Uchaguzi wa Meya Halmashauri ya Mpwapwa- kituko chatokea

Uchaguzi wa Meya Halmashauri ya Mpwapwa- kituko chatokea

laurent Msembeyu

Senior Member
Joined
Oct 5, 2015
Posts
121
Reaction score
101
Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa leo wamefanya uchaguzi wa mwenyekiti wao kwa upande wa chama cha mapinduzi (CCM),wagombea walikuwa ni madiwani watatu.

1.Mh Dastan Malogo ambaye ni Medical Doctor LT.
2. Mh. Honorati Pima graduate from UDSM na ni mwalimu wa secondary mstaafu level ya Headmaster
3. Mh. Ng`wenzi diwani mstaafu ambaye alisusa udiwani na kufuata mwanamke ruaha mbuyuni Iringa kwenye uchaguzi wa mwaka 2010, alihudhulia kikao kimoja tu mwanamke akamnogea akaacha na udiwani, ila ana vicent kidogo na ving`ombe kama arobaini hivi ni darasa la nne

Uchaguzi huu alisimamia mkurugenzi kama kawaida ila thinktank wa wadiwani wa majimbo mawili alikuwa Mh. Simbachawene mbunge wa Kibakwe.

Matokeo:

1.Mh. Ngw`Enzi na utoro wake amepata kura 30
2. Mh. Dr Malogo kura 7 na U-doctor wake
3. Mh. Pima kura 2 na degree yake

Kesho ndiyo uchaguzi wa vyama vyote ambapo majimbo yote mawili hakuna diwani wa upinzani, ina maana mwenyekiti wa halmashauri ya Mpwapwa atakuwa ni darasa la nne

Kwa makamo nako ni vituko amachaguliwa Mh. George Fuime amepita bila kupingwa, ni mbena wa kijiji cha Wino, kata ya madaba Songea alitoroka shule kwao siku nyingi na aliacha shule akiwa darasa la tatu.

Kituko chenyewe:
Hiyo meza kuu ya halmashauri wote hawawezi kutumia kalamu na notebook, wachilia mbali Laptop.

Yote yakifanyika Mbunge na waziri Simbachawene yupo. Mbunge wa Mpwapwa Mh. Lubeleje yeye alijitetea asihusishwe kwani sasa hivi macho yake hayaoni.
 
Umeandika kishabiki sana bro.Pima ni Mwalimu wangu ni mtu mzuri na muungwana.
 
Ndo level za akili zao mkuu... Ccm hawaangalii kipaji na uzoefu wao wanaamin katka visenti uchwala tuuu... Mbna wana wabunge wengi std 7 tu... Ndo ccm hiyo mkuu
 
Nikikuita mbea,mnafiki na mzandiki nitakua nakosea?
Katika ulimwengu huu wa digitali viongozi hao ni wa kukaa meza kuu? ukiniita ulivyosema basi wewe akili zako ziko kwenye magoti,na kichwani mwako una kamasi siyo ubongo
 
KAMA MPWAPWA IPO DODOMA hakuna shida maana bado hawajaamka toka usingizi wa CCM

"ingekuwa mpwapwa mkoa kama MWANZA, KILIMANJARO, ARUSHA ingekuwa shida maana wanahitaji maendeleo
 
Huo ukanda maji safi ni sawa na dhahabu. But wanasema ukanda huo ndio unaoongoza kwa udumavu wa akili TZ, tatizo kubwa ni lishe duni.
 
Huyu broo kaandika usahihi mtupu, mpwapwa ni nyumbani ila daaah ! Hayo yanawezeka fitina tupu Ngw'enzi asha wapigana Ngw'enzi wasomi na elimu zaoo
 
Huyo ndiye amepata kura mbili,yakwake na mke wake.

Sasa si tunaambiwa siku zote kuwa kama elimu ni gharama ama taabu jaribu na ujinga. Kwani huko ccm si ndio nilikoona clips za madiwani wao wengine wakishindwa kusoma hata viapo vyao? Wanawake kwa wanaume ila ukiangalia walivyovalia utadhani ni graduates.
 
Kweli hawa wagogo wanahitaji maombi du,udumavu wa mwili na akili
 
Ndio hivyo tena ccm imeamua kuwa chama cha ubeberu.
 
Back
Top Bottom