Uchaguzi wa ghana tumejifunza nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi wa ghana tumejifunza nini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mpaka Kieleweke, Jan 22, 2009.

 1. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #1
  Jan 22, 2009
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Uchaguzi Mkuu wa Ghana ulifanyika mwaka huu na kuna mengi yaliyojitokeza kutokana na uchaguzi huo, ila ningependa sisi kama watanzania na zaidi kama wana wa Afrika tuweze kujiuliza uchaguzi huu umetupa funzo gani?

  Kwanza , ni kuwa chama cha NDC ambacho kilikuwa chama tawala mpaka mwaka 2000 kiliondolewa madarakani na chama kilichokuwa cha Upinzani cha NPP.

  Mwaka 2008 chama tawala cha NPP kiliondolewa madarakani na chama cha upinzani cha NDC baada ya John Atter Mills kumshinda Nana Akufo Addo wa NPP, japo kwa ushindi mwembamba sana ila ni ushindi uliopatikana kwenye raundi ya pili.

  Je? Kuna umuhimu wa kiongozi wa Tanzania kushinda kwa 50 plus?

  je? kama Ghana wameweza nini kinafanya nchi nyingine za Kiafrika kushindwa?

  Rais wa Ghana bado hajaapishwa kwani wao wana utaratibu wa kumpa kiongozi muda wa kupewa secrets of the state, kabla hajakabidhiwa dola na ukuu wa majeshi, pia muda huo huutumia kupanga timu yake kikamilifu.

  MATOKEO YALIKUWA KAMA IFUATAVYO.

  NPP - 4,480,446 - 49.77%

  NDC - 4,521,032 - 50.23%

  Turnout was 72%.

  Kwa kuangalia matokeo hayo inakuwaje wenzetu Zanzibar, Kenya, Zimbabwe na Zambia kuapishana usiku? kama kweli huwa wanashindaga?

  Mjadala mwema , ila inawezekana kuwa huyu Mills ni Rawlings kaingia kwa mlango wa uwani ?
   
Loading...