Uchaguzi wa Meya Halmashauri ya Mpwapwa- kituko chatokea

niliku huko madiwani wa kike wanaweza kuwa wamekeketwaaaa
 
Yes, hata mm ndo maeneo ya home..kaz inatakiwa tena co ya kitoto...
 
Huenda ulikuwa na ujumbe/taarifa nzuri tu,
Ila kwa uandishi wako huu uliojaa hisia, you seems to make hollering!!
 
Mwl mstaafu level ya headmaster ndiyo kitu gani?
 
Inaniuma sana Mpwapwa is my home place. Hakuna maendeleo ni wasomi ndo hivyo tumebaki mjini na mambo ndo yanaharibika.
 
Sasa si tunaambiwa siku zote kuwa kama elimu ni gharama ama taabu jaribu na ujinga. Kwani huko ccm si ndio nilikoona clips za madiwani wao wengine wakishindwa kusoma hata viapo vyao? Wanawake kwa wanaume ila ukiangalia walivyovalia utadhani ni graduates.

Hahahaaaa,Wakina kibajaji @co.
 
NAIBU Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Utumishi na Utawala Bora, Selemani Jaffo amewatangazia kihama wakurugenzi wote nchini watakaoshindwa kuwasimamia wakuu wa idara katika Halmashauri zao.

Jaffo amesema wakurugenzi ambao watashindwa kuwasimamia wakuu wa idara na kujikuta wanafanya kazi zao bila ufanisi waandike barua ya kuomba kuondoka kazini wenyewe.
Naibu huyo alitoa kauli hiyo jana alipofanya ziara yake ya kikazi ya kwanza ya kushtukiza katika wilaya ya Bahi iliyopo mkoani Dodoma.

Mbali na hilo ametoa muda wa siku 27 kwa halmashauri zote nchini kuhakikisha zinatumia mfumo wa kielektroniki kwa ajili ya kukusanya mapato katika halmashauri husika.

Hiyo paragraph ya mwisho inalingana na viongozi wa halmashauri ya Mpwapwa?
 
ni makosa tu ya kawaida hayoo.. Sas mbona wee mwenyewe umekosea au huoni? karamu badala ya kalamu au wee mnyarwanda? Nadahani hata wew haujamaliza shule achilia mbali kukosoa watu
 
Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa leo wamefanya uchaguzi wa mwenyekiti wao kwa upande wa chama cha mapinduzi (CCM),wagombea walikuwa ni madiwani watatu.

1.Mh Dastan Malogo ambaye ni Medical Doctor LT.
2. Mh. Honorati Pima graduate from UDSM na ni mwalimu wa secondary mstaafu level ya Headmaster
3. Mh. Ng`wenzi diwani mstaafu ambaye alisusa udiwani na kufuata mwanamke ruaha mbuyuni Iringa kwenye uchaguzi wa mwaka 2010, alihudhulia kikao kimoja tu mwanamke akamnogea akaacha na udiwani, ila ana vicent kidogo na ving`ombe kama arobaini hivi ni darasa la nne

Uchaguzi huu alisimamia mkurugenzi kama kawaida ila thinktank wa wadiwani wa majimbo mawili alikuwa Mh. Simbachawene mbunge wa Kibakwe.

Matokeo:

1.Mh. Ngw`Enzi na utoro wake amepata kura 30
2. Mh. Dr Malogo kura 7 na U-doctor wake
3. Mh. Pima kura 2 na degree yake

Kesho ndiyo uchaguzi wa vyama vyote ambapo majimbo yote mawili hakuna diwani wa upinzani, ina maana mwenyekiti wa halmashauri ya Mpwapwa atakuwa ni darasa la nne

Kwa makamo nako ni vituko amachaguliwa Mh. George Fuime amepita bila kupingwa, ni mbena wa kijiji cha Wino, kata ya madaba Songea alitoroka shule kwao siku nyingi na aliacha shule akiwa darasa la tatu.

Kituko chenyewe:
Hiyo meza kuu ya halmashauri wote hawawezi kutumia karamu na notebook, wachilia mbali Laptop.

Yote yakifanyika Mbunge na waziri Simbachawene yupo. Mbunge wa Mpwapwa Mh. Lubeleje yeye alijitetea asihusishwe kwani sasa hivi macho yake hayaoni.

Hivi kwa CCM hicho ni kituko au ndio hali halisi?!!
 
Ndio maana niliona aibu hata kujitangaza kuwa niliwahi kufanyakazi dodoma
 
ni makosa tu ya kawaida hayoo.. Sas mbona wee mwenyewe umekosea au huoni? karamu badala ya kalamu au wee mnyarwanda? Nadahani hata wew haujamaliza shule achilia mbali kukosoa watu

Hata wewe umekosea vile vile NADAHANI ndiyo ulimananisha nini? Nafikiri wewe umesoma Enzi za Kikwete ambapo magoli yalipanuliwa ili na watu kama nyinyi mfaulu.
 
Huyo std 7 ndiye wameona anastahili kuwaongoza,japo ni ajabu kweli kwa karne hii. Cha msingi ni kuangalia upya vigezo vya mtu kuchaguliwa kuwa diwani au mbunge.

Haiwezekana eti mtu wa darasa la 7 akasimamie, akajadili, akachambue na kupitisha miswada na bajeti iliyoandaliwa kitaalam na watu ambao ni graduate au hata PhD holders.

Elimu ya mwisho ya mtu kuajiriwa na serikali na form four, ila elimu ya kuwa mbunge/diwani ni 'kujua kusoma na kuandika' kiswahili au kiingereza. We are not serious.

Ndiyo maana katika wabunge zaidi ya 250 wa ccm, rais ameshindwa kupata watu wanne wanaofaa kuwa mawaziri!
 
NAIBU Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Utumishi na Utawala Bora, Selemani Jaffo amewatangazia kihama wakurugenzi wote nchini watakaoshindwa kuwasimamia wakuu wa idara katika Halmashauri zao.

Jaffo amesema wakurugenzi ambao watashindwa kuwasimamia wakuu wa idara na kujikuta wanafanya kazi zao bila ufanisi waandike barua ya kuomba kuondoka kazini wenyewe.
Naibu huyo alitoa kauli hiyo jana alipofanya ziara yake ya kikazi ya kwanza ya kushtukiza katika wilaya ya Bahi iliyopo mkoani Dodoma.

Mbali na hilo ametoa muda wa siku 27 kwa halmashauri zote nchini kuhakikisha zinatumia mfumo wa kielektroniki kwa ajili ya kukusanya mapato katika halmashauri husika.

Hiyo paragraph ya mwisho inalingana na viongozi wa halmashauri ya Mpwapwa?

Hee! mama yangu weee, si mleta mada kasema hawajui kutumia hata notebook? Basi mkurugenzi ana kazi sana, kila kitu itabidi afanye yeye
 
Hata kama hakusoma zaidi lakini kama utendaji wake ni mzuri anafaa. Kwani ni wangapi Maprofesa lakini wana matatizo katika utendaji?????

Kama wananchi wamemkubali hadi kumpa udiwani hivyo ina maana pia anaweza kuwatumikia.
 
Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa leo wamefanya uchaguzi wa mwenyekiti wao kwa upande wa chama cha mapinduzi (CCM),wagombea walikuwa ni madiwani watatu.

1.Mh Dastan Malogo ambaye ni Medical Doctor LT.
2. Mh. Honorati Pima graduate from UDSM na ni mwalimu wa secondary mstaafu level ya Headmaster
3. Mh. Ng`wenzi diwani mstaafu ambaye alisusa udiwani na kufuata mwanamke ruaha mbuyuni Iringa kwenye uchaguzi wa mwaka 2010, alihudhulia kikao kimoja tu mwanamke akamnogea akaacha na udiwani, ila ana vicent kidogo na ving`ombe kama arobaini hivi ni darasa la nne

Uchaguzi huu alisimamia mkurugenzi kama kawaida ila thinktank wa wadiwani wa majimbo mawili alikuwa Mh. Simbachawene mbunge wa Kibakwe.

Matokeo:

1.Mh. Ngw`Enzi na utoro wake amepata kura 30
2. Mh. Dr Malogo kura 7 na U-doctor wake
3. Mh. Pima kura 2 na degree yake

Kesho ndiyo uchaguzi wa vyama vyote ambapo majimbo yote mawili hakuna diwani wa upinzani, ina maana mwenyekiti wa halmashauri ya Mpwapwa atakuwa ni darasa la nne

Kwa makamo nako ni vituko amachaguliwa Mh. George Fuime amepita bila kupingwa, ni mbena wa kijiji cha Wino, kata ya madaba Songea alitoroka shule kwao siku nyingi na aliacha shule akiwa darasa la tatu.

Kituko chenyewe:
Hiyo meza kuu ya halmashauri wote hawawezi kutumia kalamu na notebook, wachilia mbali Laptop.

Yote yakifanyika Mbunge na waziri Simbachawene yupo. Mbunge wa Mpwapwa Mh. Lubeleje yeye alijitetea asihusishwe kwani sasa hivi macho yake hayaoni.

Kwi,kwi, kwi kwi kwi, kwi, kwi, kwi kwi,kwi, kwi, kwi, kwi,kwi,kwi, kwi kwi, kwi, kwi aaaaaaaaaa.
 
Yule aliyekuwa mwenyekiti pale bwana Bulamulete kaishia wapi?
 
Back
Top Bottom