Uchaguzi Mkuu Umepita, Sasa Kazi Tu!

Uchaguzi Mkuu Umepita, Sasa Kazi Tu!

HKigwangalla

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2008
Posts
722
Reaction score
971
Na. Dkt. Hamisi Kigwangalla.

Uchaguzi Mkuu Tanzania, mwaka 2015 umeisha salama. Tunamshukuru Mungu kwa kuwapa watanzania hekima na busara ya kushiriki mchakato huu kwa amani na utulivu mkubwa. Ushindani ulikuwa mkali sana kuliko wakati wowote ule katika historia ya nchi yetu. Ushindani ndiyo, kwa mtazamo wangu, nguzo kuu kwenye jitihada za kuleta mapinduzi ya haraka kwenye mfumo wetu wa demokrasi.

Kuna mambo makubwa yafuatayo ya kujifunza:

Kwanza, kwamba ushindani siyo upinzani, na kwa maana hiyo siyo jambo la kututenganisha na kutugawa. Kwamba, tujifunze kutofautiana zaidi kwa hoja za msingi za namna tunavyofikiri tofauti juu ya njia mbalimbali zilizopo za kuleta maendeleo kwenye nchi yetu. Na hii iishie hapo hapo tu - tutofautiane kiitikadi. Tudumishe udugu wetu; tusibinafsishe tofauti zetu kisiasa.

Tukubaliane kutofautiana tu lakini tusigombane wakati kila mtu akianza kuvutia kwake. ‪#‎SisiNiNdugu‬. Kampeni zimeisha, siasa zimeisha,‪#‎SasaKaziTu‬. Tuungane nyuma ya Rais wetu kufanya kazi ya kuijenga‪#‎TanzaniaTuitakayo‬.

Tuulinde udugu wetu kwa nguvu zetu zote. Tuulinde mshkamano wetu kwa nguvu zetu zote. Tuulinde umoja wetu kwa nguvu zetu zote. Haya ni mambo yanayotuunganisha. Ni tunu za Taifa letu.

Pili, mabadiliko ya ukweli yatatokea ndani ya CCM kwa presha ya upinzani toka nje ya CCM. Mbio tulizokimbizwa mwaka huu zitakuwa chachu ya ukweli ya kutufanya tufanye kazi kwa nguvu zaidi ili tuendelee kujijengea uhalali wa kuchaguliwa na wananchi. Sidhani kama kuna MwanaCCM wa kweli atalegea kazini kuanzia sasa.

Binafsi nina matumaini makubwa sana na Ndg. John Pombe Magufuli, kuwa atatuvusha kwenye hali hii, ambapo tunalazimika kuujenga upya uhalali wetu wa kuongoza nchi ili 2020 tusipate kazi kubwa ya kampeni. Kazi yetu ya sasa inatakiwa iwe kampeni tosha kabisa. Bunge ni lazima liikimbize serikali kufanya kazi yake siyo ligeuzwe kuwa mahali pa kufanyia siasa za 'siasa', badala ya siasa za kazi! Party caucus ya CCM ni lazima iwe na nguvu zaidi kuliko ilivyokuwa nyuma huko.

Tuna changamoto za kuhakikisha fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo inayowagusa wananchi zinafika kwenye halmashauri zetu nchini kama zilivyopitishwa kwenye bajeti na kwamba fedha zinazokusanywa kutokana na vyanzo vya ndani ya halmashauri zitumike zaidi kutekeleza miradi ya maendeleo kuliko matumizi ya kawaida; tuna changamoto ya kuhakikisha ahadi tulizotoa zinatekelezwa kwa wakati; tuna changamoto ya kuhakikisha tunabana matumizi yetu ya kawaida na kuwekeza zaidi kwenye miradi ya maendeleo; na pia tuhakikishe tunahamasisha na kusimamia zaidi uwajibikaji na nidhamu ya kazi ili kwenda sambamba na spidi ya mahitaji ya maendeleo wanayoitarajia wananchi.

Ili kuyapatia ufumbuzi mambo haya, ni lazima tufanye mabadiliko ya uhakika na ya haraka kwenye serikali na kwenye chama chetu. Ni lazima tukuze uchumi wetu kwa haraka ili tuzalishe ajira na tukusanye kodi ya kutosha kuwahudumia vizuri zaidi watanzania wote.

Ili kutia chachu ya kukua kwa uchumi kwa haraka, tunalazimika kutumia approaches zinazotokana na nadharia kama za Kigwanomics: kwamba tuwekeze kwa watanzania zaidi kwenye sekta zinazozalisha ajira kwa wingi na kwa haraka, mfano sekta za kilimo, mifugo, uvuvi, uchimbaji madini etc, na viwanda vyenye backward linkage na sekta hizi - ni lazima tuanzishe 'mifuko maalum miwili' ya kukopesha wawekezaji (wa kati na wakubwa) wa ndani. Mfuko wa wawekezaji kwenye mashamba makubwa na viwanda, na mfuko wa kukopesha watu wadogo wadogo (mama ntilie, bodaboda, wamachinga, wasindikaji wadogo wadogo etc). Na ni lazima tuigawe Tanzania kwenye kanda za kiwekezaji.

Miradi hii ni lazima iendane na uwekezaji kwenye sekta za mawasiliano ya barabara, reli, nishati ya umeme na mawasiliano ya simu na intaneti.

Tatu, nimejifunza somo kubwa sana kwenye uongozi kutokana na uchaguzi huu, kwamba 'hard work pays', kufanya kazi kwa bidii kunalipa, Rais wetu Ndg. Magufuli amekuwa Rais, kwa kiasi kikubwa, kwa kubebwa na rekodi yake ya nyuma ya utendaji. Ni mtu wa ku-deliver tu. Tungepata shida sana kumpigia kampeni mgombea wa aina nyingine yoyote ile zaidi ya huyu 'mchapakazi'.

Jimboni kwetu Nzega Vijijini hakukuwa na ugumu hata kidogo kwenye kampeni kwa sababu wananchi waliishaamua kumpa kura zote Ndg. Magufuli kwa rekodi yake, na Ndg. Kigwangalla kwa rekodi yake. Kila mahali walikuwa wakiniambia, nyie wawili mmeishapita tu. Subirini kuapishwa. Nimefanya kampeni kwenye jimbo letu lote kwa siku 12 tu na tumeshinda kwa takriban asilimia 80!

Naamini Ndg. Magufuli hatobadilika, maana anajua kilichotubeba uchaguzi huu ni rekodi yake ya ku-deliver. Na mimi ninawaahidi wananchi wa jimboni kwetu kuwa sintobadilika, nitawapigania siku zote za uongozi wangu.

Nikitumia somo hili zito la namna Ndg. Magufuli alivyoingia ikulu (kwa rekodi ya uchapakazi wake), sina namna nyingine zaidi ya kuchapa kazi na kuleta matokeo chanya kwenye maisha ya wana Nzega Vijijini wenzangu. Sina namna. Nitafanya kazi kwa nguvu na spidi kubwa zaidi ya miaka mitano iliyopita.

Na wananchi tujiandae kufanya kazi kwa spidi ya Rais wetu. Na wanaNzega Vijijini tujiandae kufanya kazi kwa spidi ya Mbunge wetu...maana nitawakimbiza kweli kweli. Kama huko nyuma mlinisifia kwa kazi tu, nikiongeza spidi sijui itakuwaje! Hakuna 'short-cut' kuelekea mabadiliko ya kweli. Mabadiliko ya kweli yataletwa na sisi wenyewe kujituma zaidi kufanya kazi.

 
MATARAJIO YANGU KWA JOHN POMBE MAGUFULI
Baada ya kuapisha kuwa Rais wa awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 05.11.2015 (10:49 A.M), mimi kama raia wa Tanzania nina matarajio yafuatayo kwa Mh. Dr.John Pombe Magufuli.
? Kutatua haraka tatizo la Zanzibar lililotokana na ZEC kufuta uchaguzi pasipo na sababu za Kimsingi.Hii ni hatari kwa mustakabali wa Taifa na Wananchi wake.
? Kuwaunganisha Watanzania ambao wametofautiana kutokana na Vyama vya siasa kuwagawa kwa misingi ya itikadi za vyama,dini,makabila na ukanda wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba,25,2015.Makovu haya ni mengi na kwa watu wote sehemu zote.
? Kuinua ari ya uwajibikaji na uchapakazi Serikalini na watu binafsi na Viongozi wote watakaozembea wawajibishwe mara moja.
? Kuboresha huduma za afya katika Hospitali zote nchini na Zahanati na kuepuka Viongozi kwenda kutibiwa nje ya nchi.
? Kuhakikisha kila anayepaswa kupata elimu anaipata na hatimaye kufuta ujinga ambao umekithiri sana hivi karibuni.(Rejea kura nyingi kuharibika)
? Kuwashughulikia wote waliohusika na watakaohusika na rushwa (Matumizi mabaya ya Ofisi na mali za Umma kwa manufaa yao binafsi)
? Kuboresha Viwanda vilivyokuwepo kwa kuvipatia ruzuku na kuondoa mlolongo wa kodi na michango ambayo badala ya kuviendeleza huviumiza zaidi.
? Utatuzi wa matatizo ya wakulima uwe wa kweli na wenye tija.Matatizo kama pembejeo,masoko,mitaji n.k huwarudisha nyumba sana wakulima na hatimaye Taifa.
? Ajira kwa Vijana ambao wanamaliza shule na vyuo. Kuiunua viwanda,kufufua kilimo,kukomesha rushwa,uwajibikaji na elimu za ufundi kwa pamoja zitatoa ajira kwa vijana.
? Kutokomeza umaskini wa kipato kwa wananchi wa hali ya chini kwa kufufua kilimo,kutoa ajira,kukomesha rushwa na kutoa huduma safi za afya.
? Kupunguza pengo kati ya wenye nacho na wasionacho (Tajiri na Maskini) kwa kupunguza mianya ya unyonywaji kwa wasionacho.
Ni matumaini yangu kila Mtendaji atatoa ushirikiano mkubwa katika kufanikisha haya na JPM atafuatilia kwa ukaribu watendaji wasio na tija wenye nia ya kuendekeza ulaji na upigaji wa madili badala ya kuleta maendeleo.
 
Sawa mhe.

Ila mpasuko uliokuwepo hausahauliki kwa wepesi wa aina hiyo...

Makovu ya uchaguzi hayaishi kwa kuambiwa hapa kazi tuu...

Kejeli na dhihaka za uchaguzi hazitaisha kirahisi kwa kuwambia wananch wawe na ushirikanno na viongozi.

~Nearly 40% yawanchi mioyo yao haipo kabissaaa kwenye serekali hii, kama hakuna juhud za ziada zitakazofanyika kwenye hii 40% basi kila jema kwao lazima litaonekana baya.

Nashauri serekali kutoipuuza hata kidogo 39% or40%

Zingatieni hoja zao, na mawazo yao,
 
Hapa Kazi Tu ya Rais kukagua madaftari ya mahudhurio?
Tayari jamaa yenu ameshaonesha udhaifu katika uteuzi wa AG.
Tunaendelea kusubiri uteuzi mwingine.
 
Mkuu HKigwangalla, kwanza hongera kwa ushindi wa kishindo, pili nimeziona juhudi zako katika kuhakikisha unakumbukwa na haswa mchango wako, usisahauliwe!, kiukweli juhudi kama hizi, kipindi kama hiki zinalipa sana!.

Kuna msemo usemao, ukibebwa, bebeka!, pale mwanzo ulibebwa, na baada ya kubebwa, hukubweteka bali ulibebeka na this time wote tumekushuhudia jinsi ulivyojibeba!.

Kazi kubwa iliyopo mbele ya JPM ni kuunda kikosi kazi, hivyo hiki ni kipindi anapokea mapekezo, kama kuna fursa za kuhakikisha mtu anapendekezwa, this is the time!, na ikitokea mtu huna uhakika kama utapendekezwa au la, then unahakikisha unajipendekeza!.

Keep it up!, inalipa!.

Pasco
 
Mmefanya siasa za kijinga za matusi,kihuni, ubinyaji wa demokrasia halafu leo mnataka yasahaulike kirahisi rahisi hivyo.

Kwetu unyamwezini kuna falsafa moja inasema: 'hawi lingi ndoho igongozi', yaani 'kwenye ngoma za ushindani, malenga wanaoshindana huwa hawamwagiani sifa'. Lakini hii hutokea tu wakiwa jukwaani, nje ya hapo, ni ndugu na wanazungumza na kushirikiana tu. Nadhani falsafa hii inafanya kazi kwenye majukwaa ya kisiasa. kwamba, wakati wa kampeni hauwezi kutegemea mimi mgombea/mpiga kampeni wa CCM, nimsifie mgombea wa ACT/mpiga kampeni wa ACT...hii ndiyo haswa maana ya kampeni!

Bahati mbaya sana kwnye uchaguzi lazima mmoja wetu ashinde...
 
Mkuu HKigwangalla, kwanza hongera kwa ushindi wa kishindo, pili nimeziona juhudi zako katika kuhakikisha unakumbukwa na haswa mchango wako, usisahauliwe!, kiukweli juhudi kama hizi, kipindi kama hiki zinalipa sana!.

Kuna msemo usemao, ukibebwa, bebeka!, pale mwanzo ulibebwa, na baada ya kubebwa, hukubweteka bali ulibebeka na this time wote tumekushuhudia jinsi ulivyojibeba!.

Kazi kubwa iliyopo mbele ya JPM ni kuunda kikosi kazi, hivyo hiki ni kipindi anapokea mapekezo, kama kuna fursa za kuhakikisha mtu anapendekezwa, this is the time!, na ikitokea mtu huna uhakika kama utapendekezwa au la, then unahakikisha unajipendekeza!.

Keep it up!, inalipa!.

Pasco

Pasco, nimekusoma. Nimekuelewa.

Nakushukuru kwa neno lako la shukrani na ushauri wako umezingatiwa...hahahahahh!
 
Kwetu unyamwezini kuna falsafa moja inasema: 'hawi lingi ndoho igongozi', yaani 'kwenye ngoma za ushindani, malenga wanaoshindana huwa hawamwagiani sifa'. Lakini hii hutokea tu wakiwa jukwaani, nje ya hapo, ni ndugu na wanazungumza na kushirikiana tu. Nadhani falsafa hii inafanya kazi kwenye majukwaa ya kisiasa. kwamba, wakati wa kampeni hauwezi kutegemea mimi mgombea/mpiga kampeni wa CCM, nimsifie mgombea wa ACT/mpiga kampeni wa ACT...hii ndiyo haswa maana ya kampeni!

Bahati mbaya sana kwnye uchaguzi lazima mmoja wetu ashinde...

Sio kwa staili ya matusi, kejeli, dhihaka na udhalilishaji uliotokea. Kuna mchangiaji kasema don't ignore the 39%.
 
Hapa Kazi Tu ya Rais kukagua madaftari ya mahudhurio?
Tayari jamaa yenu ameshaonesha udhaifu katika uteuzi wa AG.
Tunaendelea kusubiri uteuzi mwingine.

Akionyesha udhaifu si ndo furaha yenu? Mbona mnaonekana kama mnaumia sana...nyie ndo wale mnaoingia kazini mnaacha koti kwenye kiti afu mnaingia mtaani...no wonder ulipinga sana JP kuingia ikulu...wewe utakuwa ni kibaka-mvivu
 
ndugu yangu Kingagwala heshima kwako kuna jambo moja tu muhimu naomba usisahau kumkumbusha rais wetu nalo ni mahakama ya mafisadi sisi wananchi wakawaida kuwashuhulikia mafisadi kwetu ni jambo kubwa kuliko yote aliyoahidi tunaamini akiliweza hilo mengine yote yatakua rahisi sana naomba miwapo bungeni mkumbusheni aanze nalo mapema
 
Zanzibar je!? Kazi haiwezi kuanza bila Zanzibar kurudishiwa ushindi uliopokonywa..
 
Mkuu HKigwangalla, kwanza hongera kwa ushindi wa kishindo, pili nimeziona juhudi zako katika kuhakikisha unakumbukwana haswa mchango wako, usisahauliwe!, kiukweli juhudi kama hizi, kipindi kama hiki zinalipa sana!.

Kuna msemo usemao, ukibebwa, bebeka!, pale mwanzo ulibebwa, na baada ya kubebwa, hukubweteka bali ulibebeka na this time wote tumekushuhudia jinsi ulivyojibeba!.

Kazi kubwa iliyopo mbele ya JPM ni kuunda kikosi kazi, hivyo hiki ni kipindi anapokea mapekezo, kama kuna fursa za kuhakikisha mtu anapendekezwa, this is the time!, na ikitokea mtu huna uhakika kama utapendekezwa au la, then unahakikisha unajipendekeza!.

Keep it up!, inalipa!.

Pasco

Hadi tarehe 19 tutashuhudia vionjo vingi toka watarajia!
 
Back
Top Bottom