Uchaguzi huu uwe fundisho kwa wasimamia sheria

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
4,086
6,568
Nimemsikiliza kwa makini H Polepole, amelalamika sana juu ya wanaCcm kufanyiwa ukatili na unyama. Mmoja ameuwawa Songwe na mwingine Mkoani Njombe. Kwa nchi tuliozoea kuishi kwa amani hii sio jambo jema. Na linatia hofu kwa wananchi.

Pia kupigwa mapanga kwa wafuasi na wanachama wa CCM huko Unguja na Pemba sio jambo jema. Lakini law enforcement agencies hasa Dpp na Police,wawe na msimamo kushughulikia kesi kama hizi, sio mpaka mwana Ccm apate majanga ndio tuone Dpp anachukua hatua ndani ya siku mbili.

Polepole kama ukizunguka mikoani Tanzania nzima utakuta wananchi ambao ofisi za waendesha mashitaka za mikoa zinawazungusha wananchi kupata haki zao,hata kama ndugu zao wameuwawa au kujeruhiwa. Kwa hiyo Humphrey Pole pole unapozungumzia haki kwa wana Ccm wanaopigwa mapanga tambua kuna wanaCuf,wanaAct,wanaCdm na wanaChauma ambao pia ni wahanga wa kukosa haki.
 
CCM wanauana na kukatana mapanga wenyewe...

Hakuna amani bila haki.....Watu walichaguliwa kwenye nafasi mbalimbali za kugombea, from no where anasikia jina lake limekatwa kawekwa mtu aliyeshika nafasi ya tano....maana yake.amepokonywa haki yake....Kamwe hakutakuwa na amani

Wacha wakatane na kuuana
 
Mkuki kwa nguruwe! Wasituchoshe na upuuzi wao kwa hiyo wenye damu ni ccm tu,huu uchaguzi uishe tu tupumzike
 
Back
Top Bottom