damian marijani
JF-Expert Member
- Jan 31, 2010
- 695
- 458
Habari zinazohusiana na uchakachuaji wa mafuta ya vyombo vya moto zimekuwa zikionekana mara kwa mara katika vyombo mbali mbali vya habari. Habari hizi zinakera kwani tuna vyombo au taasisi ambazo zinaweza kudhibiti hao wamiliki wa makampuni ya mafuta. Baya zaidi ni kuwa wahanga wa vitendo hivi ni wamiki wa magari. As a result ya kuwekewa hayo mafuta yaliyochakachuliwa, magari yao yanaharibika na kusababisha gharama kubwa ya matengenezo.
La pili kuhusiana na mafuta, utagundua kuwa vito vingi havina Unleaded Petrol, hii inasababisha kuharibika kwa magari ambayo yametengenezwa kwa mfumo wa kutumia petol ya unleaded. Hivyo basi wote wenye magari hayo wanapata shida kupata unleaded petrol kwenye vituo vya Puma na Total.
Swali ninalouliza ni hivi, inakuwaje sisi authorities kama Ewura na wengine wanaohusika na kuratibu na kusambaza mafuta kushindwa kwenda na wakati haswa wakati huu ambao nchi nyingi zinasitisha utumiaji wa leaded petrol. Hivi sasa nchi niyingi zimebadilisha leaded petrol na aina nyingine ya petrol ambayo inaweza kutumika kwenye magari ya zamani ambayo hayana uwezo wa kutumia Unleaded petrol.