Kwa Sanders mbaya zaidi ni kwamba pamoja na kushinda Rhode Island kwa asilimia 56% dhidi ya Clinton 44%, katika jumla ya wajumbe 33, Clinton kazoa wajumbe 20 na Sanders 13 tu. Hii ni kutokana na uwiano unaojumuisha wajumbe wanaotambulika kama pledged delegates.Mkuu Mag3
Katika hali ya kuzooeleka miaka ya karibuni, wagombea hufikia ''threshold' ya at least 30% ya kupata ugombea kabla ya kuelekea New York Primary. Kwamba front runner anaonekana wazi
Kama utakumbuka, tulisema uwezekano wa Republican kwenda convention ni inevitable
Wachambuzi wote wa siasa za ndani na nje waliona hilo wazi
Kilichosukuma hitimisho ni ukweli kuwa Trump alishinda chini ya 50% sehemu nyingi
Uwepo wa wagombea watatu, haukuweza kumpa mgombea yoyote 45-55%
Ushindi mfululizo wa Cruz na na kuchomoza kwa Kasich ilikuwa dhahiri RNC haiepukiki
Kwa Democrat, Sanders kushinda caucus 7 mfululizo na majimbo 8 kati 9 kulionyesha ni mapema mno kuhitisha majaaliwa ya Bi. Clinton.
Uwezo wa kukusanya makundi ya watu na nguvu ya kampeni yake kwa kona zote, kuchangisha pesa, kushambulia, hoja n.k. ilikuwa ngumu kufikia hitimisho
Hesabu zote zilionyesha Clinton kuongoza, muda haukuwa na nafasi.
Michigan ili define mweleko wa uchaguzi ikimshtua Clinton na kumpa nguvu Sanders
Ilifahamika, ukubwa wa New York, Pennyslavania, Maryland, Connecticut ungetoa picha kubwa. Haikuwa makosa kufikiri hivyo.Picha imebadili mtazamokwa pande zote
Kilichobadilika:
NY iliwapa ushindi mnono Trump na Clinton na kubadili mwelekeo.
Matokeo ya jana yamehitisha matarajio yaliyokuwepo kuhusu wawili hao
Matarajio yamebadili sana uwezekano wa kwenda Convention kwa RNC.
Trump akiwa na wenzake wawili amewashinda kwa asilimia hadi 60.
Huko nyuma, ilibidi Trump ashinde kwa 58% majimbo yote ili kupata 1237.
Kwasasa inawezekana. Kashinda hadi 63 kwanini idhaniwehaitawezekana?
Clinton aliongoza kwa wajumbe kuanzia mwanzo, wawe pledge au super delegates.
Kasi ya Sanders ilionekana kumsimisha kwa muda. Naye kama Trump , NY, Pa, Md, Conn na delaware kumepanua pengo kati yake na Sanders.
Ili kumuzia, Sanders anahitaji 85% ya ushindi katika majimbo yote, jambo gumu sana
Trump na Clinton wanaelekea November kama hakutatokea miujiza mingine
Tusemzane
Ukiangalia hesabu, ushindi wa Sanders Washington state, Idaho, Utah na Wisconsin umefutwa na idadi ya wajumbe wa New York, na PennyKwa Sanders mbaya zaidi ni kwamba pamoja na kushinda Rhode Island kwa asilimia 56% dhidi ya Clinton 44%, katika jumla ya wajumbe 33, Clinton kazoa wajumbe 20 na Sanders 13 tu. Hii ni kutokana na uwiano unaojumuisha wajumbe wanaotambulika kama pledged delegates.
Update..hii hapa chini ndiyo idadi ya wajumbe wa kila mgombea hadi leo tarehe 29/4/2016;SANDERS
Wakati timbwili la Trump likifunika anga za habari, Senata Sanders ametangaza kupunguza wafanyakazi wa kampeni yake.
Hili linazua maswali endapo Sanders sasa ameamua kuachia ngazi.
Akiwa Indiana Sanders amesisitiza bado anagombea kupata kuteuliwa
Pengine kwa kujua huenda asiwe mgombea,ameamua kupunguza wafanyakazi ambao
Ni ngumu kujua wapi anasimamia na nini lengo lake la mwisho
Haionekani kama amekata tamaa na kuna sababu za kuamini kipo anachokitafuta
Pengine uchaguzi wa Indiana utatoa jibu sahihi kuhusu kuendelea au kutoendelea na kampeni. Na pengine ni dalili za awali za kuondoka katika shindano. Haiujulikana kiuhalisia
HOTUBA YA TRUMP: MAMBO YA NJE , ULINZI NA USALAMA
Ulinzi na usalama imekuwa agenda kubwa kwa Republican kwa miaka mingi
Matarajio ya GOP ni mbeba bendera kuiendeleza sera hiyo kama ilivyo desturi
Dunia inabadilika kila uchao, changamoto nazo zinabadilika.
Ni makosa kudhani ulinzi na usalama unahitaji silaha tu.
Kuna suala la uchumi na washirika kwasababu vyote vinaambatana
Katika jitihada za kuua mjadala wa wanawake, Trump alitoa hotuba kwa kutumia teleprompter.Huko nyuma aliponda matumizi ya chombo hicho kama udhaifu wa kujieleza
Inaonekana alishauriwa kuhusu unyeti wa suala hilo na kwamba si la kuzungumza tu
Hotuba yake imepokelewa kwa hisia tofauti, wachunguzi na wataalamu wa siasa za nje wanaiona kama 'incoherent' inachanganya na haieleweki.
Inajichanganya kutoka sentesnsi moja hadi nyingine.
SenataLindsey Graham ambaye ni miongoni mwa Magwiji wa GOP ameiponda vilivyo.
Ndivyo alivyoichambua nguli wa habari za kimataifa Farid Zakharia
Kwa ufupi hotuba ya Trump haionyeshi weledi au ufahamu wa anachozungumzia.
Kibaya zaidi, hoja zake za siku za nyuma zinapingana na anachosema sasa
Hilo limemweka mahali pagumu hasa kwa GOP na ndiyo maana jitihada za 'kuzuia' asifikie 1237 zinaendelea kwa kasi.
Ikiwa, Republican watakwenda RNC, mzunguko wa kwanza ukashindwa kupata mgombea, Trump atakuwa katika wakati mgumu mzunguko wa pili au tatu
Tusemezane
Nakushukuru mkuu Nguruvi3 pamoja na kukuulizia pm lkn uliheshimu mawazo yangu na kunipa kile nilichotaka kufahamu. Ushauri wako pia niliuzingatia na kwa sasa tupo pamoja. Naendelea kukufuatilia ntarudi..!Mkuu magode kwa idhini uliyotoa tutafafanua kuhusu hoja uliyoniuliza pembeni.
Magode anauliza mbona tunazungumzia sana Democrat kuliko Republican katika mabandiko?
Mkuu, tunaangalia pande zote sawa, kama ukifuatilia toka mwanzo
Hata hivyo, kuna sehemu ambazo kina cha mjadala wa Republican hakifikiwi kutokana na sababu mbali mbali
1. Hali ya Republican katika mijadala ni ya ukakasi.
Wagombea walijikita katika personal issues and attacks badala ya hoja.
Inakuwa si kwa public interest kujadili urefu wa vidole vya Trump au ufupi wa Marco Rubio. Tofauti na hivyo, Democrat wana afadhali hadi siku za karibuni
2. Kuna maeneo mengine yanachanganya kuhusu Republican na hivyo yanaelezwa kwa ufupi ili kuelewaeka kwa urahisi zaidi badala ya kuwachanganya wasomaji
Mfano, tangu mwanzo tumezungumzia namba 1237 kama mstari wa mwisho wa mshindi kuufikia. Lakini ndani ya 1237 kuna kanuni( formula) nyingi sana ambazo si rahisi kuzieleza kwa lugha nyepesi bila kuwachanganya wasomaji.
Ndio maana tulieleza maana ya winner take all, winner take most na mgawanyo wa congressional districts, state convention, Caucus n.k.
Mfano, juzi Pennyslavania , haikuwa rahisi kupata namba ya wajumbe kwasababu katika wajumbe 95 , wapo 54 wasiotengwa kwa mgombea yoyote.
Yapo majimbo mgombea anapata wajumbe kutokana na kura za Urais za 2012
Yapo majimbo anachaguliwa na state convention kwa mgawanyo maalumu n.k.
Kwa mifano hiyo, ni ngumu kupata namba za mwisho hadi zitakapotolewa na RNC
Tofauti kidogo ni Democrat mtiririko wao wa uwiano ni rahisi ukilinganisha na GOP
Kuhusu siasa napo kuna tofauti kubwa na hapo ndipo panapozua ukina wa eneo moja ukilinganisha na jingine
Tuseme kuwa tunazungumzia pande zote kwa usawa na hakika Republican wamechukua sehemu kubwa ya mjadala kutokana na hali ya mambo ilivyo
Nguruvi3, tukiachana na swala la wajumbe, mpaka sasa, hizi ndizo idadi ya kura walizopata hawa wagombea kwenye caucuses na primaries katika majimbo yaliyokwisha kupiga kura;SENETA SANDERS KASEMA NINI LEO?
Seneta Sanders amesema ' Suala la super delegates liangaliwe,kwamba wanapaswa kufuata matakwa ya wananchi. Kwa maana hiyo Bi Clinton hana namba ya wajumbe wa kuchaguliwa(2383) bila super delegates, na kwamba wakifuata matakwa ya wananchi, hatafaikia namba hiyo na jibu ni kwenda mkutano mkuu kwa contested convention ''
Haya ni maneno ya Sanders kama tulivyowahi kueleza mabandiko mengi ya nyuma.
Kwa ufupi anachosema Sanders tumekileza bandiko #122
Baada ya NY (Bandiko 103) tulisema hoja ya Sanders kushinda majimbo 7 tena yakiwa ya Caucus ndogo ililenga kubadilisha msimamo wa SD.
Alitamka wazi super delegates waanze kumuunga mkono.
Tukaeleza NY ita define mweleko, na ndivyo ilivyokuwa.
Ushindi wa point 15 NY wa Clinton ulizima kabisa uwezekano wa kuvuna wajumbe.
Mambo yalimwende kombo Sanders Pennsylvania, Maryland, Connecticut na Delare ambapo kwa usiku mmoja alipoteza majimbo makubwa 4 kwa pointi Zaidi ya wo.
Hesabu zikionyesha njia imefungwa kwa Sanders
Tulisema haja ya Sanders kubaki katika uchaguzi ni kutafuta njia za kupeleka uchaguzi mkuu kama kauli za kampeni meneja wake zilivyoashiria(Bandiko 10).
Mag3 akaonyesha hofu waliyo nayo Democrat kutokana na mwenendo wa Sanders (# 113).
Tuksema hali ilipofikia Democrat wana hofu yasije wakuta ya Republican (#111) n.k.
Kauli ya leo ya Bwana Sanders inaeleza umuhimu mkubwa kwa Clinton kampeni kuendelea na kasi ili kukabiliana naye.
Sanders ameshindwa kushawishi wapiga kura na super delegates kwa njia za kura na maoni kama ilivyo katika kanuni za uchaguzi za Democrat
Sanders anachofanya sasa hivi ni kile kile tulichosema
1. Kutaka super Delegates wasiwe sehemu ya mchakato ili Bi Clinton asipate 2383 na kulazimisha kwenda mkutano mkuu wa DNC Philadephia
2. Akifanikiwa hilo kwa maoni yake, atatumia formula ya Republican.
Rejea mabandiko matatu nyuma utaona Super Delegates wa Republican wanafungwa kumchagua mgombea kutokana na ushindi. Super Delegates wa Democrat wapo huru
Hapa Sanders anataka Democrat watumie formula ya Republican.
Kwamba SD wapige kura kutokana na matokeo ya majimboni.
Kwa maana mbili, atakuwa amezuia 2383 ya Clinton, na pili ataanza kampeni ndani ya mkutano mkuu na kuzua kizaa zaa ndani ya Democrat
Mpango wa Sanders una matatizo makuu mawili
1. Kwanza, itawalizimu Democrat wabadili kanuni ili kukidhi haja yake
2. Kutaendelea kugawa chama wakati wa uchaguzi mkuu
Kwanini Sanders hatafanikiwa kwa mpango wake?
Inafuata
Mkuu hapa ndipo tunafika katika hoja ya 'kwanini Sanders hatafanikiwa'Nguruvi3, tukiachana na swala la wajumbe, mpaka sasa, hizi ndizo idadi ya kura walizopata hawa wagombea kwenye caucuses na primaries katika majimbo yaliyokwisha kupiga kura;
Mpaka hapo tu Clinton anamzidi Sanders kwa kura 3,167,708! Wakati huo huo Clinton anamzidi Sanders kwa wajumbe zaidi ya 800 pamoja na SD. Hali hii imewaacha Democrats njia panda wakijiuliza ni kitu gani anataka Sanders.
- Hillary Clinton.....12,135,109
- Bernie Sanders..... 8,967,401
Hata hivyo wanasita kumtibua kwa wakati huu kwa sababu kwa kufanya hivyo chama kitayumbishwa wakati wanataka umoja udumishwe. Hata Clinton mwenyewe amejizuia kumshambulia Sanders kwa hofu hiyo hiyo ya kupoteza mashabiki na wapenzi wake.
Hata hivyo dalili zinaanza kujitokeza za uvumilivu kufikia mwisho kwani kila siku Sanders anazua jambo jipya na mengi ya matamshi yake hayasaidii chama. Matamshi ya wapenzi wake nayo yanazidi kukoleza mambo na hasa wale ambao wazi wazi wanasema hawatampa Clinton kura zao akiwa ndiye mgombea.
Hilo moja lakini la pili ni kwamba mgombea wa GOP anayeongoza, Donald Trump, anaonekana kuchangamkia hoja za Sanders na anapanga kutumia mashambulizi hayo hayo dhidi ya Clinton.
Hebu turudi nyuma kigodo hadi mwaka 2008 Hillary alipojitoa na kumuunga mkono Obama, je mambo yalikuwaje?Nimewasikia baadhi ya pundits wa Dem, inaelekea wamechoka na haya ya Sanders
Namuona Trump akipenya aisee...TRUMP ASHINDA INDIANA
SENETA TED CRUZ AACHIA NGAZI
Trump ameachia ngazi (suspended his campaign)
Democrat bado matokeo ya mwisho hata hvyo inaelekea Sanders atashinda
Tutaendelea na tahmini hasa tukiangalia nini kinafuata GOP ambako Trump sasa ni ''Mgombea' wa GOP