shumanice
Member
- Jul 21, 2011
- 64
- 25
Salaam wanajamvi.
Awali ya yote naomba niwakumbushe kuwa siku si nyingi sana zilizopita tulikuwa na mchakato wa Katiba ambao ulikwama na hakuna ajuae ulipokwamia na "what is next" yake!. Nikikumbuka vizuri wakati mkulu anatoa hotuba zake (ile ya kutangaza mchakato wa kuanza kukusanya maoni na ule wa uzinduzi wa BMK) moja ya kipaumbele ilikuwa ni kuwapa Watanzania Katiba mpya kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Kwa maana nyingine ni kwamba uchaguzi wa mwaka huu ulitakiwa kufanyika chini ya Katiba mpya ambayo miongoni mwa mambo "tuliyopendekeza" sisi wananchi ni pamoja na mabadiliko kwenye vipengere muhimu. Kwa mfano suala kama la kuwa na tume huru ya uchaguzi, kuruhusu mgombea binafsi, matokeo kuhojiwa, nk ni baadhi tu ya yale mambo muhimu tuliyohitaji yaingie kwenye katiba.
Sasa mchakato umekwama kama nilivyosema hapo juu na hakuna ajuaye ulipokwamia!! Lakini harakati za utangazaji wa nia unaendelea; ishara ya kwamba uchaguzi upo pale pale. Sina shaka kuwa uchaguzi utafanyika kwa mujibu wa Katiba ya 1977.
Lakini ikumbukwe kuwa viongozi wengi wakiowemo wa upinzani na wachama tawala walikuwa wakiunga baadhi ya vipengere vya Katiba pendekezwa vikiwemo tajwa hapo juu. Cha ajabu ni kwamba hakuna anaekumbuka tena!!! Woote (watangaza nia na wapiga kura) tumesahau kuwa uchaguzi utafanyika chini ya Katiba ya 1977 ambayo haijafanyiwa mabadiliko na hivyo kutokuwa na tume huru ya uchaguzi, wala hakutakuwa na mgombea huru, nk, badala yake tumekalia kushabikia tuu watangaza nia bila hata kufuatilia hizo nia zao ni dhati kweli?.
Kwanini nasema hakutakuwa na mabadiliko?
Bunge la sasa ndo la mwisho na sijaona mbunge hata mmoja mwenye nia ya kuwasilisha hoja binafsi ya kuomba Katiba kufanyiwa mabadiliko. Kila mmoja yupo busy majimbini na kutangaza nia. Sina hakika bunge likivunjwa kuna namna ya kuliitisha ili lifanye mabadiliko ya Katiba. Kwa maana hiyo tujiandae kwa kila kitakachotokea wakati wa uchaguzi kwani I see "business as usual". Ama kweli watanzania bado tumelala!!!!