Uchaguzi mkuu Zambia.....

Uchaguzi mkuu Zambia.....

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
49,320
Reaction score
117,667
Hivi kuna mtu anaefuatilia huu uchaguzi mkuu wa Zambia?
nimeshangaa kuwa Uchaguzi unafanyika baada ya Rais kukaa mwaka mmoja tu
kuna anaejua why?

Na huyu Rais alishinda kwa tofauti ya kura elfu 20 tu
na ndani ya mwaka mmoja anakutana tena na mpinzani wake

Kuna anaejua kidogo zaidi ya huu uchaguzi wa Zambia?
 
Michael SATA alifariki, ndio uchguzi ukafanyika mwaka jana kumalizia muhula
 
Hivi kuna mtu anaefuatilia huu uchaguzi mkuu wa Zambia?
nimeshangaa kuwa Uchaguzi unafanyika baada ya Rais kukaa mwaka mmoja tu
kuna anaejua why?

Na huyu Rais alishinda kwa tofauti ya kura elfu 20 tu
na ndani ya mwaka mmoja anakutana tena na mpinzani wake

Kuna anaejua kidogo zaidi ya huu uchaguzi wa Zambia?

Kwenye uchaguzi huu Rais Edgar Lungu, wa Chama Tawala cha Patriotic Front(PF) anatetea nafasi yake aliyoingia madarakani mwaka uliopita 2015 baada ya kifo cha Michael Satta.
Mpinzani wake mkuu ni Hakainde Hichilema, wa chama cha United Party for National Development(UPND) na ndiye Rais wa Chama hicho.
Ndugu Hichilema ni mfanyabiashara tajiri huko Zambia anagombea kwa awamu ya 5 safari hii, Mwaka 2006 na 2011 aligombea kwenye Uchaguzi Mkuu na kuambulia nafasi ya 3.
2008 na 2015 aligombea kwenye Uchaguzi Mdogo kufuatia vifo vya Marais Levy Mwanawasa na Michael Satta na kwa Mwaka 2015 alishika nafasi ya 2 baada ya kutoa upinzani kwa Rais Edgar Lungu wa PF.

Medani za Siasa za Nchi ya Zambia zinaonesha Mfanyabiashara huyo Tajiri Hakainde Hichilema atatoa upinzani mkubwa baada ya kuungwa mkono na makundi mengi ya Vijana,Wafanyabiashara wadogo, wakulima na wafugaji kama ambavyo Rais Satta alivyojinyakulia umaarufu na kumshinda Rais aliyekuwa akitetea nafasi yake Rupiah Banda.
 
Back
Top Bottom