Richard mtao
JF-Expert Member
- May 13, 2018
- 271
- 378
Kwasasa mikoa yote Tanzania na wilaya zake chaguzi kwa nafasi tofauti tofauti zinaendelea kama ambavyo anavyopaswa kufanyika.
Lakini kuna kitu hakipo sawa kwa baadhi ya wanachama wanao wania hizi nafasi, hapa najikita sana katika chaguzi za viongozi katika jumuiya ya umoja wa vijana.
Viongozi walioachia nafasi hizo wengi wamerudia kuwania nafasi hizo bila kujali maelekezo ya chama ya umri wa mgombea na hata katiba ya umoja wa vijana Ccm.
Kwa maeneo mengi wagombea hao wamekatwa kwakua wamekiuka maelekezo pamoja na katika, lakini cha ajabu baada ya kufutwa katika kinyang'anyiro hicho bado wameomba kuteuliwa kugombea nafasi zingine kama ujumbe katika nafasi tofauti tofauti na bado chama kimewapa idhini hiyo.
Hofu yangu.
Viongozi hawa wastaafu ambao bado wanauchu na madaraka kwa kiasi icho ni tatizo kubwa kwa chama kama viongozi wataangalia kwa makini.
Jiulize kwanini hataki kuachia nafasi watu wengine? ili wao pia waweze kuonesha uwezo wao na kujifunza zaidi namna ya uongozi ili siku za usoni tuweze kuwa na vijana wengi wenye utashi na weledi mkubwa katika maswala ya uongozi na siasa.
Chaajabu bado chama kinaendelea kuwaweka katika nafasi zingine na kuendlea kuficha uwezo wa vijana wengine ambao nafasi zao ni kama zimepokonywa.
Kama kuna mtu nimemkwaza naomba radhi.