Uchaguzi 2020 Uchaguzi 2020: Tunahitaji Serikali Jumuishi

Mohamed Abubakar

JF-Expert Member
Jun 26, 2014
512
638
Tukijilinganisha sisi na wakenya ktk maeneo mengi tunakuta wakenya wametutangulia kwa kuonyesha dhamira njema katika kila jambo.

Mathalan tukilinganisha katiba ya Kenya na ya Tanzania utagundua dhamira njema iliopo katik katiba ya Kenya katika kuwaunganisha raia wake. Huku ya ya Tanzania yaonyesha unyonge na udhaifu mkubwa. Na ukifanyia tafiti kuangalia uhalisia tutaona kama vile wale tuliowapa mamlaka hawako tayari hata kulijadili mapungufu haya kupitia sheria mama, zaidi ya maneno matupu jukwaani.

Hali hizi ndizo zilizokatisha tamaa watz wengi hata kupoteza mwamko wa kupiga kura. Tunahitaji chama kitachoweza kurudisha ari ya wapiga kura kwa kuonyesha nia ya dhati ya kubadili aina hizi za ubaguzi na unyanyapaa.

Vipengele vinavyoelezea kuwaunganisha watanzania kwenye katiba ya Tz vilivyotajwa havizidi 5 ukilinganisha na ya Kenya vimetajwa zaidi ya Mara 18.

Tujiulize:

Kwanini ktk awamu zote zilizopita hakuna teuzi zilizotokea ambapo watz wenye asili ya Asia, Arabuni kuliteuliwa ktk nafasi za wafanya maamuzi?

Tujiulize Tena kwanini baadhi ya Watanzani wasiofata ustaarabu wa kizungu mfano; ktk majina, dini wahazidi 8% ktk teuzi.

Jibu rahisi kwa mtz wa kawaida ni kuwa katiba yetu haijatoa nafasi ya kuwaunganisha watz bila kujali rangi, dini,, kabila, jinsia nk.

Tunahitaji chama mbadala zaidi ya kuleta ngonjera za kila wakati wa uchaguzi kujinadi kujenga barabara, mahospitali nk, Bali chama kitakachorudi chini zaidi na kuangalia misingi ya kibaguzi na kuweka misingi imara ya kuwaunganisha.

Nimelizie kwa kuweka mifano iliopo ndani ya katiba ya Kenya ineyoonyesha dhamira njema ya kuwaunganisha wakenya. Kama vile.

1. Nafasi za wafanya maamuzi (executives) ni lazima ziwe jumuishi wenye uwiano kwa matabaka Pasi na ubaguzi wa aina yoyote au fadhila ya rais kumteua amtakae.

2. Nafasi za majeshi yote ni lazima wawe jumuishi kwenye uwiano wa matabaka yote nk

Kwa haya naanini kwa dhati ya moyo kuwa CCM ilishindwa, imeshindwa na haitoweza kubadili matakwa haya ya kikatiba. Kwani kwa mpiga kura kutopiga kura kwao ni fursa.

Screenshot_20200529-150207_1590911517616.jpg
Screenshot_20200530-213624_1590911329120.jpg
Screenshot_20200530-213703_1590911281585.jpg
Screenshot_20200530-213720_1590911229612.jpg
Screenshot_20200530-213755_1590911191295.jpg
Screenshot_20200530-213650_1590911036517.jpg
Screenshot_20200530-213929_1590911144881.jpg
Screenshot_20200530-213650_1590911036517.jpg
Screenshot_20200530-213542_1590910962912.jpg
Screenshot_20200530-213105_1590910882309.jpg
Screenshot_20200530-213028_1590910826914.jpg
 
Wakashirikiane na Mabeberu. Tanzania haiwezi kushirikiana na vijakazi wa mabeberu

Hebu CCM jibuni hoja. Kwann tabaka hizi nilizozitaja wanatengwa. Ikiwa katiba iliopo inasema haibagui kwanini hatuoni watanzania wenye asili ya Asia wakipata teuzi za executives.
 
Kuna Nchi yeyote Asia iliwahi kumthamini mtu mweusi?
Ccm INA jeuri iliyopitiliza. Kweli maneno hata ya kibaguzi yanaweza kutoka kwa mfuasi anayetegemewa kwenye mitandao.
Kama unawezawa kuwabagua watz kwa misingi ya rangi zao nani anaweza kusalimika na ubaguzi huu.

Sitaki kukuliza kwa watz wenye asili ya uarabu.

Sotokuuliza kwa waislam ambao licha ya uwimgi wao, na wengi kutokuwa na ajira ingawa ni weledi lkn ktk teuzi wanapata chini ya 8%. Sijui hapa utajibu vp
 
Kumbe Unataka kuleta hoja za udini, sorry rafiki hiyo haina nafasi kwangu
Ccm INA jeuri iliyopitiliza. Kweli maneno hata ya kibaguzi yanaweza kutoka kwa mfuasi anayetegemewa kwenye mitandao.
Kama unawezawa kuwabagua watz kwa misingi ya rangi zao nani anaweza kusalimika na ubaguzi huu.

Sitaki kukuliza kwa watz wenye asili ya uarabu.

Sotokuuliza kwa waislam ambao licha ya uwimgi wao, na wengi kutokuwa na ajira ingawa ni weledi lkn ktk teuzi wanapata chini ya 8%. Sijui hapa utajibu vp
 
Mwaka huu hakuna chama CHA upinzani dume kinacho weza kuitoa jasho chama tawala,
 
Kumbe Unataka kuleta hoja za udini, sorry rafiki hiyo haina nafasi kwangu
Sasa kosa ni nini?!?!? Kosa ni dini, kosa ni udini.....

Na kama kosa si dini ya mtu bali ni udini..... katiba yetu inasemaje?!?!? ....naa Ccm inafanya nini ktk teuzi
 
tutaendelea kua taifa la kifala kama utawala wa CCM utaendelea na hakuna wanachoweza kubadili narudia hakuna.. tutapiga mark time mpaka basi.
 
Tunajadili katiba na dhamira ya vyama ktk kuwaunganisha watz.

Suala la nani ana ubavu au hana ni topic ingine.

Kwani ubavu tulionao sisima ni kukataaa kubadili vipengele vya sheria za uchaguzi ili kupata tume huru.

Hata hivyo tume huru sio tatizo la watz, watz wanahutaji dhamira ya dhati ya kuondoa ubaguzi wa aina yyt

Mwaka huu hakuna chama CHA upinzani dume kinacho weza kuitoa jasho chama tawala,
 
-1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom