Uchaguzi mdogo katika majimbo ya Ludewa na Masasi

babumapunda

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
4,644
3,288
Uchaguzi katika majimbo haya unafanyika leo kuchagua Wabunge kufuatia kufariki kwa Wagombea wa nafasi ya Ubunge wa CCM Ludewa na NLD Masasi.

Masasi alifariki Dkt. Emmanuel Makaidi na kwa Ludewa alifariki Deo Haule Filikunjombe

Twende pamoja
========================
Update

CCM - 16597

CUF - 14069

CDM - 512 ACT - 347

NLD - 70

CCM YATETEA JIMBO LAKE LA MASASI KWA KURA 2528

=========================

UPDATE
Wakati CUF ilionekana kuongoza katika vituo vya awali kwenye uchaguzi wa ubunge Jimbo la Masasi, CCM imeonekana kuamba katika hatua hiyo katika uchaguzi mwingine kama huo Jimbo la Ludewa.

Matokeo ya awali Masasi

Kituo cha Machinjio namba 1 katika Kata ya Mkuti, CUF ilikuwa mbele kwa kura 187 dhidi ya 98 za CCM huku Chadema ikiwa na kura nne, ACT na NLD kura mojamoja. Kituo namba 2, CUF ilikuwa na kura 188, CCM 90, Chadema tatu na NLD moja. Kituo namba 3, CUF pia iliongoza kwa kura 184, CCM 102, Chadema moja. Kituo namba 4, CUF ilipata kura 178, CCM 91, NLD 21 na ACT 0.

Kituo cha Maji namba 1 katika Kata ya Napupa, CCM ilipata kura 37 na kuachwa mbali na CUF iliyopata kura 122. Kituo namba 2, ilipata kura CCM 73 huku CUF ikizoa kura 114. Katika Kituo cha Msufini namba 1, CCM iliibuka kidedea kwa kura 108, dhidi ya 77 za CUF. Kituo namba 3 CCM 78, CUF 101.

Matokeo katika Kata ya Nyasa, Kituo cha Hoteli Halmashauri namba 1, CCM 98, CUF 105, Kituo namba 2, CCM 94 na CUF 107.

Kituo cha Shule ya Masasi Sekondari Kata ya Migongo, CCM 84, CUF 118, ACT 2, Chadema 4 na NLD 0. Kituo cha Meff namba 1 Kata ya Jida, CCM 140, CUF 154, ACT 3, Chadema 0 na NLD 0. Kituo cha Jamhuri namba 1 Kata ya Jida CCM 85, ACT 2, CUF 145 na NLD 0.

Kituo cha Zahanati namba 1 Kata ya Jida CCM 105, CUF 107. Kituo cha Zahanati namba 2 CCM 105, CUF 107

Matokeo ya awali Ludewa

Wakati CUF ikitamba Masasi, Ludewa hali ilionekana kuwa ngumu kwa upinzani kwani matokeo katika Kituo cha Kijiji cha Ludewa Mjini A, CCM iliongoza kwa kura 152 huku Chadema ikifuatia kwa kura 57. Kituo cha Ludewa Mjini B, CCM ilipata kura 164, Chadema 43. Kituo cha Shule ya Msingi Kimbila A, CCM iliendelea kuiburuza Chadema kwa kupata kura 144 na Chadema 55. Shule ya Msingi Kimbila B, CCM 147 na Chadema 52.

Kituo cha Kilimahewa CCM 123, Chadema 23. Kituo cha Ligumbiro CCM 108, Chadema 17.

Wafuasi mbaroni

Awali, watu saba wanaodaiwa kuwa wafuasi wa CCM wanashikiliwa na polisi Njombe kwa tuhuma za kuwashambulia wafuasi watatu wa Chadema.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Wilbroad Mtafungwa alisema tukio hilo lilitokea juzi jioni saa moja usiku katika Kijiji cha Lugarawa, Ludewa.

Alisema tukio hilo lilitokea baada ya wafuasi wa Chadema kuwahoji wenzao wa CCM waliokuwa ndani ya gari, kuwa wanafanya nini katika eneo hilo usiku ndipo waliposhuka na kuanza kuwashambuli. Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema (Bavicha), Patrick Ole Sosopi alisema: "Tuliona hilo tukio ni kutaka kutuhamisha kwenye uchaguzi."

Katibu wa CCM Wilaya ya Ludewa, Lusiana Mbosa alisema hilo lilisababishwa na mgombea ubunge wa Chadema, Bathoromeo Msambichaka kufika Lugarawa kwa kile alichodai kuwa ni kutaka kuhujumu uchaguzi.

Akijibu madai hayo Msambichaka alisema: "Kama anasema mimi nilikuwa nataka kuhujumu uchaguzi, ungemuuliza muda huo wa saa mbili usiku jana (juzi) kulikuwa na uchaguzi gani unafanyika?"

Chanzo:
Mwananchi
 
Ukawa wameishiwa pumzi sidhani kama kuna kiongozi alikanyaga huko,lakini Arusha mafisadi wote walipiga kambi.
 
Ukawa wameishiwa pumzi sidhani kama kuna kiongozi alikanyaga huko,lakini Arusha mafisadi wote walipiga kambi.

Hapa masasi kundambanda tayari ni mbunge kupitia ukawa ccm chaaliiiiiii
 

Attachments

  • 1450587714831.jpg
    1450587714831.jpg
    67.8 KB · Views: 4,433
Ukawa wameishiwa pumzi sidhani kama kuna kiongozi alikanyaga huko,lakini Arusha mafisadi wote walipiga kambi.

Alikuja katibu wenu,akaja prezdaa mastaafu mwisho wa siku alionekana kona ya himo akila kona, Lema akawa mbunge, mafisadi wamebaki fisiem na wengine wameteuliwa kuwa mawaziri, rais wenu,sera za ukawa:D
 
Masasi ilipaswa kipindi kile cha mabadilikooooo!!
Ila sasa pepo la Magufuli linawaendeshaa wananchi
 
Jibu wewe unaye ona mimi sipo sahihi,ccm kusini imeshafutika jamani

Swali nakuuliza wewe unataka nijibu mimi muuliza swali? Mimi nilidhani unalijua anguko la ccm huko kusini utufahamishe ili tuoanishe na maneno yako kama yanauhalisia
 
Swali nakuuliza wewe unataka nijibu mimi muuliza swali? Mimi nilidhani unalijua anguko la ccm huko kusini utufahamishe ili tuoanishe na maneno yako kama yanauhalisia

Ccm kusini ndiyo bye byeeeeeeeeee
 
Mtwara mjini-cuf
Tandahimba-cuf
Liwale-cuf
Mchinga-cuf
Kilwa kusini-cuf
Kilwa kaskazini-cuf
Masasi-cuf
Ndanda-chadema
Nanyamba-mgombea cuf alihongwa akajitoa
Newala-waliiba
Mtama-waliiba
Lindi-waliiba
 
Mtwara mjini-cuf
Tandahimba-cuf
Liwale-cuf
Mchinga-cuf
Kilwa kusini-cuf
Kilwa kaskazini-cuf
Masasi-cuf
Ndanda-chadema
Nanyamba-mgombea cuf alihongwa akajitoa
Newala-waliiba
Mtama-waliiba
Lindi-waliiba

Unge muwacha huyo ngiri maana hana faida
 
Hali Masasi haitabiriki ila watu wamejitokeza kwa wingi kupiga kura ila sintofahamu iliopo ni uoga kwa kila RAIA baada ya kuwa na vifaru na magari ya deraya takribani matano na cruiser za field kutoka Lindi na MTWARA sasa haieleweki kunani hapa masasi
 
Back
Top Bottom