Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Bango la mgombea wa urais nchini Djibouti
Raia wa Djibouti leo wanapiga kura kumchagua rais mpya.
Lakini tayari kuna utata kwani baadhi ya vyama vya upinzani vinasusia uchaguzi huo, ishara ya jinsi upinzani umegawanyika hivyo kujipata katika hali hiyo hafifu mbele ya chama tawala cha rais aliyeko madarakani, Ismael Omar Guelleh.
Upinzani umekuwa ukilalamika kwamba serikali, haijaweka mazingira sawa ya ushindani.
Wagombea vinara wa upinzani ni Omar Elmi Kaireh na Mohamed Daoud Chehem, lakini kwa sababu ya kutokuwa na umoja miongoni mwao, watakuwa na kibarua kigumu na wachambuzi wa kisiasa wanasema hawatarajiwi kuung'oa utawala wa rais Ismael Omar Guelleh ambaye amekuwa madarakani tangu 1999.
Rais Guelleh ni rais wa pili tu tangu nchi hiyo ijikomboe kutoka kwa utawala wa kikoloni wa Ufaransa mwaka wa 1977.
Djibouti ni nchi iliyozungukwa na mataifa majirani ya Somalia, Yemen na Eritrea ambayo yamekumbwa na mizozo ya kisiasa.
Bandari ya Korale
Djibouti pia inategemewa sana na Ethiopia ambayo haina ufuo wa bahari.
Meli katika bandari ya Dorale nchini Djibouti
Lakini pia inatumiwa kama kituo muhimu kwa majeshi ya Marekani na Ufaransa huku Saudi Arabia nayo pia ikitaka kuwa na kituo cha kijeshi nchini humo.
Uwepo wake katika ghuba la Aden na karibu sana na njia ya baharini ya Suez imeifanya Djibouti kuwa kitovu na kiunganishi muhimu kwa safari za meli za kimataifa.
Mkutano wa kampeini nchini Djibouti
Viongozi hao wa upinzani wanadai hizo ni baadhi ya sababu zinazoifanya jumuiya ya kimataifa kufumbia jicho mfumo wake hafifu wa kidemokrasia.
Wanadai polisi huwanyanyasa kwa kutafuta vijisababu vya kuendeleza vitendo vya mateso dhidi yao huku wakiwanyima nafasi ya kujieleza katika vyombo vya habari.
Pia wanasema serikali imekataa kutekeeza mabadiliko ya kisiasa yaliyopendekezwa katika makubaliano nao baada ya vurugu za uchaguzi wa ubunge hapo 2013, madai ambayo serikali imeyakana.
Chonzo: BBC Swahili