FairPlayer
JF-Expert Member
- Feb 27, 2006
- 4,145
- 733
Yatakutoka mengi na matusi mengi mimi binafsi hayanipati; kwani mtu hayo matusi yote yanakurudia mwenyewe sipo hapa kwa ajili ya kutukana mimi ni mtu mzima mwenye familiya na heshima zangu. Hunijui na mimi sikujui tafadhari changia mada kama huna la kuchangia nenda ukalale.
JF siyo sehemu ya watoto kuja kucheza mdako na kombolela watu wenye heshima zao wanachangia mada hapa.
Rekebisha tabia yako kuwa mstaarabu hatupo kijiweni hapa au kwenye mpira wa chandimu.
Tafadhari sana sijakutukana katika hoja zangu zote na wewe naomba jiheshimu kijana.
MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
Mkuu wangu taratibu. Yaani unasema kwa kinywa kipana kwamba S.F. Holdings siyo yake? Sema tena kwamba Mr. Price siyo sehemu ya S.F Holdings ambayo anaimiliki? Sema tena kwamba S.F holdings haimiliki shamba la kuku chini ya kampuni moja hivi. Sema tena kwamba hana kampuni inayolisha kwenye migodi. Hayo tu
itakuwa ndio anaweka historia nadhani, ni vema sana ili watu watakaogombea ubunge next time wajipange kweli na wasiinvest wakidhani watarudisha mitaji yao kwa hela zetu au kwa vizawadi vya uwaziriHivi katika historia ya Tanzania, kuna Mbunge alishawahi kujiuzulu Ubunge ?
Kimbunga,
Mkuu afadhali wewe umeuliza. Nami nitakujibu kama ifuatavyo.
Vyote ulivyoandika hapo juu ni UONGO au VINAFANANA na ukweli lakini sio vya kweli KASORO kampuni inayolisha kwenye migodi miwili.
SF Holdings haimilikiwi na huyo Mbunge na SF Holdings (sijui mumeitoa WAPI!!!) Haimiliki Mr price wala kampuni ya kufuga kuku.
Ila ni kweli ana kampuni inayolisha migodi miwili tu.
Nadhani umeshaanza kuona mimi na Mizambwa nani ana data na nani anakurupuka humu.
Kwani alipogombea alidhani kuna nini huko?
Haya mkuu japokuwa najua hivyo nilivyoandika hapo juu. Lakini hii haikuwa theme ya hii thread basi naachana na hayo mambo ya makampuni.
Hapa battom line ni kwamba wabunge ambao ni wafanya biashara wamesikika wakipiga mayowe; nadhani walifikiri kwamba watajiongezea vipato huko bungeni kumbe huko wanaenda kuwatumikia watu. Tujue pia kwamba wafanya biashara wengi ni mean hivyo kuamka asubuhi na kukuta wapiga kura wapo milangoni na makapu ya shida naona kama imewaput off. Wengi wanalalama.
Mizambwa,
Nahisi wewe ni mwanaume. Kama u mwanaume sisi watanzania wanaume hatuna tabia ya UMBEA.
Ukiwa Mbea unaitwa mwanamke.
Natoa USD 1,000 mtu yeyote aende BRELA akaniambie S.F Holdings ni kampuni namba ngapi (usajili) maana NAAMINI na NAJUA hakuna kampuni inayoitwa S.F Holdings ambayo inamilikiwa na Huyo mbunge wa KIBAHA.
Kwahiyo basi nathibitisha hajaongeza mtaji kwa kisichokuwepo!
Ndugu yangu kama huyu Mbunge alikuacha pole sana mbembeleze akurudie inaelekea unampenda sana mpaka unamtungia UONGO
Mgamba Rostam alijiuzuluHivi katika historia ya Tanzania, kuna Mbunge alishawahi kujiuzulu Ubunge ?
Kwa sababu ya nyoka-mtu "aliyeonekana" kituo cha polisi Buguruni, na masanduku? UVUMI? hata Mpendazoe nasikia anajua ulikuwa uvumi ndiyo maana kwenye malalamiko yake, nasikia hilo la mtu kukamatwa na masanduku wala hajalilalamikia! Na yeye anawashangaa hao mashahidi wake wanaokomalia suala ambalo haliko kwa mahakamani! Pale hakuna kesi! Labda mjiandae kwa uchaguzi Ubungo na Arusha mjini.Mkuu hiyo ya Kibaha sijui, ila nina uhakika uchaguzi wa jimbo la Segerea unanukia kwa karibu sana!
Kuna uwezekano mkubwa wa kutangazwa nafasi wazi nafasi ya Ubunge ya Jimbo la Kibaha Mjini kufuatia kukinai kwa Mbunge aliyepo,Silvestry Koka-CCM.Mbunge huyo amekaririwa mara kwa mara akijuta kugombea na kupewa ushindi dhidi ya aliyekuwa mpinzani wake,Habib Mchange-CHADEMA.Koka anadai kuwa muda wa kusimamia biashara zake unakosekana na hivyo anapata hasara kubwa.
Sitajihusisha na swali la 'source' kwakuwa hamnijui siwajui...kila mtu humu JF ana wadhifa/nafasi yake hapa nchini.Mimi ni mpiga kura wa Ubungo ila naishi Kibaha.Kaeni chonjo..