaji wasiojituma kuwa wataachwa? pia huu ni ujumbe kwa mashabiki wote wa Yanga kwamba waache kelele za kutaka rotation ifanyike? pia hii ni salamu kwa upande wa pili kuwa kuanzia kesho kutwa tegemeeni kuona full mkoko katika kombe la mapinduzi.

Saikolojia inasema kwamba “RATIONALIZATION is a defense mechanism (ego defense) in which apparent logica reasons are given to justify behaviour that is motivated by uncouscious behaviour instictual impulses".

Endapo GAMOND ataaminiwa tutegemee thank you za kutosha dirisha dogo na kubwa, pia mlionza kupongeza rotation tegemeeni full mkoko game ijayo, msije kuwa suprised.

Nawasilisha.
 
Kuna watu walipiga kelele humu, kwanini Moloko apangwi, sijui Farid Mussa anakiwasha lakini kocha hampangi. Niliwahi kuwaambia ukiachana na first eleven ya Gamondi hakuna mchezaji mwenye kiwango kinachofanana na wanaoanza.

Gamondi kawachezesha wote angalau Sureboy pekee ndiye mchezaji anaweza kukaa hata sub ila zaidi ya hapo sijaona mchezaji wa kusema Gamondi anamuingiza ili akabadilishe mchezo dhidi ya Al Ahly au Belouizdad.
 
Kuna watu walipiga kelele humu, kwanini Moloko apangwi, sijui Farid Mussa anakiwasha lakini kocha hampangi. Niliwahi kuwaambia ukiachana na first eleven ya Gamondi hakuna mchezaji mwenye kiwango kinachofanana na wanaoanza. Gamondi kawachezesha wote angalau Sureboy pekee ndiye mchezaji anaweza kukaa hata sub ila zaidi ya hapo sijaona mchezaji wa kusema Gamondi anamuingiza ili akabadilishe mchezo dhidi ya Al Ahly au Belouizdad.
jana OKRAH alivyoanguka chini kamera za azam zilimulika Gamond akaonekana anakuna kichwa ni kama vile anayecheza hiyo namba kwa wakati huu tofauti na okrah haaminiki, itafute hiyo ciip utaona.
 
GAMOND ameaminiwa ngushi kauzwa kwa mkopo, je nani amafuata ?
 
Back
Top Bottom