Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,779
- 18,747
Waziri Mkuu akiongea katika kikao cha maafisa Utamaduni na maafisa michezo Jijini Dodoma, alishangaa kwa nini Tanzania haina kocha hata mmoja anayefundisha nje ya nchi, hata Burundi au Rwanda lakini yenyewe ikiwa inachukua makocha wa kigeni kutoka nchi hizo.
Kinachoshangaza zaidi ni Tanzania ndio nchi inayoongoza kuwa na wachambuzi wengi wa mpira ambao utawasikia wanavyowakosoa makocha wa nje, wanavyokosea kufundisha na kupanga timu zao na wanavyowakosoa wachezaji wa ndani na nje ya nchi wanavyofanya makosa ya kiufundi uwanjani na kuzigharimu timu zao.
Utamsikia mchambuzi wa Tanzania akimchambua kocha kama Mikel Arteta akielezea ni kwa jinsi gani alivyopanga kikosi vibaya hadi kupelekea timu yake kupoteza mchezo, au wachezaji wa Arsenal walivyokuwa wakifanya makosa yaliyopelekea timu yao kufungwa, au wakikosoa kocha wa Yanga au Simba.
Je, ni kwanini Tanzania tuna wachambuzi mahiri sana lakini hatuna makocha?