GE2025 Uchaguzi bila CHADEMA, ni Uchaguzi mfu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Andromeda Galaxy

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2025
Posts
5,369
Reaction score
6,878
Nimejaribu kuangalia mijadala ya wagombea wa Chama Chaumma(CHAUMMA), CUF, na AAFP, nikiri kuwa ukosefu wa Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo (CHADEMA), kumefanya uchaguzi wa mwaka huu kuwa Moja ya chaguzi za hovyo tangu mfumo wa vyama vingi uanzishwe,

Nakiri kuwa Tundu Antipas Lissu na John Wegesa Heche ni miongoni mwa wanasiasa wenye hoja mtambuka zenye kugusa maisha ya wananchi na pengine ni wagombea wenye ushawishi zaidi ambao kwa kukosa kwetu demokrasia madhubuti basi tumekosa michango yao madhubuti na jadidifu kuelekea uchaguzi ambao pengine ni uchaguzi wa hovyo zaidi kuwahi kutokea tangu mfumo wa vyama vingi uingie nchini Tanzania

Kwa kweli ni huzuni kubwa kwa taifa letu changa la Tanzania.
 
Yaani Yanga anaingia uwanjani bila Simba
FB_IMG_1756663995199.jpg
 
Yaani kwa jinsi nilivyopuuza hizi chaguzi za kishenzi, hata muda wa kufuatilia hizo kampeni sina. Ni kampeni zinaowagusa wanaccm tu, maana hata vyama vingine vinavyoshiriki ni matawi yake.
Tindo, kwa kweli huu ni uchaguzi wa hovyo kabisa , yaani kama Lissu angekuwepo at least tungefurahia kampeni za uchaguzi tofauti ilivyo hivi sasa
 
Mm sio chadema wala sio ccm, tatizo lenu watu wa JF mnataka kila mtu aongee mnayotaka kuyasikia.
Ndugu yangu Mbaga,kwani huoni uovu na ukiukwaji wa kanuni za kidemokrasia na kikatiba kutoka CCM, ukiacha unafki na uongo CCM wanatawala kimabavu na sio jambo la msingi kwenye utawala wa kidemokrasia, CHADEMA ni wahanga wa kidemokrasia
 
Tatizo lenu tukiwachana ccm Hua mnasoma na kupita kimya kimya ila tukiwachana chadema ndo inawauma sana hadi mnakariri watu.
Tulia.
 
Lini umewachana ccm ndugu Mbaga Jr? Shusha Uzi wako ukiwachana ccm
 
Nimejaribu kuangalia mijadala ya wagombea wa Chama Chaumma(CHAUMMA), CUF, na AAFP, nikiri kuwa ukosefu wa Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo (CHADEMA), kumefanya uchaguzi wa mwaka huu kuwa Moja ya chaguzi za hovyo tangu mfumo wa vyama vingi uanzishwe,

Nakiri kuwa Tundu Antipas Lissu na John Wegesa Heche ni miongoni mwa wanasiasa wenye hoja mtambuka zenye kugusa maisha ya wananchi na pengine ni wagombea wenye ushawishi zaidi ambao kwa kukosa kwetu demokrasia madhubuti basi tumekosa michango yao madhubuti na jadidifu kuelekea uchaguzi ambao pengine ni uchaguzi wa hovyo zaidi kuwahi kutokea tangu mfumo wa vyama vingi uingie nchini Tanzania

Kwa kweli ni huzuni kubwa kwa taifa letu changa la Tanzania.
Hakuna uchaguzi
 
Back
Top Bottom