Uchaguzi wa simba, kinachoendelea

Uchaguzi wa simba, kinachoendelea

Zatara

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2012
Posts
716
Reaction score
512
Wadau wa michezo, baada ya kukuru-kakara za kila aina za kugombania madaraka kwa njia zote. Hatimaye leo J2 uchaguzi wa Simba SC unafanyika.

Twaomba mtujuze kinachoendelea
 
Kuondoa mizengwe kila kura tutaandika Wambura, hata kama wamemuondoa.
 
Naskia wambura kazuiwa kuingia

...ni kweli...!
MICHAEL WAMBURA AZUILIWA: Aliyekuwa mgombea urais katika Klabu ya Simba, Michael Wambura amezuiliwa kuingia katika ukumbi ambao uchaguzi huo unafanyika leo.
 
Wanachama watatu wa Klabu ya Simba wamekamatwa wakifanya kampeni wakati mchakato wa upigaji kura ukiendelea, wameondolewa ukumbini.
 
Watu wengi walikuwa wakimpigia wambura hata kama agombei, sijui hili limekaaje kisheria
 
Tunaomba matokeo ya uchaguzi wanamsimbazi,humu kwenye uzi kuna akina ndala ambao hawatutakii mema
 
sisi azam tuliyaona mapema,
ndio maana huwa hatuna uchaguzi. c ni mpira na makombe 2
 
yeye mwenyewe kapija hivyo ndio maana....

Matokeo ya awali ambayo BIN ZUBEIRY
imeyapata kutoka chumba cha kuhesabia kura
ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi,
Oysterbay, Dar es Salaam, Evans Elieza Aveva
ameshinda Urais kwa kupata kura 1452 kati
ya 1845 zillizopigwa, mpinzani wake Andrew
Tupa akipata kura 387 wakati kura sita
zimeharibika. Hata hivyo, matokeo rasmi ya
uchaguzi huo yatatangazwa na Kamati ya
Uchaguzi ya klabu hiyo chini ya Mwenyekiti
Dk Damas Ndumbaro baadaye

SOURCE: Bin Zubeiry
 
Back
Top Bottom