Uchambuzi: Hivi tunataka makinika (masalia) ya dhahabu au hata ile dhahabu inayosafirishwa kwa siri?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,885
Nimefuatilia kwa karibu sana mjadala kuhusu mchanga wa dhahabu unaokwenda nje ya nchi toka Rais John Pombe Magufuli atangaze kuuzuia bandarini na baadae kuunda kamati mbili na kamati moja kuwasilisha matokeo ya uchunguzi wao kwa Rais na Rais kuchukua hatua!.

Nimefurahishwa kwa jinsi watanzania walivyoonesha hasira zao baada ya ripoti kuainisha namna biashara hii ilivyo,nimeshuhudia,nashuhudia na nitashuhudia mijadala mikali kutoka kwa watu wa kada mbali mbali!.

Baadhi ya wabunge wametoa maoni yao,wanasheria wameonesha umahiri wao katika kuzichambua sheria zinazoisimamia sekta hii,watumiaji wa mitandao ya kijamii wamejadili na bado wanajadili,vyombo vya habari na wasomi vyuo vikuu wanajadili,huko vijiweni kwenye kahawa napo wanajadili kila mtu kwa mtazamo wake!.

Nilichogundua mijadala yetu haijadili tatizo la msingi kwenye sekta ya madini,tunajadili sehemu ndogo sana kwenye sekta ya madini na katika hili hata wataalam serikalini wamemua nao kujadili hivyo hivyo!.

Kwa nini nasema hivi?

1.Makinikia yanayojadiliwa ni kutoka eneo moja tu la Migodi ya Kahama,na tunajadili masalia ya dhahabu yanayokwenda tafutwa kwenye mchanga,hatujadi dhahabu wanayoivuna hapo Kahama na kuisafirisha kwa ndege zinazotua migodini,huko ndiko nchi inapopata hasara siyo kwenye michanga,huko ndiko serikali inapopigiwa kwa kupewa mrabaha wa asilimia 4,huku wawekezaji wakikwapua asilimia 96,huko ndiko kwenye usiri mkubwa kati ya serikali na wawekezaji!

Mpaka sasa tunajadili masalia ya dhahabu!hatujadili tunachopigwa kwenye dhahabu yenyewe inayoondoshwa kila kukicha kwa mandege makubwa yanayotua migodini!.Tuamke watanzania,hayo makinikia ni mabaki tu,tukishapata suluhisho kwenye masalia(Makinikia),tuanze mjadala wenyewe kwenye madini!.

2.Siyo migodi yote inasafirisha mchanga,kwa uchunguzi wangu,nimebaini Mgodi wa Geita hakuna mambo ya kusafirisha hayo makinikia,pale Geita mwekezaji aliyejibadilisha jina kutoka Ashanti mpaka GGM,yeye hasafirishi michanga kama wanavyofanya Acacia kule kahama,pale Geita,ndege zinatua nchini na kubeba matofali ya dhahabu na chakushangaza nasikia hata uwanjanwa ndege wa Mwanza hazitui,zinatoka Ulaya moja kwa moja mpaka Geita na kubeba dhahabu.

Mgodi wa Geita naambiwa ndiyo mgodi wa pili kwa ukubwa barabi Afrika,mwekeza yule hasafirishi hayo matakataka(makinikia) kwenda kusaka mabaki,yeye hubeba mzigo,anaupeleka nje,anauza halafu serikali yetu inapewa asilimia 4 ya mapato baada ya kuuza na mwekezaji anabaki na asilimia 96!.

Kwa taarifa nilizonazo,watu wetu wa serikali hawaruhusiwi kuingia "Strong room",hiki ni chumba cha kuhifadhia dhahabu,wala hatujua kiasi cha dhahabu kinachoondoka,tunapewa ripoti tu,huku ndiko tunapopigwa,huku ndiko kwenye siri kati ya serikali na wawekezaji na serikali muda wote imegoma kuiweka wazi mikataba hii!.

3.Kule Mererani na hata Nyamongo,hawasafirishi makontena ya mamichanga kwenda kusaka mabaki(Makinikia),huko wawekezaji wanapata dhahabu na Tanzanite safi na kusafiri nayo,wao ndiyo wanajua wamebeba kiasi gani cha madini,mwisho wa siku wanakwambia kiasi walichopata,mwisho wa siku wanakupa 4% huku ndiko tunapopigwa kweli kweli,achana na hiki kipigo cha makinikia,hiki ni cha mtoto,twendeni huko kwenye siri kati ya serikali na wawekezaji!.

4.Mikataba ni siri,mpaka sasa baadhi ya vyombo vya habari,wabunge tena baadhi wamefanikiwa kuuona mkataba mmoja tu kati ya serikali ya mwekezaji,ni mkataba wa Mgodi wa Buzwagi uliovuja mwaka 2007,mikataba mingine yote imebaki kuwa siri kati ya serikali na mwekezaji!.

Huu mjadala unaoendelea sasa,tunajadili na kulia na wizi kwenye mabaki,hebu tukajadili wizi uliopo kwenye madini yenyewe,ikiwa hayo masalia ya madini yaliyomo kwenye mchanga yamekutwa na dhamanj ya shilingi Trilion 1.4

Hivi madini wanayoyabeba kwenye mandege yanayoruka toka kwenye nchi zao na kutua kwenye migodi yana thamani ya shilingi ngapi?!.

Tunachokifanya ni mfadhabiashara wa kuku analalamika wizi uliopo kwenye bei ya vichwa vya kuku na miguu,badala ya kuchambua wizi uliopo kwenye vidali,mapaja ya kuku n.k!.

Hongera Rais kwa hili,sasa hebu tuhamie kwenye biashara yenyewe!.Watanzania wajue haya makinikia yapo Kahama tu,kwenye mgodi mkubwa wa Geita na Nyamongo hakuna mambo ya michanga sijui makinikia!.Huko mamia ya matofali ya dhahabu yanaoandishwa ndege na kuiacha Geita hoooooiiii,wenyeji masikini wa kutupwa!.
 
Back
Top Bottom