wazanaki
JF-Expert Member
- Mar 20, 2020
- 1,092
- 804
Wakuu wakuu. Ninaandika kwa machungu na hasira sana. Hivi wakuu kwann hatuzingatii vitu vya msingi vyenye athari ya moja kwa moja kwenye jamii.
1. Uchomaji taka holela
Kuna watu huku mtaaani wanachoma taka inakua ni usumbufu. Maana moshi ni kuanzia asubuhi hadi jioni. Mbona kuna mitaa hapa dar ukifanya hivo unaingia matatizoni. Kwa mfano masaki huwezi fanya ujinga huo. Ukichafua hali ya hewa watu wanafika fasta unapigwa fine. Nilikua naomba kama kitengo cha mazingira. Basi iwekwe sheria ya uchomaji taka au kuwe kuna jalala kuu la kuchomea taka asee. Nafikiri pia sometimes watu wanaugua vifua kwa sababu kama hizi. Au kama vipi serikali iangalie njia zinazotumika kwa mataifa yalioendelea kuona wanavo monitor air pollution. Kwa kweli hali ya hewa dar es salaam ni chafu sana. Kuna kipimo cha air quality siku moja nilikua nacho nikapima nikakuta tunavuta hewa chafu sana.
2. Magari yanayotoa moshi mwingi
Wakuu haya magari yamekua ni tabu sasa. Yani magari yote yaliyokwisha yanatupwa tanzania kama jalala mwisho wa siku yanakuja kutuchafulia hewa. Traffic tanzania imefocus sana kwenye makosa mengine lakini kosa la gari kutoa moshi mwingi wala hata hawafatilii. Leo hii ukienda ulaya gari likitoa koshi utapigwa faini ya bei y ma kiwanja na jela utaenda. Ni kwa.ba watanzania tunathamini sana pesa kuliko afya au ni nn. Hali ya hewa ya dar sio nzui kabisa. Ukitaka kuamini uwe unatoka mkoani unaingia dar uone hewa ilivo nzito.
3. Viwanda ndani ya jiji
Wakuu. Ni kwa nn tunakua na maviwanda ndani ya residential areas, hii sio sahihi. Hata standard za viwanda haiko hivo. Ki standard, viwanda vinapaswa kukaa 60km kutoka residential area. Ndo maana matatizo ya magonjwa hasa ya mapafu hayaishi dar.
Niishie hapo.
Lakini kumbuka hii ni topic ya muhimu kati ya topic muhimu jamii forum