Uchaguzi Mkuu wa Yanga ni Juni 05, 2016

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo imetangaza Juni 05, 2016 kuwa siku ya Uchaguzi Mkuu wa viongozi ndani ya klabu ya Young Africans SC ya jijini Dar es salaam.

Akiongea na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi TFF, Wakili Aloyce Komba amesema mchakato mzima wa uchaguzi wa klabu ya Young Africans utakuwa ndani ya siku 33, ambapo mchakato unatarajiwa kuanza rasmi Mei 03, 2016.

Komba amesema jukumu lao Kamati ya Uchaguzi TFF ni kusimamia na kuhakikisha Uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo unafanyika katika hali ya demokrasia.

Ifuatayo ni kalenda ya mchakato wa Uchaguzi katika klabu ya Young Africans SC:

Mei 03, 2016 Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi TFF, atatangaza mchakato wa kulabu ya Young Africans, nafasi zinazogombewa na kubandika kwenye mbao za matangazo.

Mei 04-9, 2016 – Kuanza kuchukua fomu za kugombea na mwisho wa kurudisha fomu kwa wagombea.

Mei 10, 2016 Kamati ya Uchaguzi TFF itakaa kikao cha mchujo wa awali wa wagombea na kuandika barua za kuwajulisha wagombea juu ya mchujo wa awali.

Mei 11, 2016 Kamati ya Uchaguzi TFF itachapisha na kubandika kwenye mbao za matangazo orodha ya awali ya wagombea.

Mei 12-13, 2016 Kipindi cha kupokea na kuweka pingamizi kwa wagombea wote.

Mei 14-15, 2016 Kamagi ya Uchaguzi TFF itapitia pingamizi zote na kufanya usajili wa wagombea.

Mei 16, 2016 Kamati ya Uchaguzi TFF itatangaza na kubandika kwenye mbao za matangazo matokeo ya awali ya usahili.

Mei 17, 2016 Sekretarieti kuwasilisha masuala ya kimaadili kwenye Kamati ya Maadili ya TFF.

Mei 18-19, 2016 Kamati ya Maadili TFF itapokea, kusikiliza na kutolea maamuzi ya kamati ya maadili.

Mei 20, 2016 Kamati ya Maadili ya TFF itatangaza maamuzi ya kamati.

Mei 21-22, 2016 Kipindi cha kukata Rufaa kwa maamuzi ya masuala ya Kimaadili kwenye kamati ya Rufaa ya Maadili TFF.

Mei 23, 2016 Kamati ya Maadili tff itasikiliza rufaa za kimaadili.

Mei 24, 2016 Kamati ya Rufaa ya Maadili itatoa maamuzi ya Rufaa.

Mei 25-26, 2016 Kipindi cha kukata Rufaa dhidi ya Kamati ya Uchaguzi kwenye kamati ya Rufaa ya Uchaguzi TFF.

Mei 27-28, 2016 Rufaa kusikilizwa na kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF.

Mei 29, 2016 Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi TFF kutangaza maamuzi ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF.

Mei 30, 2016 Kamati ya Uchaguzi TFF kuchapisha orodha ya mwisho ya wagombea na kutangazwa na kubandikwa kwenye mbao za matangazo.

Mei 31 – Juni 04, Kipindi cha kampeni kwa wagombea.

Juni 05, 2016 siku ya Uchaguzi Mkuu wa klabu ya Young Africans.

Wakati huo huo Kamati ya Rufaa ya TFF Jumamosi, itasikiliza pia rufaa ya klabu ya Geita Gold pamoja na rufaa ya kocha msaidizi wa Toto Africans Choke Abeid,
 
Cha zaidi alichofanikiwa mpaka sasa toka tumfahamu ni timu yetu yanga kutolewa 'kiume' raundi za awali..!!sasa kabakiza nini tena?5 - 0 Kama vile zimemshinda kulipa,Habari ya uwanja miaka inakatika hata kifusi hatuoni..
Hivi ule tuliombiwa tubebe mashoka,mapanga na majembe kule Bunju umeishia wapi?
 
Si Bure,pengine aliyeturoga Kafa..!Jangwani sasa ni mazalia ya mbu..kambale waweza kuvua..!Hamna kiwanja,vibonde wetu afrika ni shelisheli na APR..!
 
Mnapowalazimisha yanga kufanya uchaguzi je wanachama wakiamua kuchagua viongozi walewale itakuwa nini maana nguvu iko kwa wanachama Bmt wanasema uongozi sio halali hamuoni kuwa itakuwa aibu kwenu nyie mnaotaka kuwalazimisha uchaguzi wana yanga?
 
Back
Top Bottom