Uchaguzi mdogo Magogoni: Matokeo

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,873
Jumla ya wapiga kura waliojiandikisha ni 5,494 na zilizopigwa ni 4,917.

Matokeo:

CCM: 2,874

CUF: 1,974

SAU: 22

Zilizobaki (47?) zimeharibika.
 
kama waliojiandikisha ni elfu 5 na ushe hivi, basi wakazi wa sehemu hiyo hawazidi 10,000 sana sana 20, 000. je hiyo idadi ya watu na gharama za kumuweka huyo mwakilishi/mbunge ni za busara? hizo fedha zingetumika kuwawekea shule nzuri tu na zahanati au hospitali, infwact hawa wakazi wangekuwa wanaishi kwenye hali iliyo bora
 
Sio ndio gharama za siasa hizo eti wenyewe wanaita demokrasia..Nikiangalia huko Busanda mambo ni yaleyale..Niliwahi kutoa wazo hapa ..waTZ tuachane kutumia rasilimali zetu haba kuitumikia siasa.
 
Mjadala ufungwe tena? Watu wanapaswa kuchambua kwanini upinzani ushindwe huko Zanzibar ilhali wananchi hasa wa Pemba wanasadikiwa kutokuipenda CCM. Je kuna mchezo mchafu au ni ushindani wa kawaida? Je wazanzibar wameanza kuichoka CUF kama wabara walivyoanza kuichoka CHADEMA? Je tuhuma kwamba CUF imekuwa ikiibiwa kura na CCM kwenye kila chaguzi kuu ni uzushi mtupu? Mjadala huu hauwezi kufungwa. Lazima tujiulize ni kwanini wananchi wanaonekana kukichoka chama tawala, ilhali inapokuja uchaguzi mdogo, basi CCM bado wanaendelea kushinda. Je wananchi ndio wanafiki? CCM ndio wanaiba kura?
 
Wananchi wengi bado wanaipenda CCM

Wasioipenda CCM ni wachache sana na wengi wao wanapatikana kama hapa JF.

Muda si mrefu watajitokeza kwenye thread hii.
 
Wananchi wengi bado wanaipenda CCM

Wasioipenda CCM ni wachache sana na wengi wao wanapatikana kama hapa JF.

Muda si mrefu watajitokeza kwenye thread hii.

Na mimi najitokeza kama mmoja ya wananchi wasioipenda CCM. I really hate CCM. Why? You know the reasons. Dont you? Cammon, we dont have to repeat every stuff daily here. Nashauri tu wananchi waache unafiki na waichukie CCM kikweli kweli.
 
Sasa huo ushauri unautoa kupitia hapa JF? Wananchi wanaoipenda CCM wengi wao hawaingii hapa JF, ni sisi wachache tu ndiyo tupo hapa JF.

I love CCM
 
Wananchi wengi bado wanaipenda CCM

Wasioipenda CCM ni wachache sana na wengi wao wanapatikana kama hapa JF.

Muda si mrefu watajitokeza kwenye thread hii.

Ndio unavyojidanganya na hao "mabwana" zako unaowatumikia kwa ufisadi..? Ngoja kuna siku mtavalia nguo zenu za ndani vichwani....
 
Hapana naona mnachangia bila kujua siri za siasa za Zanzibar, CUF ni pemba na CCM Unguja. Ingekuwa ni ushindi hasa kama CUF wangeshinda nje ya ngome yao. Kura za Zanzibar ni chuki na ukabila. Mpo. waambie CCM wajaribu Pemba kama waaambualia.

Busanda CCM wanashinda licha ya kuingia gharama kwa uteuzi wa mtu asiyeuzika kwa wapiga kura, ili linatokana na uroho wa upinzani, vinginevyo Helikopta ingefanya kazi.
 
Jimbo wapiga kura 5,000??

Mbona wacheche sana??

basi yawezekana 20% ya wakazi wa Visiwani ni wanasiasa au wanakula ktk siasa.

Angalia Dar ina watu 4-5 million na ina wabunge 7..yaani kila mbunge anawakilisha watu 600,000 hivi!
 
usianze mwenzio nna hasira.
 
Asalamu alaykum.

Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Magogoni umefanyika kwa usalama na amani na hakuna udanganyifu uliofanyika katika upigaji kura kwa ile jana tatizo kubwa lilikuwa wakati wa uandikishaji kuna watu wengi sana walikataliwa kuandikishwa kutokana na kutokuwa na vipande vya ukaazi ambavyo waratibu wa vipande hivyo ni viongozi wa serikali za mitaa (masheha) wanatuhumiwa kutoa vipande hivyo kwa ubaguzi mara nyingi hukataa kuwapa watu wenye asili ya pemba.

Tatizo jengine sio kama watu wamechoka na upinzani lakini kutokana na hali za maisha zilivyo ngumu wananchi wanachoka kukipa chama ambacho kila kinapotokea uchaguzi kinakoseshwa ushindi hivyo wananchi wengi wamekata tamaa lakini kubwa zaidi kuliko yote wananchi wengi hawana elimu ya uraia na hivyo wamekuwa wakitilia chama ambacho wanaamini hata kama hukukipa kitashinda tu kwani mara kadhaa viongozi wake wamesikika waksiema hawatoi nchi kwa kura kwa kuwa wamepindua.

lakini pia wananchi wengi hawajajitokeza kupiga kura kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo kuvunjika moyo, kuogopa kwa kuwa kila uchaguzi unaofanyika zanziabr huwa hauna salama lakini zaidi kazi ya kuihamasisha jamii haikuwa kubwa hivyo wananchi wengi wameona huu ni uchaguzi ambao hausaidii kitu katika kubadilisha utawala.

kila la kheri huo ni mtazamo wangu
 
Stone town,
Naona kama umevunjiaka moyo hivi kaka yangu,
Unamkumbuka marehemu babu alivyosema?
"IPO SIKU ITAKUWA KWELI"
Huu ni usia
Na mimi naongeza hakuna refu lisilokuwa na mwisho.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom