PatPending
JF-Expert Member
- Aug 17, 2007
- 491
- 102
Wadau kama mnavyofahamu leo hii ndio itifaki ya soko la pamoja la Afrika Mashariki inaanza kufanya kazi. Kuna maengi ambayo yamejadiliwa na kuandikwa humu humu kuhusiana na hili swala na haya yako katika jukwaa husika (za Kimataifa n.k).
Swali langu kuu ni moja, kutokana na maoni ya wengi humu ndani na hata huko mitaani, inaashiria ya kwamba waTanzania walio wengi hawajapendezwa aidha na uharakishwaji wa huu "ushirikiano" au vipengele vya itifaki hii na sera nzima kwa ujumla, au vyote viwili. Sasa je inakuwaje mpaka leo hii hakuna chama chochote cha siasa kitakacho kulizungumzia suala hili nyeti sana katika mustakabali wa taifa hili? Hili ni suala ambalo laweza kuwa moja la mikakati mikuu katika kampeni za uchaguzi wa wabunge na rais mwaka huu na miaka ijayo (kama zitakuwepo).
Katika nchi nyingi ambazo zimejikuta katika njia panda kama hii wananchi na wanasiasa husika wamekuwa mstari wa mbele katika kutetea maslahi ya taifa lao. Tumejionea katika nchi mbalimbali kama Uingereza (misimamo ya vyama vya UKIP na Conservative kuhusiana na Umoja wa Ulaya unaeleweka) na wengineo, wananchi wakiwa mstari wa mbele katika kutetea maslahi yao.
Sasa iweje leo hii hapa Tanzania watu mnakaa kimya ilihali kuna manung'uniko mengi tu ya chini chini ya nchi kuuzwa au kuburuzwa kuhusiana na hili suala la "ushirikiano" na mataifa mengine ya Afrika Mashariki?
Jamani amkeni sasa, mkishindwa kujitetea sasa msije mkalaumu au kutupa ngumi baadae !!!