Mbona mambo yao yamekuwa ni kimyakimya sana?
Hawana mvuto hao wameshachelewa!!
Ndio maana ya uchaguzi. Huenda wakaja watu wenye speed kali na wenye mvuto.
The question ni kuwa kitakuwa chama kweli cha siasa, au kitaendelea kuwa kile kile kinachotumiwa na kina Marando ku-weaken na ku-destabilize opposition, au kufuga majasusi wanaokiyumbisha kila kukicha? Kama wameamua kufanya mambo kimya kimya ili kukisafisha na kutowapa nafasi wanaokiharibu well and good, tusubiri nini kitaendelea.
Wakuu,
Kutoka jikoni NCCR naambiwa jua la kurejesha fomu limekuchwa na wafuatao ndio fomu zao ziko mezani kuwania nafasi kuu saba za uongozi wa chama.
Mwenyekiti
- John Bula Dodo
- James Francis Mbatia
Makamu Mwenyekiti- Bara
Makamu Mwenyekiti - Zanzibar
- Mama Rakia Abubakari Hassan
- Hashim Rungwe
- Haji Hambari Khamis
Katibu Mkuu
- Sam Ruhuza
Naibu Katibu Mkuu- Bara
- Raurent Tara
- Joseph Serasini
Naibu Katibu Mkuu- Zanzibar
- Musa Kombo Musa
- Ali Juma Omari
Mweka hazina
Majina haya yatahakikiwa kesho katika kikao cha halmashauri kuu ya taifa kabla ya kupelekwa mkutano mkuu, a day later
- Mama Mariam Mwakingwe
- Sebastian Thomas
Katika hii miaka mitano inayoishia, Mbatia ameshindwa kuinusuru NCCR.
Chama kimeendelea kudorora kila siku, sasa huyo John Bula mbona mgeni masikioni mwangu katika duru za kisiasa, ataweza kweli kuinusuru NCCR?
NCCR inatakiwa kurudi kwenye chati kama zamani ili kuongeza ushindani na kutanua wigo wa demokrasia.Kwahiyo basi kama Mbatia atashinda tena anwajibika kubadilisha mikakati ya kukiongoza chama chake ili kiweze kushindana badala ya kusindikiza ama kutumiwa na mahasidi kuivuruga demokrasia.
Mi naamini kabisa kuwa mwenyekiti ndiye anayetoa taswira ya chama husika.
Au Bula amewekwa kumsindikiza Mbatia?Kwangu mimi bado sioni kama Bula atatoa ushindani wa kutosha kwa Mbatia.Labda kama mimi ndiye simfahamu vizuri bw.Bula naomba kufahamishwa.
BTW mbona mgombea urais mwanasheria Edmund Sengondo Mvungi hajawania nafasi yeyote?au yeye ni maalum na uraisi tuuu!!!????
Ni kweli huyu jamaa ni mgeni hata kwangu mimi katyika siasa za upinzani. Au amewekwa kama kanyabwoya kuonyesha kuwa Mbatia alikuwa na mshindani?sasa huyo John Bula mbona mgeni masikioni mwangu katika duru za kisiasa, ataweza kweli kuinusuru NCCR?
Ni kweli huyu jamaa ni mgeni hata kwangu mimi katyika siasa za upinzani. Au amewekwa kama kanyabwoya kuonyesha kuwa Mbatia alikuwa na mshindani?
Mimi sioni tatizo katika upya wa Bula, badala yake naona ishara njema kwani mtu mpya kajitokeza na kwa mantiki hiyo huenda ana jipya.
Kwa taarifa nilizo nazo Bula ni candidate anayetokea upcountry, ni changamoto hasa kwa Mbatia ambaye 'katokea' Uholanzi kuja kutetea kiti chake.
Nani kamuweka nani hapo sijui na sidhani. kila mmoja wao kajaza fomu kwa wakati wake.
Mkuu Mwita,
Sidhani kutofahamika kwa Bula kunaweza kuwa sababu pekee ya kumwangusha, itategemea competence yake. Aidha kama unavyosema, endapo ni kweli Mbatia hakufanya vizuri basi Bula anaweza kutumia upenyo huo kushinda.
Kuhusu Mvungi, sidhani kama ana umaalum wa kugombea urais, usishangae akijitokeza mtu/watu wapya kabisa kuwania urais kwa tiketi ya NCCR come 2010
wanajf,
hii ni kutaka kukuhabarisheni kwamba ndani ya chama cha nccr-mageuzi kinachondelea kwa sasa ni hatua za mwisho mwisho za kuhitimisha mchakato wa uchaguzi mkuu wa viongozi wa kitaifa wa chama.
Kama ilivyo ada, kila baada ya miaka mitano unafanyika uchaguzi wa namna hii.
Itakumbukwa kwamba hadi sasa nccr imekwisha kuwa chini ya uongozi wa wenyeviti wanne tofauti kwa nyakati tofauti
- alianza mhe.mabere marando
- akafuatia mhe.agustine mrema
- akaja mhe.aidari maguto(marehemu)
- na wa sasa mhe.james mbatia
katika uchaguzi huu, habari za ndani zinatonya kwamba wanaowania uenyekiti ni wawili (sijajua kama wote watapitishwa)
vile vile yaelekea nafasi nyinginezo kv. Makamu mwenyekiti,katibu mkuu,naibu katibu mkuu,mweka hazina zitakamatwa na sura mpya kabisa kwa sababu wengi wa waliogomea nafasi hizo na wenye mwelekeo wa kushinda si wale waliokuwa wakizishikiria.
Wachunguzi wa mambo wanasema, mwelekeo huo ni ishara kwamba chama hiki kimepania kujijenga upya kabisa, ya kale yatapita...
Tega sikio, soon nitakuhabarisheni nani kang'olewa, nani kashinda, nani kawaje.
Duru zinasema mtanange huu ni jumapili ya juma hili.