Uchaguzi 2010 na Uraia wa Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi 2010 na Uraia wa Tanzania

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Asprin, Aug 23, 2010.

 1. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,050
  Likes Received: 23,825
  Trophy Points: 280
  Ndugu zangu watanzania wenzangu (kama kweli mi ni mtanzania kwa mujibu wa CCM)

  Uchaguzi wa mwaka huu umegubikwa na wimbi la watu waliokuwa wanajijua kuwa ni watanzania kumbe kwa mshangao wao wanajikuta kuwa si watanzania.

  Kuna mmoja aliyekuwa anataka kugombea ubunge kupitia CHADEMA huko Mwanza aliwekewa pingamizi na Waziri Lawrence Masha na pingamizi hilo kukubaliwa. Amenifanya nipate uchungu na kuanzisha sredi hii ili wajuvi mnisaidie

  Binadamu huyu amezaliwa Tanzania Miaka 33 iliyopita. Hajawahi kuishi nje ya Tanzania. Baba yake ni mtanzania aliyezaliwa Tanzania. Baba wa baba yake (babu) ni mtanzania aliyezaliwa Tanzania. Ila mama yake ni mzaliwa wa Kenya aliyekulia Tanzania.

  Kinachonigongeshaa kichwa:
  Baba anapokuwa raia wa Tanzania na mama si raia, na mtoto kazaliwa na kukulia Tanzania mtoto anakuwa raia wa wapi?
  Kama mtoto anakuwa si raia wa Tanzania, anapaswa afanye nini ili awe Raia wa Tanzania?
  Mwenye mamlaka ya kumtangaza mtu kuwa ni raia wa Tanzania ni nani?
  Je uraia wa mtu unagundulika tu pale anapogombea nafasi za uongozi wa kiasiasa?

  Naomba msaada wenu, nina mpango wa kuikomboa nchi hii mwaka 2015 sasa nahofia nisije kukomboa nchi isiyo kuwa ya kwangu.
   
 2. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  sijui viongozi wanategemea tujijue vipi uraia wetu ikiwa wakati tunapojiandikisha shule, vyuo vikuu, mikopo ya serikali, kote huku hatujaambiwa kama kuna uwezekano wa sie kuwa si raia.

  wangeliweka sheria basi kuwa ukitimia miaka 18 lazima ukathibitishwe uraia wako na upewe ushahidi wa kuwa raia (japo hili linaweza lisisaidie ccm wakikusudia kusema weewe si raia)
   
 3. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,050
  Likes Received: 23,825
  Trophy Points: 280
  Kila alipopita alikuwa anajitambulisha kama mtanzania na haikuwa nongwa. Inakuwaje anaonekana si raia wa nchi hii kwa kuwa tu kawekewa pingamizi na Waziri wa Mambo ya Ndani? Hivi mtu unatakiwa uonyeshe nyaraka zipi ili uthibitishe uraia wako?:confused2::confused2::confused2:
   
 4. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ushindi ni lazima! Hii ndiyo kauli mbiu ya CCM mwaka huu, wao ndo wameshikilia serikali, Masha ndiye waziri mwenye ridhaa ya mambo ya ndani ambayo ndiyo inasimamia idara ya uhamiaji. Sikushangaa kuona kuwa anatumia madaraka yake kuwaamuru wasaidizi wake (Uhamiaji) wahakikishe kuwa mpinzani wake anatafutiwa zengwe lolote lile. Kama siyo raia je kwa nini hajakamatwa na kurudishwa kwao kama sheria ambayo Masha na wizara yake wanatakiwa kuisimamia?????

  Ombi langu kwa wananchi wa Ilemela na Mwanza ni kutomchagua mgombea yeyote wa CCM. Kwa sababu moja kuu kuwa serikali ya CCM imeshindwa kusimamia utawala wa sheria na hivyo kusababisha wageni kutumia rasimali zetu kadri wapendavyo.
   
 5. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #5
  Aug 23, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  hiyo nchi inayoitwa tanzania kwani inaendeshwa na sheria?

  wanatakiwa wawe na mfumo ambao mtoto anaezaliwa na mzazi mmoja asiye kuwa raia, wampe notification akifika miaka 18 achague uraia wa nchi anaoutaka.....................sio wanaenda wanamu ambush mtu tu

  ati waziri akisema wewe si raia maana yake wewe si raia.
   
 6. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #6
  Aug 23, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Tena wamesema ushindi wa kishindo ni lazima kwa gharama yoyote!
  mix with yours
   
 7. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #7
  Aug 23, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,050
  Likes Received: 23,825
  Trophy Points: 280
  Huwa sina hasira kwenye haya mambo ya siasa. Ila hili la Masha kwakweli limeniudhi.

  I HATE LAWRENCE MASHA:confused2::welcome:
  I HATE CCM na viongozi wake wote, na wanachama na mashabiki wake wote..........:mad2::mad2:

  :banplease::banplease::banplease:
   
 8. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #8
  Aug 23, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,050
  Likes Received: 23,825
  Trophy Points: 280
  I hate Lawrence Masha! I hate Tanzania (After all, sina uhakika kama mimi ni mtanzania kwa mujibu wa Serikali ya Tanzania ya CCM ya JK
   
 9. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #9
  Aug 23, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,050
  Likes Received: 23,825
  Trophy Points: 280
  Ushindi wa Kishindo si ndo huu wa kutumia vigezo vya uraia? Wameona wizi kwenye visanduku vya kura mwaka huu itakuwa ngumu, kwa hiyo wamekuja na mbinu mpya.......... URAIA!!

  Can you imagine? Pingamizi zote walizowekewa CCM zinatupwa kapuni. Mohamed Dewji huko Singida kawekewa pingamizi na wagombea wawili wa upinzani pingamizi zimetupwa. Yeye kawawekea pingamizi wagombea wote wa upinzani na pingamizi zote aliaoweka zimekubaliwa..... Naye AMESHAKUWA MBUNGE TAYARI.........Damn it!
   
 10. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #10
  Aug 23, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  mtu wa ngapi sijui huyo anatajiwa uraia kisa kagombea ubunge!

  ikiwa wanafanyiana wenyewe kwa wenyewe ccm watashindwa kumfanyia mgombea wa upinzani?

  ushaambiwa ccm imesema itashinda kwa kishindo kwa gharama yoyote ......wategemea nini?
   
 11. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #11
  Aug 23, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,050
  Likes Received: 23,825
  Trophy Points: 280
  Namshukuru Mungu silaha haziuzwi kama pipi Kariakoo. Kuna mtu angeenda Jehanam wakati mimi naelekea Segerea kusubiri signecha ya rais wa CCM nining'inizwe kitanzini!:confused2::confused2:
   
 12. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #12
  Aug 23, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  nchi ilivyokuwa haina sheria na tushukuru tu hakuna silaha nje nje .............manake tungemalizana japo kuwa sasa hao elite few wanatumaliza raia wa chini kwa madhila :mad:
   
 13. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #13
  Aug 23, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,050
  Likes Received: 23,825
  Trophy Points: 280
  Haya hebu turudi darasani kidogo hapo.......:confused2:
   
 14. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #14
  Aug 23, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,649
  Likes Received: 1,473
  Trophy Points: 280
  Hommie, hivi wewe ni raia in the first place? tuanzie hapo


  Inaonekana suala la uraia wa nchi yetu ni privilege na sio right ya mtu.. kwa wale tulioshuhudia suala la Bashe, hili la Masha ni cha mtoto tu!:confused2:
   
 15. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #15
  Aug 23, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  hahaha dont tell me! mpwa nna wasi wasi na urai wako.....
   
 16. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #16
  Aug 23, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Kwani mbona hata Masha wenu huyo si Mtanzania.... Mwambieni athibitishe muone
   
 17. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #17
  Aug 23, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,649
  Likes Received: 1,473
  Trophy Points: 280
  Halafu sasa, huyu msimamizi wa uchaguzi bwana Kabwe alidai kwamba mgombea wa CHADEMA kashindwa kuthibitisha uraia wake......lakini mbona hajatuambia kuwa ni vielelezo gani vinamfanya asiwe raia? alikutwa na pasipoti ya nchi nyingine? ana fanana fanana na msomali? au ni kipi hasa KINACHOTHIBITISHA kuwa sio raia hadi aenguliwe kwenye kugombea?

  kijana chakarika na rufaa hadi kieleweke!:confused2:
   
 18. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #18
  Aug 23, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  System nzima ya CCM inaboa sana ..swala zima hapa ni kwamba hawajiamini hata kidogo ..wamekuwa wakiishi kwa hofu ,mashaka na kuotea. maisha yao ..wana hofu kubwa na upinzani
   
 19. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #19
  Aug 23, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,050
  Likes Received: 23,825
  Trophy Points: 280
  Nyie watu, haya maswali na utata wa uraia wangu hebu nendeni kwa mtaalamu wa kutambua uraia marehemu, sore, mheshimiwa Masha.
   
 20. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #20
  Aug 23, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,050
  Likes Received: 23,825
  Trophy Points: 280
  Taratibu mtumishi.......Hatupendi kukukosa bana. Yaani huyu raia namba moja wa Tanzania unasema si mtanzania?:confused2:
   
Loading...