Hakuna mtu atatoka ccm akomboe taifa. Wote wameshirikiana kuliua taifa. Hakuna mwenye dhamira safi wala uwezo wa kuiponya nchi kwa sababu kinachoongoza ni mfumo. Huyo kiongozi wa ccm analazimika kulinda maslahi na itikadi za ccm ambazo ni kuteteana , kulindana, ufisadi, uwongo, hadaa, udanganyifu, wizi na uonevu kwa Watanzania kwa kulinda chama chao na wanachama chao. Angalia Green Guards, wamefanya madhara mangapi, nani kasimama n akuwakemea ziadi ya kuamrisha jeshi la polisi liwalinde?
Uharamia wote dhiid ya taifa wameufanya pamoja, nani kati ya hao unaowaita hawawezi kupelekshwa alisimama kukemea? Msidanganyikie.
Ccm kama kuna mtu wamemwacha, si kwamba atakisaliti chama na itikadi zao. Mfano Lowasa ni fisadi nambari moja, jizi na danganyifu kuliko wana ccm wote. Limeutibia fedha zetu kwa mikataba na makampuni fake ya Richmond, hadi leo limegoma eti haliijui Richmond. Hili ndio dude la kulipa nchi?
Kama ccm wameyaacha mafisadi mengine, si kwa sababu yangesalisti chama kwa sababu mfumo huo ndio yanaupenda kwa manufaaa ya yenyewe na mafirauni. Ispokuwa ni kwa kuwa wameyaona yataanza kuwalipizia visasi kwa tofauti zao binafsi ili kukomoana lakini si kwa sababu yana uchungu na taifa. Yatalipizana visasi kwa makosa waliyofanyiana binafsi kwenye migawo yao ya kifisadi lakini si kwa maslahi ya taifa. Na malipizano ya visasi hivyo, kamwe yasingekuwa na maslahi ya taifa, zaidi ya kuimarisha mifumo ya kifisaid.
Wanyama pori wanapogombana na kuuana, si kwamba mmoja wao atakuwa anatetea binadamu au mashamba ya watu yasiharibiwe. Ccm hata kama wengekosana, watapigana na kukomoana wao kwa wao lakini kamwe si kwa sababu mmoja kawa na uchungu na nchi kwa sababu wananchi ndilo shamba lao la misukule. Ugomvi wao kwa lugha nyingine ni kaika mgawanyo wa maslahi na fursa miongozi mwao lakini haina maana wanaacha kuwafisadia Wananchi.
Ccm ni kkundi la mafisadi no matter what, na halifai kuongoza nch iyetu.
Wtanzania tunapiga kura kuanzia Raisi, Mbunge, hadi Diwani kutoka UKaWA, tujenge nchi yetu kwa mfum mpya.
Hata yeye ataendeshwa tu,
Ndo maana wanaogopa kuwakubali baadhi ya waomgombea kwa kuwa wanafahamu fika si rahisi kupelekeshwa.