Nimebahatika kumsikia diwani wa kata ya Kibakwe akilizungumzia suala hili.
Ikumbukwe kuwa Halmashauri ya Mpwapwa ni kongwe lakini watendaji wake ni sifuri. Mleta mada hebu sema hao wasomi waliopita walifanya nini zaidi, zaidi ya kula pesa ya walipakodi kwa kujifanya wajanjawajanja?? .
Katika hotuba yake ya ufunguzi, M/Kiti mpya ndg Nghwenzi alisema kwa muda mrefu halmashauri imekuwa pango la wanyang'anyi lakini kuanzia sasa amesema halmashauri itakuwa Lulu na ameahidi utendaji uliotukuka na wa haki kwa sababu hana chochote cha kujivuna kama wengine wanaojivunia elimu zao kubwa.
Na kwa kuanza kamati za halmashauri wamepitishwa watu wa kazi tu bila kuangalia elimu zao na hicho kinawauma sana wanaojifanya wamesoma. Diwani wa Kibakwe anasema safari hii wamepewa nguvu kubwa sana na formula ya dkt Magufuli kwamba kwa mfano pesa za Elimu bure kwenda kwenye akaunti za shule huku Mkurugenzi akiarifiwa kwa copy tu, hili litakomesha ufisadi wa Wakurugenzi wa wilaya.
Mimi ni
Malezo kuwaletea habari hii