MBUNGE na Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeo(CHADEMA), Tundu Lissu amemshukia Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harison Mwakyembe akimtuhumu kuwa anataka kuharibu uchaguzi wao wa uraisi wa Chama cha Wanasheria nchini (TLS) uliopangwa kufanyika Machi 18 mwaka huu.
Tundu Lissu ametaka ajumuishwe katika kesi ya Godfrey Sabato Wasonga dhidi ya TLS na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu uchaguzi wa TLS.
Mbunge Mstaafu na Mwanasheria, Lawrence Marsha akizungumza wakati wa mkutano huo.
Akizungumza na wanahabari katika Hoteli ya Southern Sun jijini Dar es Salaam, Lissu amesema kuwa Mwakyembe anamtuhumu kuhusika kuwashawishi wanasheria wawili waliofungua kesi mbili za kupinga kutokufanyila uchaguzi huo kwa madai y akuwa uchaguzi huo unaingiliwa na masuala ya kisiasa jambo ambalo lisu amelikataa akisema:
“Uchaguzi wetu wala hauhusiki na masuala ya kisiasa kwani sheria ya Chama cha Wanasheria inavyovigezo vya kuzingatia na kuheshimu Katiba yake na ndipo mwanachama anaruhusiwa kuomba uongozi pale anapokuwa amekidhi vigezo.”
Tundu Lissu akizungumza na wanahabari.
“Katika kugombea Urais wa Chama cha Wanasheria, mimi sijatumia vyeo vyangu katika chama bali nimetumia vigezo vya kisheria ya chama cha wanasheria ndio maana hata ukiangalia mwenzangu Laurence Masha naye ametokea chadema.
“Kwa hiyo kama tungeingiza mambo ya siasa asingegombea yeye tukawa wawili ndani ya chama, Mawakili waliofungua Kesi mkoa wa Dodoma na wengine wa Dar es Salaam tutahakikisha tunanunua kesi hiyo kwa kwenda Mahakamani kufungua kesi inayopinga kutokufanyika kwa uchaguzi huo, na hilo tutalitekeleza kabla ya kufanyika kwa uchanguzi huo ili uchaguzi wetu hauvurugiki,” Alisema Lissu
CHANZO: Global Publishers