Kamati Kuu CHADEMA imepoteza uhalali wa kuchuja wagombea

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
22,178
41,706
IMG-20250109-WA0036.jpg

Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akiwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu.

Inawezekana itaonekana kuwa ni kitu cha ajabu kwa baadhi ya watu wanaoamini kwenye kufanya mambo kimazoea, lakini ukweli ni kwamba Kamati Kuu ya CHADEMA imepoteza kabisa uhalali wa kuchuja wagombea kwenye uchaguzi unaotarajiwa kuanza kufanyika kuanzia tarehe 13/01/2025.

Kamati kuu hii ambayo imegawanyika na yenye wajumbe wanaopita kwa wajumbe wa mikutano ya uchaguzi, kuwaombea wagombea wanaowaunga mkono kura, inawezaje kufanya maamuzi bila ya kutanguliza mbele maslahi ya wagombea wao?

Kisheria siyo tu haki hutakiwa itendeke, bali pia inatakiwa ionekane imetendeka. Hawa wajumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA wanapungukiwa sifa hiyo ya kuaminika kwamba watatenda haki badala ya kutanguliza maslahi ya wagombea wanaowaunga mkono.

Kwa ushauri wangu Kamati Kuu iangalie mambo tu ya msingi kwa wagombea, na majina ya wagombea WOTE yapelekwe kwenye vikao vya uchaguzi vikachague wagombea kwa jinsi itakavyokuwa.
 
Sasa hii saccos ndiyo unataka na yenyewe iongoze nchi?
Ndiyo. Tatizo la nchi kuongozwa na SACCOS ni lipi?

Kama watu wamefanikiwa kuendesha SACCOS kama chama Cha siasa Kwa miaka zaidi ya 30 huku chama kilichoko madarakani kisijue kuwa CHADEMA ni SACCOS , watashindwaje kuendesha nchi.

Mramba aliposema "hata kwa kula nyasi , ndege ya Rais ni lazima inunuliwe.." bado fikra zilikuwa ni zile zile za kuwaona watanzania wengine ni Ng'ombe.
 
Back
Top Bottom