Uchaguzi wa Arumeru Kusimamishwa Mahakamani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi wa Arumeru Kusimamishwa Mahakamani?

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by ibange, Feb 11, 2012.

 1. i

  ibange JF-Expert Member

  #1
  Feb 11, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nipo Arusha nilikuwa napitapita Arumeru kujua hali ya hewa huko. Vijana wengi wanalalamika kuwa walikuwa hawajajiandikisha na wengine walipoteza vitambulisho na wengine wamerudi kutoka mererani na maeneo mengine walipokuwa wamejiandikisha, wengine walikuwa hawajafikisha miaka 18 uchaguzi uliopita. Wengi wao ni wafuasi wa chadema.

  Kijana mmoja alini impress ana argue kwamba ni haki yake ya kikatiba kupiga kura na wakati wa uchaguzi wa mwaka juzi hakuwa amefikisha umri. Pia anasema kulikuwa hakuna sababu ya daftari la kudumu maana ilikuwa kazi yake ni kurahisisha mambo. Wameniahidi wanatafuta mwanasheria though hawana hela ili wafungue kesi ya kikatiba Mahakama Kuu na waombe kusimamisha uchaguzi.

  Nafikiri hawa vijana pamoja na kwamba wanaonekana hawana shule ya maana wana hoja na inaonyesha ni vipi watanzania wameanza kujua haki zao
   
 2. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #2
  Feb 11, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,253
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  kwahiyo ina maana mtu mmoja akiwa hana kitambulisho cha kupigia kura anaweza kwenda mahakamani kuishtaki tume!? Na una amini kabisa kwamba hao watu watashinda!?
   
 3. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #3
  Feb 11, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwa mahakama za ******* haitawezekana
   
 4. i

  ibange JF-Expert Member

  #4
  Feb 11, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Labda wanasheria watuambie ila nadhani hata haki ya mtu mmoja mahakama itailinda. Lakini najiuliza, ni kwanini tume ya uchaguzi inadhulumu haki ya watu kupiga kura? Tangia 2010 mambo mengi yametokea, kwanini wasitoe fursa ya watu kurekebisha daftari la kudumu?
   
 5. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #5
  Feb 11, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  kama si hivyo hebu sema njia mbadala!kwa hiyo unafurahia huyo mtu mmoja kukosa haki yake ya kupiga kura?
   
 6. amkawewe

  amkawewe JF-Expert Member

  #6
  Feb 11, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 2,029
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kama tunafuata utawala wa sheria then ni haki yako kwenda mahakamani kudai. Wenye mapenzi mema kwa nchi hii watawasaidia
   
 7. escober

  escober JF-Expert Member

  #7
  Feb 11, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 391
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  ibange= bange
  same thinking
   
 8. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #8
  Feb 11, 2012
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  p*o*r*o*j*o.....
   
 9. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #9
  Feb 11, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mtikila alishawahi kufungua kesi ya aina hiyo, na akashindwa
   
 10. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #10
  Feb 11, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,253
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  kwa hiyo unamaanisha kwamba kila mwaka daftari la kudumu liwe linafanyiwa marekebisho kwa sababu kila mwaka watu wanafikisha miaka 18, Lakini naona inapokaribia mwaka wa general election huwa wana update ili kwamba waliofikisha miaka 18 waweze kupiga kura.
   
 11. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #11
  Feb 11, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,765
  Likes Received: 6,090
  Trophy Points: 280
  Mkuu nakubaliana na wewe. Hayo ya watu kupoteza vitambulisho yanaweza kabisa kuwa hayana nguvu sana za kisheria. Lakini kwa wale ambao 2010 walikuwa under 18 na siku ya uchaguzi watakuwa over 17 kuna hoja hapa tena zenye nguvu kisheria; pamoja na mambo mengine ikihusisha HAKI YA URAIA. Ni suala la kuweka wataalamu wazuri wa kujenga hoja zenye mantiki kuweza kuishawishi mahakama.

  Ni bahati mbaya sana Tume "Mpya" ya Uchaguzi imeanza na mguu mbaya; ingeweza kabisa kurudisha heshima yake kwa kiasi fulani angalau kwa kuhakikisha kasoro zote katika uchaguzi huu zimeondolewa. Kwa lugha nyingine, wangehakikisha uchaguzi wa Arumeru Mashariki ungekuwa wa mfano lakini ndio hivyo tena ukishakunywa maji ya bendera sijui akili zinakuwaje?

  Kazi kwako Mh. Jaji Damian Lubuva na timu yako.
   
 12. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #12
  Feb 11, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,253
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  hapana sio kwamba nafurahia huyo mtu kutopiga kura, la hasha. Ila nadhani ile njia ya kufanya marekesho ya kudumu ya daftari la wapiga kura ikikaribia general election ndio nzuri zaidi ili kupunguza gharama, kama inawezekana basi wanaweza fanya kila baada ya mwaka lakini hiyo inatofauti na utoaji leseni ya udereva ambapo kila siku inawezekana kwasababu watu wanalipia, lakini hii nyingine inaweza ikawa ngumu kwa sababu vitambulisho vinatolewa bure!
   
 13. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #13
  Feb 11, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Escoba = pablo escoba bavilio. colombian drag dealer.
   
 14. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #14
  Feb 11, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,765
  Likes Received: 6,090
  Trophy Points: 280
  Oh yes! Sio kila mwaka bali kila SEKUNDE linatakiwa kuwa updated kuingiza wale waliofikisha umri wa kupiga kura. Ni haki yao ya msingi kuwemo kwenye hilo daftari. Vivyo hivyo wale waliotangulia mbele ya haki ni budi kuondolewa humo mara moja kwani pia ni haki yao kutokuwemo humo.

  Kutokana na uduni wa miundombinu yetu ndio maana mambo mengi ya msingi yanasubiri hadi matukio muhimu kama uchaguzi mkuu ndipo watendaji wanafanya kazi walizopaswa kuzifanya kila wakati na hivyo kuleta mitafaruku isiyo na lazima katika jamii.

  Hivyo basi, ingekuwa busara sana kuboresha daftari la A/Mashariki kipindi hiki kutokana na tukio hilo muhimu. Lakini pia usishangae, "uduni wa miundombinu" na "gharama" vikatumiwa kwa faida za kisiasa. Hii ni Afrika Mkuu.
   
 15. KXY

  KXY JF-Expert Member

  #15
  Feb 11, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 876
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 60
  Jibu zuri hili hapa   
 16. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #16
  Feb 11, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Jamani hii Tume ya Uchaguzi si ya Kudumu? Je baada ya Uchaguzi huwa wanafanya nini kama si moja ya kazi wanazopaswa kuendelea nazo ni pamoja na kuboresha daftari la kudumu la Wapiga kura! Au nao huwa wanakwenda likizo mpaka General Election nyingine au utakapotokea Uchaguzi mdogo ndo waende kusimamia! Basi hii Tume haijui wajibu wake. Kila mwezi kuna Watanzania Wanaotimiza umri wa Miaka 18 kwanini wasiwe wanaongezwa kwenye daftari kila mwezi?
   
 17. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #17
  Feb 11, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,798
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  Sio swala la mtu mmoja au elfu kumi kinachotakiwa kabla ya uchaguzi wowote inatakiwa ku review daftari la kupiga kura kwa sababu haki ya kuchagua na kuchaguliwa ilyotajwa kwenye katiba yetu haisemi idadi ya watu ila inatoa haki hiyo kwa kila mtu awe mmoja wawe elfu sasa bila kureview daftari utapataje takwimu za wapiga kura waliiongezeka???
   
 18. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #18
  Feb 11, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,765
  Likes Received: 6,090
  Trophy Points: 280
  Mkuu naomba nikusahihishe kidogo hapo kwenye red! Sio kila mwezi bali kila sekunde au hata pungufu ya hapo kuna makumi kama sio mamia ya watanzania wanaingia kwenye umri mpya! Kwa mfano, tangu ulipo-post hadi nilipokujibu kuna makumi kadhaa ya watu wamevuka kuingia 18.

  Nawashauri hawa watu wa Tume wawasiliane na wataalamu wetu pale Mlimani (UDSM) Kitengo cha Demokrafia (Demographic Unit) angalau wapate msasa juu ya immigration, emigration, etc. na sio kufanya kazi zao ki-local. Nakumbuka sana nondo za uhakika za Prof. Kamuzora (RIP) enzi zetu.
   
 19. Sorrow to Joy

  Sorrow to Joy JF-Expert Member

  #19
  Feb 11, 2012
  Joined: Jan 22, 2012
  Messages: 293
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  I like it, lazima waandikishwe upya na wengine wa-update taarifa zao. Hakuna haja ya serikali kukwepa hili. Safi sana, natamani asasi za kiraia ziingilie kati kuwasaidia vijana hao.
   
 20. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #20
  Feb 11, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,765
  Likes Received: 6,090
  Trophy Points: 280

  Sure! Haki za Msingi za Kikatiba za wananchi zisichezewechezewe kana kwamba mtu anachezea sijui nini? Ni kwa haki hizi na nyinginezo za msingi taifa linakuwepo! Tunategemea kusikia kauli kutoka kwa wadau hususan Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria na Masuala ya Kibunge.
   
Loading...