Uchaguzi wa NEC Hanang': Sumaye abwagwa na mama Nagu

Fisadi Mtoto

JF-Expert Member
Jan 7, 2008
639
79
Matokeo ndio yamemaliza kutolewa Mama Nagu kapata kura mia sita na alobaini na mh waziri mkuu mstaafu na mgombea urais mtarajiwa kapata kura mia nne ishirini.

TAKUKURU yawafuata Sumaye, Nagu Hanang

na Mwandishi wetu, Katesh
Tanzania Daima

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), imeingia kwa siri wilayani Hanang' kukabiliana na vitendo vya rushwa katika uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa kutafuta wajumbe wa halmashauri kuu yake ya Taifa (NEC), wilayani humo, imefahamika.

Hatua hiyo ya TAKUKURU imekuja baada ya kuwepo kwa taarifa za kuwepo kwa vitendo vya rushwa katika kampeni, vinavyodaiwa kufanywa na mmoja wa wanaowania nafasi ya mjumbe wa NEC kutoka wilayani Hanang'
CCM imewapitisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Dkt. Mary Nagu na Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye kuwania nafasi ya mjumbe wa NEC katika wilaya hiyo.

Kumekua na madai mazito kuhusiana na ugawaji fedha unaofanywa na mgombea huyo na kwamba anatumia mbinu ya kugawa fedha hizo kwa njia ya mtandao.

Akizungumzia madai hayo ya rushwa, Kaimu Kamanda wa TAKUKURU wilaya ya Hanang' Samson Sanga alikataa kuzungumzia kuhusu taasisi yake kufanya kazi zake kwa siri kwa maelezo kwamba kwa sasa ofisi yake haiwezi kuzungumzia suala hilo.

Wiki hii, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Dk. Edward Hoseah alinukuliwa akisema taasisi yake inafuatilia kwa karibu uchaguzi huo ndani ya CCM ili kubaini watu wanaotumia rushwa.

Dk. Hoseah alitoa kauli hiyo akijibu hoja mbalimbali za washiriki wa kongamano la kujadili utekelezaji wa awamu ya pili ya mpango wa kupambana na rushwa nchini na mapendekezo yanayopaswa kuzingatiwa katika utekelezaji wa mpango wa awamu ya tatu (2012 – 2016).

"Tatizo ni kwamba wagombea wengi wa nafasi ya uongozi wamekuwa wakijiandaa kutoa rushwa wakati wa uchaguzi na kwa bahati mbaya hata wananchi ambao ni wapiga kura ni kama wanajiandaa kupokea rushwa kila uchaguzi unapokaribia, hili ni tatizo kubwa," alisema Dk Hosseah na kuongeza:

"Tunaendelea kufuatilia, lakini ni kazi kubwa kwelikweli kwa mfano, sasa tunafuatilia uchaguzi wa ndani wa CCM na tunafanya hivi ili kuhakikisha kwamba hatupati viongozi wanaotokana na rushwa, maana tukiwa na viongozi wa aina hii hatuwezi kushinda vita hivi."

Katika kikao kilichofanyika Jumapili ya Septemba 2, mwaka huu na kuongozwa na katibu wa CCM Wilaya ya Hanang' Allan Kingazi, wajumbe wa kikao hicho walipitisha jina la Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye na Leonsi Marmo huku Dkt Nagu akitoswa kufuatia kudaiwa kuwa na majukumu mengi ya kikazi ikiwemo ubunge na uwaziri.

Wakizungumzia maamuzi ya vikao vya juu vilivyopitisha jina la Dk. Nagu kuwa mmoja wa wagombea wa nafasi hiyo, baadhi ya wajumbe wa kamati ya siasa ya Wilaya ya Hanang' walioomba kutotajwa majina yao gazetini walisema kamati hiyo haikuwatendea haki.

"Kamati kuu haikutenda haki kabisa, kwa kuwa imepuuza maamuzi yetu, haiwezekani sisi tufanye maamuzi tena kwa kufuata kanuni za CCM ilizotunga yenyewe halafu maamuzi yetu yabadilishwe na kuonekana sio sahihi, huku ndio kunakopeleka pabaya hiki chama,"alisema mmoja wa wajumbe waliodaiwa kupigia kura jina la Dkt.Nagu kutopitishwa katika kikao kilichofanyika Septemba 2 mwaka huu.
 
Hata kama Mzee Sumaye angeshinda kwa hawa waliopitishwa kugombea then kuwa ndiyo wapiga kura kumchagua mgombea wa CCM 2015 HAKUNA WA KUMSHINDA LOWASSA maana JK kamtengenezea njia kumpa wajumbe waliopo kwenye kambi yake!

Kumpinga Lowassa ndani ya CCM 2015 ni kujimalizia resources zako bure bila any return onto your favor!Kama Dr Hunter-Kyela kachukua Uenyekiti wa Wilaya kiurahisi kwa hela chafu na hata Mzee Wakasuvi nae jina lake limerudishwa Tabora nani basi wa kumshinda Lowassa?
 
DAKITARI(sijui wa kufuga samaki) NAGU KAMBWAGA SUMAYE, WOTE WAPENDA MASLAHI BINAFSI TU.
 
Nagu inasemekana amegawa shs. 500000/= kwa kila mjumbe. Je, hiyo ni kweli fisadi mtoto?
 
M4C ndio kiboko yao wote hao, wapitishane, waumizane watajijua ila 2015 hawataamini kitakachowapata. Tumeshachoka watu walewale na mambo yao yasiyobadilika, tamaa za maslahi binafsi haziwaishi huku hali za wananchi zinazidi kuwa duni.
 
Ahahahaha Mkirua unanikumbusha enzi zao zilee pale Morogoro canvas ahahaha!

Sikutegemea kama hawa wawili ipo siku watakuja kugombea nafasi moja bila mmoja kumuachia mwenzake!

2007-Lowassa aliongoza kati ya wagombea wote (maana zamani walikuwa kwenye kapu moja), 2012 anagombana na watu watatu. salma na Liz wamepita bila kupingwa, 2017 wataondolewa kama Nimrodi au Filikunjombe kwamba hawana sifa. Hii ndio CCM.Wanaogopana wakiwa na madaraka.Huyu maza kwanza ni mayala tu hana lolote.Wakati akiwa PM wake alikuwa anamsafishia hata viatu kwenye basi angeweza hata kumuachia siti!!
Kuichukia CCM ni kuuchukia UFISADI.Piga vita CCM kwa maendeleo ya Taifa
 
Kila mtu ametoa takrima kwa kweli lakini sio rushwa


enzi hizo ukihudumiwa vizuri ukatoa zawadi kwa mtumishi wa serikali ambae amekuhudumia vizuri unaambiwa hiyo ni rushwa kwani aliekuhudumia ametelekeza majukumu yake ambayo amepaswa kuyafanya hivyo utamfanya yule ambae hana uwezo wa kutoa zawadi kunyanyapaliwa siku ikitokea umekuja mara ya pili maana hutapanga foleni. Miaka hii tunaambiwa hawajatoa rushwa bali wametoa TAKRIMA (sie ni mabingwa wa kupoza maneno lakini maana inabaki ileile ya zeruzeru anaitwa mlemavu wa ngozi au albino na kiwete anaitwa mlemavu wa miguu wakati maana na ile ile). Fisadi Mtoto mie napendekeza tumpe mshindi wa tatu kama wote wametoa takrima kabla ya uchaguzi
 
Last edited by a moderator:
Kuna waliokamatwa au tufungue kesi

Kuna uchaguzi ambao watu walikamatwa na rushwa waziwazi kama ule wa Arumeru na bado wakapitishwa wakabwagwa na CDM, kuna yule Mwakalebela alikamatwa na rushwa na sasa naona mwaka huu kagombea tena na hakuna anayezungumzia Rushwa. Dk. Slaa kasema matokeo ya chaguzi wa CCM mwaka huu wanajimaliza, maana watu waliosema ni mafisadi wanatakiwa wajivue gamba, wasipojivua watavuliwa... Imekua ni ngonjera ya Nape na wenzake kwa miaka sasa... Nakumbuka toka NEC ya Butiama CCM imekua na kigugumizi, leo haya Lowassa na Chenge wamerudi tena kilingeni na ndio wenye kuamua nani aingie CCM kama huyu mama Nagu, wamemsaidia kwa hali na mali na ameshinda... Mgeja wa Shinyanga alikua akipambana na Lembeli, wakakatwa, mara Lowassa kaingilia kati, JK akatoka na Nape nje sijui kuzuga ama waliitwa kiana ili Msekwa amrudishe Mgeja... Leo tutake tusitake CCM inajichimbia kaburi... Aliwahi kusema Msomaji Raia katika Raia Mwema kwamba "mbele giza nyuma kaburi"... Na tokea 2006 kuna mtu alisema, "CCM kila kukicha wanateleza, wakitaka kutatua tatizo ni kama wanazima moto kwa petroli".... Tuombe Mungu nchi isiangukie kwa FISADI maana nguvu zao ni kubwa mno.
 
Kuna uchaguzi ambao watu walikamatwa na rushwa waziwazi kama ule wa Arumeru na bado wakapitishwa wakabwagwa na CDM, kuna yule Mwakalebela alikamatwa na rushwa na sasa naona mwaka huu kagombea tena na hakuna anayezungumzia Rushwa. Dk. Slaa kasema matokeo ya chaguzi wa CCM mwaka huu wanajimaliza, maana watu waliosema ni mafisadi wanatakiwa wajivue gamba, wasipojivua watavuliwa... Imekua ni ngonjera ya Nape na wenzake kwa miaka sasa... Nakumbuka toka NEC ya Butiama CCM imekua na kigugumizi, leo haya Lowassa na Chenge wamerudi tena kilingeni na ndio wenye kuamua nani aingie CCM kama huyu mama Nagu, wamemsaidia kwa hali na mali na ameshinda... Mgeja wa Shinyanga alikua akipambana na Lembeli, wakakatwa, mara Lowassa kaingilia kati, JK akatoka na Nape nje sijui kuzuga ama waliitwa kiana ili Msekwa amrudishe Mgeja... Leo tutake tusitake CCM inajichimbia kaburi... Aliwahi kusema Msomaji Raia katika Raia Mwema kwamba "mbele giza nyuma kaburi"... Na tokea 2006 kuna mtu alisema, "CCM kila kukicha wanateleza, wakitaka kutatua tatizo ni kama wanazima moto kwa petroli".... Tuombe Mungu nchi isiangukie kwa FISADI maana nguvu zao ni kubwa mno.

Yaani hata wanaochukua ela walitakiwa wachukue alafu wanatumia akili zao kwa kumchagua wanemtaka, tatizo kubwa hapa mtu anakuwa upande wako akiamini kabisa once utakapoingia madarakani atakutumia kama tool ya kufanya advocacy ili mambo yake yaende vizuri pindi anapokuwa na deal inayohitaji mihuri na sahihi za viongozi wa kiserikali. Hawa jamaa inabidi wafanye maamuzi magumu
 
Back
Top Bottom