Uchaguzi 2020 Uchaguzi 2020, Rai kwa wagombea

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,363
12,708
Kila kitu kinachosemwa na kufanywa na wanasiasa katika kipindi hiki Cha uchaguzi faida na hasara itakwenda kwa wananchi wa kawaida, hivyo wanasiasa tuchunge ndimi zenu na vitendo vyenu kwenye majukwaa.

Kwa vyovyote vile sisi wananchi tunapenda kusikia wagombea wakisema namna watakavyotupatia haya kama tukiwachagua:

1. Usalama na amani
2. Maji ya kunywa na umwagiliaji.
3. Afya kwa wote
4. Elimu kwa wote
5. Chakula kwa wote
6. Umeme kwa wote
7. Uchumi wa majumbani sio wa takwimu
8. Miundombinu ya Usafiri na usafirishaji
9. Utawala wa sheria
10. Utengamano na nchi jirani na kimataifa.
11. Uboreshaji wa Michezo na Sanaa.
12. Utunzaji wa mazingira na ukuzaji wa utalii

Wananchi tungependa kuwasikia mnasema Nini kuhusu mtakavyotupatia vitu hivyo kwa njia bora zitakazozingatia utu wetu, uhai wetu, mila zetu, utamaduni wetu, Uhuru wetu, muungano wetu, na demokrasia yetu bila kuwasahau nchi majirani.

Hatuhitaji kusikia Sera za kutaja na kulaumu watu, vyama, na taasisi mbalimbali.

Mwanasiasa atakaefanya siasa za maji taka bila shaka atashindwa uchaguzi kabla ya uchaguzi haujafanyika
 
CHADEMA itashinda kwani wananchi kwa kweli wamechoshwa na yanayoendelea sasa, hali ya uchumi imekuwa ngumu sana.
 
Hayo yote Magu na Ccm yake waliyahubiri 2015,lakini hakuna alipofikia lengo,mambo ni mbofumbofu,Utasema usalama na amani,hakuna kitu zaidi yakutishana nakupeana taharuki.
Labda mi Ndenge ya cash money zilizotoka bila utaratibu tuliozoea
 
Hivi mtu kama Lissu anaweza kukosoa swala la serikali kuhamia dodoma? wagogo na wanyiramba watamuelewa?
 
Hivi mtu kama Lissu anaweza kukosoa swala la serikali kuhamia dodoma? wagogo na wanyiramba watamuelewa?
Hilo LA Dodoma ni wazo tangu enzi za Nyerere,yawezekana kama Magu asingelifanya labda Rais ajaye Ndugu Lissu angelitimiliza
 
Hilo LA Dodoma ni wazo tangu enzi za Nyerere,yawezekana kama Magu asingelifanya labda Rais ajaye Ndugu Lissu angelitimiliza
Kama mimi ningekuwa Rais ajaye wazo hilo ningelitupilia mbali kabisa, badala yake ingetumia robo ya hela ya kuhamia dodoma kujenga na kuboresha mifumo ya mawasiliano ya habari, tehama, usafiri na usafishaji ili watu waweze kuhudumiwa hukohuko waliko bila kulazimika kusafiri kwenda makao makuu ya wizara. Na kama ulazima upo basi wangetumia train za mwendo kasi, ndege na barabara za lami nchi nzima. Kama serikali yote iko sehemu moja itakuwaje wakati wa milipo ya magonjwa kama covid 19?

Wakati Nyerere anatoa wazo hili la dodoma technologia ya mawasiliano ilikuwa duni sana iliyomlazimu mtu kwenda ofisini kuhudumiwa.
 
CHADEMA itashinda kwani wananchi kwa kweli wamechoshwa na yanayoendelea sasa, hali ya uchumi imekuwa ngumu sana.
Ni ngumu kweli kweli hasa kwa watui ambao ni wavivu hawajishughulishi. Lakini wewe unasema hapa hali ngumu lakini jirani yako anainuka na kujishughulisha anatoba. We unabaki kusema hali ngumu. TUCHAPE KAZI WATANZANIA.
 
Kila kitu kinachosemwa na kufanywa na wanasiasa katika kipindi hiki Cha uchaguzi faida na hasara itakwenda kwa wananchi wa kawaida, hivyo wanasiasa tuchunge ndimi zenu na vitendo vyenu kwenye majukwaa.

Kwa vyovyote vile sisi wananchi tunapenda kusikia wagombea wakisema namna watakavyotupatia haya kama tukiwachagua:

1. Usalama na amani
2. Maji ya kunywa na umwagiliaji.
3. Afya kwa wote
4. Elimu kwa wote
5. Chakula kwa wote
6. Umeme kwa wote
7. Uchumi wa majumbani sio wa takwimu
8. Miundombinu ya Usafiri na usafirishaji
9. Utawala wa sheria
10. Utengamano na nchi jirani na kimataifa.
11. Uboreshaji wa Michezo na Sanaa.
12. Utunzaji wa mazingira na ukuzaji wa utalii

Wananchi tungependa kuwasikia mnasema Nini kuhusu mtakavyotupatia vitu hivyo kwa njia bora zitakazozingatia utu wetu, uhai wetu, mila zetu, utamaduni wetu, Uhuru wetu, muungano wetu, na demokrasia yetu bila kuwasahau nchi majirani.

Hatuhitaji kusikia Sera za kutaja na kulaumu watu, vyama, na taasisi mbalimbali.

Mwanasiasa atakaefanya siasa za maji taka bila shaka atashindwa uchaguzi kabla ya uchaguzi haujafanyika
Hakika nimependa sana andiko lako hili. Wanasiasa wasitusukume katika matakwa yao wao lakini sisi Watanzania tuwe na malengo fulani, tujue mtu anaetakiwa kutuongoza awe na maoni fulani kwa maendeleo ya taifa letu sio kila kukicha vurugu.
 
ngumu kweli kweli hasa kwa watui ambao ni wavivu hawajishughulishi. Lakini wewe unasema hapa hali ngumu lakini jirani yako anainuka na kujishughulisha anatoba. W
Sisi Tunataka kushughulika kwa faida siyo hasara.
Hakuna jirani hata mmoja anayetoboa zaidi ya Magufuli na ndugu zake.
 
Ni ngumu kweli kweli hasa kwa watui ambao ni wavivu hawajishughulishi. Lakini wewe unasema hapa hali ngumu lakini jirani yako anainuka na kujishughulisha anatoba. We unabaki kusema hali ngumu. TUCHAPE KAZI WATANZANIA.
Mkopo wenye riba ya 20% utatoboa vipi? ndio maana wanaotoboa wengi wanakwepa kodi ya TRA. Pamoja na riba kubwa pia umudu matumizi ya nyumbani, matibabu, pango, umeme, maji, elimu za watoto, wazazi na tegemezi, rambirambi, usafiri, michango ya kijamii, nk. huyo mtu atatoboa kivipi? Watu wengi wanatoboa kwa kukwepa kodi, kunyima familia mahitaji ya lazima, kutowapeleka watoto vyuoni,
 
Ndugu yangu nikushauri kitu kimoja, Kama unaogopa Mikopo basi hautaweza kutoboa, Mkopo ukichukia hakikisha unajambo la kufanyia lakini ukichukua mkopo hujajipanga matokeo yake Mjomba akijua unahela atakwanmbia binamu yako hana sare za shule utatoa, Mchango wa harusi utatoa, sijui msiba unatoa hapo, unataka bia moja au kuku unatoa hapo, ikifika jioni upo kitandani ukiangalia 100,000 uliyokopa uanze biashara ya karanga itakua imebaki 20, na bado hujanunua surwale nzuri hapo hapo na Mwajuma hujampa ya salon.

Jiungeni katika Vikundi vya vijana, wasomi ni wengi sana kila kona ya nchi hii, mkikutanisha mawazo yenu yupo mtaalam wa kuandika andiko la kuwapa fedha, mwingine atasema baba anashamba kubwa tukimuomba heka moja tuweke banda la kuku hata kataa. thena mnaanza taratibu na mtatoka ila kubwa zaidi ni nidhamu ya fedha ya Mkopo na ile ya mradi inahitajika sana. Hata nidhamu ya mshahara. Maana yupo mtu ambaye mnapokea nae 120,000 lakini mwingine anafika tar 23 mwingine hamalizi nao siku 7 anaanza kulia.
 
Back
Top Bottom