Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,494
- 113,590
Wanabodi,
Kwanza naomba nikiri kuwa nimeandika uzi huu kwa kuwa inspired na mwana jf huyu,
Mkuu, Steven Robert Masatu, kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake, na mafanikio kwenye kilimo yanategemea msimu, kuna msimu wa mvua, ni kipindi cha kulima, kupanda na kupalilia, kuna msimu wa kiangazi ni wakati wa kuvuna, ila pia kuna wakati kunatokea ukame, hakuna mvua, hakuna mazao hakuna kuvuna na kinachofuatia ni baa la njaa!. Pia kuna wakati kunanyesha mvua kubwa zaidi kupitiliza, hadi kuleta maafa ya mafuriko, kama elnino, lakini mavuno ya maeneo ya mabondeni baada ya elnino ni mavuno makubwa ajabu, kutokana na kurutubishwa kwa siltation ya elnino!.
Kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu, ndio kipindi cha neema kwa media na waandishi!, huu ndio wakati wetu wa mavuno, kama ni mvua hizi sasa mvua za elnino!.
Zamani enzi za chama kimoja, kwa media kuripoti uchaguzi mkuu, ilikuwa bure!, media ndio zilikuwa zinawagharimia waandishi wake kuripoti uchaguzi. Vyama vingi vilipoanza, bure ikaendelea ila ili chama kipate preferential coverage rupia ilianza kupenyezwa kidogo kidogo kwa siri and unofficial.
Kuanzia uchaguzi wa 2005, media campaign zilianza kuwa official na waandishi kulipwa sasa ilikuwa rasmi, mfano gazeti la Mtanzania lilitake side na kumsaidia mgombea mmoja tuu fulani ndani ya CCM na lilifanya kazi kubwa kuwaangamiza wagombea wengine wowote tishio, hata ikibidi kuwatungia story za uongo hadi kutengeneza picha za photoshop!, kazi hii nzuri ya media campain ilizaa matunda mema, baadhi ya wale viongozi wa kampeni hizi kuzawadiwa kuanzia ukurugenzi, hadi ukuu wa wilaya!.
Uchaguzi wa 2010, sasa ikawa sio CCM pekee bali hadi Chadema nayo ikalipa waandishi kuzunguka na mgombea wao kwenye chopa!.
Uchaguzi wa mwaka huu, neema sasa ni kubwa zaidi, CCM yenye pesa nyingi zaidi ndio itaongoza kwa kuwalipa waandishi wengi na kununua media nyingi!. CCM itanunua airtime na kununua waandishi officially from the media houses kuzunguka na wagombea wake wa urais. Ukawa nao this time watalipa media kwa media kuzunguka na mgombea wake!.
Vyama vipya kwa ACT vinavyotambua the power of media, nao, watawalipa waandishi kuzunguka na mgombea wake!.
Baadhi ya wagombea individually wenye ukwasi mkubwa wa fedha kama kina Nimrod Mkono, Mohamed Dewji, Edward Lowassa etc, nao wataunda mitandao yao ya media officially or unofficially kuwaripotia na kote huku ni fedha tuu ndio itazungumza!.
Hongereni sana wana media, hiki ni kipindi chenu cha mavuno, tukae mkao wa kula!, huwezi jua, hata mimi labda hali ya kale ka usafiri kangu ka boda boda kalikopata ajali, huenda kanaweza kufufuka au hata kubadili kutoka boda boda hadi bajaj!.
Swali la msingi la kujiuliza ni Jee, bahasha hizi wanazolipwa media na wana siasa au vyama vya siasa ni halali?, Jee ni sahihi kwa vyama na wagombea wenye pesa, kutumia pesa zao, kununua media na kuwalipa waandishi?!.
Hili suala la waandishi wa habari na bahasha, nimeishalizungumza sana hapa
Waandishi wa Habari na Bahasha: Sio Kila Bahasha ni Rushwa.
Pasco

Milion mia saba kila baada ya miezi miwili? Na watu wa media waongezewe posho? Huu ni muda wa brother wangu Pasco kupiga hela.