Uchaguzi huru na haki maana yake nini?

Mchakato uwe wazi na huru toka hatua ya kwanza ya uchaguzi.

Ila haitawezekana kuwepo kwa tume iliyohuru kwa kila Mtanzania. Kikubwa wengi wakiulizwa je tume ni huru! Kutoka miyoni mwao wakiri ndiyo ni ya haki na huru.
 
Uchaguzi huru na wa haki ni ule utakao toa ushindi kwetu sisi wafuasi wa chama kile kinachopinga kila kitu
 
Maana yake ni
1. Vyama vyote viruhusiwe kupiga kampeni bila bughudha.

2. Vyombo vya habari visiwe na upendeleo ktk kipindi chote cha uchaguzi.

3. Wapiga kura wote waliosajiliwa waruhusiwe kupiga kura bila kufanya ujanja wowote wa kuwakosesha haki yao.

4. Waangalizi mbalimbali wa uchaguzi waruhusiwe.

5. Vyombo vya dola vitekeleze wajibu wao kwa vyama vyote kwa usawa bila upendeleo.

6. Tume ya uchaguzi iwe huru na isiingiliwe.

7. Sheria za uchaguzi zitende haki kwa wagombea na vyama vyote.

8. Muda wa ufunguzi na ufungaji vituo vya kura uzingatiwe, ikitokea imechelewa eneo fulani basi muda ufidiwe.

9. Muda wa rufaa na haki ya rufaa izingatiwe.

10. Matokeo yahakikiwe na kuridhiwa na pande zote kabla ya kuyatoa kwa umma.

11.......................................

Narudi
 
Back
Top Bottom