Uchaguzi wa Zanzibar: Watakaoshiriki washiriki kwa amani na watakaosusia wasusie kwa amani

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,375
Wadau, amani iwe kwenu.

Nchi nyingi zimeingia kwenye machafuko baada ya uchaguzi Mkuu wa nchi husika. Hii ni kutokana na hulka ya kibinadamu kuwa anayeshindwa hakubali kushindwa na anayeshinda humkejeli aliyeshindwa. Siasa za nchi si sawa na upinzani wa Simba na Yanga. Siasa ndiyo hutoa mustakabali wa taifa husika. Siasa ikienda fyongo, hakuna kitakachonoga.

Tunapoelekea kwenye Uchaguzi wa Zanzibar ambao umepangwa kufanyika Machi 20, mazingira ya uchaguzi huo si mazuri. CCM wamejipanga kisawasawa kushiriki uchaguzi huo. Chama Kikuu cha upinzani CUF wamejipanga kisawasawa kususia uchaguzi huo. Hapa CUF wamehiari kuwa nje ya siasa za Zanzibar kwa miaka 5 ijayo. Haijajulikana ni aina gani ya siasa watakayoshiriki hasa kutokana na kuwa nje ya serikali na bunge. CCM itakuwa inajitanua katika maeneo yote kwa asilimia 100. Uwakilishi pekee wa CUF ni kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambako naamini ndiko CUF watakakopenyezea mambo yao.

Wito wangu kwa Wazanzibari ni kwamba, ZEC wametangaza tarehe ya Uchaguzi. Hakuna chombo chenye mamlaka ya kutengua maamuzi hayo ya ZEC isipokuwa ZEC wenyewe. Waliotangaza kushiriki naamini kuwa wamefanya hivyo bila ya shinikizo kutoka upande wowote. Na wale waliosusia, naamini kuwa wamefanya hivyo bila ya kushawishiwa na upande wowote. Kutokana na hali hiyo, nawaasa pande zote kuwa watakaoshiriki uchaguzi huo washiriki kwa amani na wanaosusia wasusie kwa amani. Fanyeni mfanyayo ila mtuachie amani yetu. Amiri Jeshi Mkuu ametangaza kuimarisha amani na utulivu kote nchini. Ni wajibu wetu kujiepusha na yale yatakayovuruga amani yetu.
 
Linapoletwa suala la Zanzibar kujadiliwa watu huwa wanajitoa ufahamu kwa makusudi na kushindwa kujenga hoja. Nakupongeza mleta mada umejenga hoja yako vizuri, ni kweli waliosusia uchaguzi wasusie kwa amani na wataoshiriki uchaguzi washiriki kwa amani. Tunataka kuona ndugu zetu wa Zanzibar kisiwa chao kinaendelea kuwa na amani, ni hayo tu!
 
Lizaboni,
Kabla ya indhari hii umetoa wito wa amani kwa Zombie wanaopiga
watu karibu mwezi wa tatu huu na serikali haijafanya kitu?
 
Sawa mtoa mada hilo la muhimu sana,kurejedha amani kama ikitoweka ni kazi ngumu kwelikweli.
Zanzibar ikichafuka hata bara hatuta kuwa salama.
 
AMANI ni tunda la HAKI. Pasipo haki hapawezi kuwa na amani!
Umenena vema.
CCM kupitia jecha wameipoka "amani" indirect kwa kuipoka "haki" ya wazanzibar ya kuchagua rais wanayemtaka.

Mazombie wakiwa na gari za polisi wanapiga, wanajeruhi, wanateka, wanaua, wanachoma nyumba na mali ila hawa watetezi wa CCM na serikali wako kimya alafu leo kiwavi mmoja anahubiri amani,
CCM rejesheni haki kwa kumtangaza Seif mtakua mmerejesha amani zanzibar tofauti na hapo ccm mtauwa raiya wengi sana na wataendelea kudai haki zao bila kujali idadi kubwa mtakayokua mmeua.
 
Rais kishasema hana mamlaka ya kuingilia ama kufanya chochote kupinga alichokisema bwana mkubwa Jecha Salum Jecha wa serikali ya ZEC ila kwa upande mwingine akiwa Amiri wa majeshi ya Ulinzi na Usalama yeye kasema huko visiwani atahusika ktk mambo yasiyohusu demokrasia yaani atapeleka majeshi kupiga watakaoleta fyoko kuitaka hiyo haki na demokrasia.
 
Lizaboni,
Kabla ya indhari hii umetoa wito wa amani kwa Zombie wanaopiga
watu karibu mwezi wa tatu huu na serikali haijafanya kitu?
Sheikh Wangu tafuta YouTube kipindi cha je tutafika? Cha Channel ten kimerushwa leo kina part one na two host ni Makwaia Wa kuhenga mgeni alikuwa ni balozi Karume utaelewa vizuri kwamba ccm hawawezi kuachia madaraka bila mapinduzi mengine, na ccm Wa Zanzibar ambao ndio wanadhani au wanajiona ndio wenye haki ya kuzaliwa kutawala urafiki wao na ccm Tanganyika ni kwa sababu ya hifadhi ya ulinzi Wa kijeshi tu ndipo kibri yao ilipo. Wao jema kwao kutoka kwa waarabu ni dini ya kiislamu tu. Ukimsikiliza Balozi Karume kwa makini huo ndio msimamo Wa Wahafidhina Wa Zanziber. Bado Nina mashaka kama hata misikitini Hawa jamaa sijui huwa wanamuabudu Mungu yupi, wanawachukia waarabu wakati mtume wao ni mwarabu pia. Mimi nimechoka kabisa.
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Nchi nyingi zimeingia kwenye machafuko baada ya uchaguzi Mkuu wa nchi husika. Hii ni kutokana na hulka ya kibinadamu kuwa anayeshindwa hakubali kushindwa na anayeshinda humkejeli aliyeshindwa. Siasa za nchi si sawa na upinzani wa Simba na Yanga. Siasa ndiyo hutoa mustakabali wa taifa husika. Siasa ikienda fyongo, hakuna kitakachonoga.

Tunapoelekea kwenye Uchaguzi wa Zanzibar ambao umepangwa kufanyika Machi 20, mazingira ya uchaguzi huo si mazuri. CCM wamejipanga kisawasawa kushiriki uchaguzi huo. Chama Kikuu cha upinzani CUF wamejipanga kisawasawa kususia uchaguzi huo. Hapa CUF wamehiari kuwa nje ya siasa za Zanzibar kwa miaka 5 ijayo. Haijajulikana ni aina gani ya siasa watakayoshiriki hasa kutokana na kuwa nje ya serikali na bunge. CCM itakuwa inajitanua katika maeneo yote kwa asilimia 100. Uwakilishi pekee wa CUF ni kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambako naamini ndiko CUF watakakopenyezea mambo yao.

Wito wangu kwa Wazanzibari ni kwamba, ZEC wametangaza tarehe ya Uchaguzi. Hakuna chombo chenye mamlaka ya kutengua maamuzi hayo ya ZEC isipokuwa ZEC wenyewe. Waliotangaza kushiriki naamini kuwa wamefanya hivyo bila ya shinikizo kutoka upande wowote. Na wale waliosusia, naamini kuwa wamefanya hivyo bila ya kushawishiwa na upande wowote. Kutokana na hali hiyo, nawaasa pande zote kuwa watakaoshiriki uchaguzi huo washiriki kwa amani na wanaosusia wasusie kwa amani. Fanyeni mfanyayo ila mtuachie amani yetu. Amiri Jeshi Mkuu ametangaza kuimarisha amani na utulivu kote nchini. Ni wajibu wetu kujiepusha na yale yatakayovuruga amani yetu.
Kwani umesikia nn? Au na wewe unajua kwamba walifanya hujuma? Hakuna amani sehemu ambayo haki haipo. Inabidi tulijue hili kabla hatujajifanya tunapenda amani ya kweli
 
Sheikh Wangu tafuta YouTube kipindi cha je tutafika? Cha Channel ten kimerushwa leo kina part one na two host ni Makwaia Wa kuhenga mgeni alikuwa ni balozi Karume utaelewa vizuri kwamba ccm hawawezi kuachia madaraka bila mapinduzi mengine, na ccm Wa Zanzibar ambao ndio wanadhani au wanajiona ndio wenye haki ya kuzaliwa kutawala urafiki wao na ccm Tanganyika ni kwa sababu ya hifadhi ya ulinzi Wa kijeshi tu ndipo kibri yao ilipo. Wao jema kwao kutoka kwa waarabu ni dini ya kiislamu tu. Ukimsikiliza Balozi Karume kwa makini huo ndio msimamo Wa Wahafidhina Wa Zanziber. Bado Nina mashaka kama hata misikitini Hawa jamaa sijui huwa wanamuabudu Mungu yupi, wanawachukia waarabu wakati mtume wao ni mwarabu pia. Mimi nimechoka kabisa.
Matola,
Nimesikiliza na nimepigwa na bumbuazi.
CCM Zanzibar kushindwa uchaguzi sababu ni masultani kutoka Oman.

Hilo la Uislam halikuwepo tokea mwanzo.

Baada ya mapinduzi mashine za kuchapa Kiarabu ziling'olewa na kutupwa
kwenye taka za mji.

Watu wakatishwa ikawa wanatupa vitabu vyote vya Kiarabu.
Muslim Academy leo panauzwa ulevi.
 
Rais kishasema hana mamlaka ya kuingilia ama kufanya chochote kupinga alichokisema bwana mkubwa Jecha Salum Jecha wa serikali ya ZEC ila kwa upande mwingine akiwa Amiri wa majeshi ya Ulinzi na Usalama yeye kasema huko visiwani atahusika ktk mambo yasiyohusu demokrasia yaani atapeleka majeshi kupiga watakaoleta fyoko kuitaka hiyo haki na demokrasia.
Maramia,
Mbona Mazombie huu kiasi mwezi wa nne wanatembea mabarabarani na silaha
na kupiga watu bado hajapeleka majeshi kuzuia ''fyoko'' hiyo?
 
Linapoletwa suala la Zanzibar kujadiliwa watu huwa wanajitoa ufahamu kwa makusudi na kushindwa kujenga hoja. Nakupongeza mleta mada umejenga hoja yako vizuri, ni kweli waliosusia uchaguzi wasusie kwa amani na wataoshiriki uchaguzi washiriki kwa amani. Tunataka kuona ndugu zetu wa Zanzibar kisiwa chao kinaendelea kuwa na amani, ni hayo tu!
Kirikou,
Huo hauwezi kuwa uchaguzi bila ya kushiriki CUF.
Zanzibar ni ''two party state.''

Ikiwa moja haishiriki katika uchaguzi hauwezekani.
Hiki cha kwetu kitakuwa kioja cha karne.
 
Back
Top Bottom