habari zenu ndugu zangu watanzania, natoa shukrani za dhati kwa wote wlioniomba niwatumie kitabu je tumwambie rais?pia nashukuru kwa maoni yote ya wachangiaji wa mada nilioitoa, ingawa kuna alieniuliza kwa kejeli kama siogopi kufa kwanini nilikimbia?napenda kuwakumbusha ya kwamba kukimbia si kuogopa kwani historia inatufundisha ya kwamba wanamapinduzi wa kweli hukimbia na kujipanga vizuri kisha hurudi, mfano fidel castro alikimbilia argentina na kukutana na akina che guevara na badae alirudi na kujificha santiago kisha akafanikisha mapinduzi, mahatma gandhi alikimbia afrika kusini, nae vladimiri ilich lenin wa urusi alikimbilia ujerumani na badae wakafanikisha mapinduzi ya wa bolsheviki 1917, hivyo basi nasisitiza ya kwamba mapinduzi yataendelea nikiwa hai au mfu kwani mi sio wa kwanza kukumbwa na mikasa hii.
Ombi langu leo ni kwamba jamii forums ianzishe foundation ambayo itatuunganisha kwa vitendo ili tuikomboe nchi yetu, nimegundua sisi wana jf tuna upeo wa hali ya juu na pia mungu katuwezesha ili tuisadie jamii ya watanzania ambao wengi wao bado wamefunikwa na giza la ujinga, umasikini na maraddhi,
uchaguzi huu uwe ni chanzo cha kutuunganisha popote pale tulipo duniani na kisha tuandae katiba yetu naamini kunawataalamu wengi hapa jf, na baada ya katiba tusajiliwe kisheria kisha tufungue akaunti bank yenye mtaji wa bilion 1 tsh, amabayo itumike kuanzisha miradi mbalimbali kwa mfano shamba la heka 200 likitumika vizuri kwa umwagiliaji tutaweza kuvuna zaidi ya tani 1500 za mchele na mahindi kwa mwaka kisha tutafute masoko nje ya nchi kisha pesa zingine zitumike kuanzisha miradi mingine kama migahawa ya jff katika miji mikubwa duniani kama vile nassau bahamas, newyork, washington na london, kisha tuuze bidhaa zetu za asili ambazo zitatuwezesha kupata pesa ambazo naamini kabisa utakuwa ndio mwanzo wa kufanya mapinduzi halisi.
jamii forums foundation itaweza fanya yafuatayo.
1.kuchapa nakala za mada mbalimbali zinazojadiliwa na kusisambaza katika maktaba mbalimbali nchini pamoja na mashuleni, pia kufadhili uandishi wa vitabu na makala mbali mbali za uzalendo, utawala bora pamoja na haki na wajibu wa wananchi.
2.kuanda makongamano na midahalo mbalimbali kuanzia shule za sekondari mpaka vyuo vya elimu ya juu.
3.kufadhili na kuwezesha tafiti mbalimbali ambazo zitafanywa kwa lengo lakuwafikia wana vijiji na kujua matatizo yao pamoja na kuwaelimisha njia sahihi za kutatua matatizo mbalimbali ya kijamii.
4, jamii forums foundation itaweza kuzalisha wataalamu na wazalendo wa kweli wenye uchungu na maslahi ya taifa lao ambao baadae watapata baraka za jff na kugombe nyanzifa mbalimbali na kisha tukifikia hatua hiyo hapo tutakuwa tumefanya mapinduzi halisi.
Naomba ifahamike ya kwamba kazi inayofanywa na jamii forums haina tofauti na kazi zilizofanya na akina socrates, aristato, plato, pythagoras, thales pamoja na wanafalsafa mbalimbali ambao walikua na upeo wa juu wa kufikiria ambao walikua wakijadili mambo mablimbali yanayo husu maendeleo ya watu na kuyafanya kwa vitendo na matokeo ustarabu ukatufikia hadi kizazi hiki.
Tutumia akili na uwezo aliotupa mungu kuwafumbua macho watanzania pamoja na kufanya kwa vitendo kama walivyofanya wa nihilist wafuasi wa lenin ambao walizunguka katia vijiji vyote vya urusi na kuhubiri mapinduzi ambayo yalifanyika na kuuangusha utawala wa akina tsar nicolas.
Dr slaa peke yake bila juhudi zetu hatoweza kutukomboa yatupasa kushirikiana na kuungana na kuwa na sauti moja kisha tutafika katika safari yetu ambayo tayari mimi nimeishaanza kukutana na vikwazo vyake ambavyo kwa njia moja au nyingine vinazidi kunikomaza na kunijenga zaidi kimapinduzi.
Mungu ibariki tanzania,mungu ibariki afrika.