Uchaguzi mdogo wanukia Sumbawanga Mjini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi mdogo wanukia Sumbawanga Mjini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OSOKONI, Sep 12, 2012.

 1. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #1
  Sep 12, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,800
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  Uchaguzi Sumbawanga Mjini, unanukia baada ya muda wa kukata rufani kwa mujibu wa sheria za uchaguzi kupita na upande wa mrufani kugubikwa na ukimya.

  Katibu wa CCM (itikadi na uenezi), Nape Nnauye, alipotakiwa kuzungumzia msimamo wa chama kuhusiana na rufani hiyo, alisema aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Aeshi Hilaly, asingeweza kukata rufani bila kuwasiliana na uongozi.
  Nape pia, aliongeza kuwa suala la kukata rufani lilitolewa na Aeshi na sio chama ambapo alimtaka mwandishi wa gazeti hili kuwasiliana na mhusika (Aeshi), iwapo anataka kujua hatma ya kauli hiyo.

  “Wewe unauliza, lakini unajua ni nani aliyetoa kauli ya kukata rufani? Tamko la kukata rufani ilitolewa na yeye au chama? Kuuliza wapi tumefikia, muulize yeye. Yeye asingeweza kukata rufani bila kuwasiliana na uongozi,” alisema Nape.

  Aidha Nape, alipohojiwa juu ya hatua iliyofikiwa ya ukusanyaji ushahidi wa tetesi za ufisadi kwa baadhi ya makada wa chama hicho wakiwamo wabunge, unaofanywa na kamati ya maadili ya CCM, alisema kwa sasa hawako kwenye nafasi ya kutoa taarifa ya kamati hiyo.

  NIPASHE ilipozungumza na Aeshi jana alisema; “Nimekiachia chama, ni muda mrefu umepita…nasubiri majibu. Mimi si msemaji wa chama, nasubiri kukaa na chama ndipo niweze kueleza, maana hata hivyo siwezi kujua kama wewe kweli ni mwandishi wa NIPASHE au la,” alisema Aeshi.

  Kwa upande mwingine, NIPASHE ilimtafuta Naibu Spika, Job Ndugai, kujua kama Bunge limeshapeleka taarifa kwa Tume ya Uchaguzi Nchini (NEC) kwamba jimbo hilo liko wazi baada ya muda wa kukata rufani kupita kisheria, alisema:

  “Tutalitolea maelezo Oktoba kwenye mkutano ujao wa Bunge. Hatuna uhakikika, tunataka kujiridhisha kwanza kwa mahakama ili tuweze kulitolea maelezo suala hilo kwenye Bunge lijalo.”

  Aprili 30 mwaka huu, Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Sumbawanga ilitangaza kuenguliwa kwa ubunge wa Aeshi (CCM), baada ya kushindwa katika kesi iliyokuwa inamkabili ya ushindi wake uliodaiwa kugubikwa na utata dhidi ya aliyekuwa mgombea mwenzake Norbert Yamsebo (Chadema) katika Jimbo la Sumbawanga Mjini, Oktoba, 2010.

  Katika uchaguzi huo, Aeshi alishinda kwa zaidi ya kura 17, 328 dhidi ya Yamsebo aliyepapata kura17,132.
  Kesi hiyo namba 01 ya mwaka 2010 ilifunguliwa na Yamsebo.

  Uamuzi wa kutengua matokeo hayo ulitolewa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Bethwell Mmilla, ambaye alisikiliza kesi hiyo na kuisoma kwa takribani saa matatu.

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #2
  Sep 12, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Mtu anayetumia sigara kubwa anaweza kukata rufaa?
   
 3. Landala

  Landala JF-Expert Member

  #3
  Sep 12, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 938
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Kwa kweli ccm wana hali ngumu kama uchaguzi ukirudiwa wajue kuwa hawana chao kwa jinsi wa sumbawanga mjini walivyokichoka chama hiki cha magamba.
   
 4. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #4
  Sep 12, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  huyu alisema aesh alisema wazi kuwa kikwete ni MUNGU, yeye ni YESU KRISTO, na yule DIwanini ROHO MTAKATIFU, sasa mahakama imetengua ushindi wa YESU KRISTO!!!!!!!
  laana hizi za kujiita Mungu zitawatafuna wote watatu, kwa kuwa sijamsikia kikwete akikana kuwa yeye si MUNGU kama alivyotajwa huko Sumbawanga, ni wakati muafaka wa yeye kukataa hili
   
 5. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #5
  Sep 12, 2012
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Hakuna ubishi CDM kuchukua jimbo uchaguzi ukiitishwa.
   
 6. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #6
  Sep 12, 2012
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 2,004
  Likes Received: 1,054
  Trophy Points: 280
  .....ni Kweli huu ni Utatu Mtakavitu.... (JK,Aeshi,Diwani)
   
 7. eumb

  eumb Senior Member

  #7
  Sep 12, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hapo kwenye red majibu yanaonyesha kuna kafrustration flani hasa baada ya CDM kumpeleka kwa Pilato. Ila pia kanikumbusha mbali sana enzi zile unaomba pocket money kwa Mdingi halafu hana hela, utakula majibu ya hasira, ha ha haaaa!!!!!
   
 8. S

  Seif al Islam JF-Expert Member

  #8
  Sep 12, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 2,158
  Likes Received: 141
  Trophy Points: 160
  Siamini hata kidogo kama ccm hawatakat rufaa coz hawana ujanja wa kushinda uchaguzi huo
   
 9. Takalani Sesame

  Takalani Sesame JF-Expert Member

  #9
  Sep 12, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Another opportunity ya kuigalagaza CCM.
   
 10. Mabreka

  Mabreka JF-Expert Member

  #10
  Sep 12, 2012
  Joined: Aug 29, 2012
  Messages: 709
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  mwaka huu magamba yatatoka tu, tunawashika kila mahali
   
 11. Kuchasoni Kuchawangu

  Kuchasoni Kuchawangu JF-Expert Member

  #11
  Sep 12, 2012
  Joined: Aug 21, 2012
  Messages: 469
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Mwigulu na Nape wapo Nkinga Igunga leo nielekezeni namna ya kupost niwaletee habari kamili.
   
 12. Kuchasoni Kuchawangu

  Kuchasoni Kuchawangu JF-Expert Member

  #12
  Sep 12, 2012
  Joined: Aug 21, 2012
  Messages: 469
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Nape na Mwigulu wapo Nkinga Igunga leo nipo kwenye tukio nielekezeni namna ya kupost habari niwaletee moja kwa moja ni mgeni ha Jf
   
 13. Electron

  Electron Member

  #13
  Sep 12, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mh this is very serious, MUNGU awarehemu na kuwasamehe, na wakatubu la sivyo wataoza wanajiona
   
 14. C

  Councious Member

  #14
  Sep 12, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni kwel ndugu maana hajui halitendalo
   
 15. Electron

  Electron Member

  #15
  Sep 12, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sirikali-ccm na mahakama yake itapiga jungu hapo utashangaa kuambiwa rufani ishawasilishwa wanavunja katiba hao kila siku.............. wanajua wakigombea watapoteza, wakikata rufaa kesi itavutwa mpaka uchaguzi ujao.....
   
 16. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #16
  Sep 12, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,847
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  CCM watateseka kama alivyoteseka Mourinho kwa Gardiola wa barcelona, kila wakichungulia
   
 17. FortJeasus

  FortJeasus JF-Expert Member

  #17
  Sep 12, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 568
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45

  Ni rahisi,fuata haya maelekezo.
  Pale katika home page ya Jamii Forums kuna majukwaa mbalimbali.
  1.Kwa kuwa hoja yako ni ya siasa bonyeza option ya ''jukwaa la siasa''.
  2.Kisha bonyeza sehemu iliyoandikwa ''post a new mesage'',
  3.Baada ya ukurasa kufunguka andika kichwa cha habari (mfano, ''Nchemba na Nape walopoka''),then shuka chini andika ujumbe wenyewe.
  4.Baada ya kufanya hivyo,chini kabisa bonyeza option iliyoandikwa ''submit''.
  5.Ukifuata hatua zote hizo kwa ukamilifu tutakuwa tumeweza kupata ujumbe wako
   
 18. Smartboy

  Smartboy JF-Expert Member

  #18
  Sep 12, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,110
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Aaa! Umenikumbusha kumbe huyu ndo alijiita utatu mtakatifu. Na kweli kanisa katoliki lililaani hii kauli ila serikali ya Jk ikatulia na hata huyo anayejiita mlezi wa vyama vya siasa sikumsikia akisema chochote. Na hii laana lazima imtafune .
   
 19. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #19
  Sep 12, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Hata nyinyiem mnajua mtashindwa! Nitakunukuu uchaguzi ukianza!
   
 20. Smartboy

  Smartboy JF-Expert Member

  #20
  Sep 12, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,110
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Bofya sehemu ambayo inasema post a new topic af andika kichwa cha habari af uanze kuflow.
   
Loading...