Uchaguzi 2015; ccm watakubali matokeo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi 2015; ccm watakubali matokeo?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by muonamambo, May 21, 2011.

 1. muonamambo

  muonamambo JF-Expert Member

  #1
  May 21, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Nimekuwa nafuatilia kwa ukaribu chaguzi mbalimbali Tangu zile za 2005 na 2010 na kuona mbinu chafu zinazotumiwa na chama Tawala CCM tangu wakati wa kampeni, kwenye tume ya uchaguzi, wakati wa kupiga kura na hata kutangazwa kwa matokeo. Mbinu hizi zikiwa pamoja na kuwaenguwa wapinzani kwa kusingizia sio raia, kuchelewesha kufungua kwa vituo, kurubuni mawakala, kupenyeza kura zisizo halali, kutishia wapiga kura, kushinikiza tume za chaguzi kutangaza matokeo ya uongo nk.

  Napotazama muelekeo wa siasa na kuanza kwa kampeni mapema zaidi na kuonekana kutokukubalika kwa chama tawala; hasa baada ya kuacha kazi ya msingi ya kuwaletea Watanzania maendeleo na kujikita kwenye siasa mapema zaidi kabla ya wakati wa uchaguzi. Napata mashaka kama CCM watakubali matokeo ikitokea kuwa wameshindwa kama walivyo fanya chaguzi zilizopita.

  Nipeni maoni yenu wana JF je mnadhani CCM watakubali matokeo kirahisi pale watakaposhindwa?
   
 2. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #2
  May 21, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  ili kuepusha machafuko lazima muundo wa tume ya uchaguzi uangaliwe upya, means ni vizuri katiba mpya iwe tayari b4 2015. Otherwise ccm wakichakachua tena hapatatosha coz wananchi wanaanza kuelimika na kujua umuhimu wa kuwa na viongozi wanaowataka afu kumbuka vijana wengi watapiga kura huo mwaka sababu washaona umuhimu na wengi wamepata kamwanga from shule za kata, so hawatadanganyika kwa t shirt, khanga na show za zekomedi. ingawa bado ni wahanga wa mfumo duni wa elimu so jazba juu! Na matokeo yakichakachuliwa patience yao ni ndogo kuna mtiti watu watadai viongozi wao ka ilivyotokea arusha na mwanza 2010
   
Loading...